Askari Polisi wakifanya ukaguzi kwa maiti zilizokutwa eneo la ajali hiyo
Kaimu
kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Juma Bwire akizungumza na
waandishi wa habari katika eneo la tukio la ajali mbaya iliyotokea eneo
la kata ya Malolo manispaa ya Tabora ambapo watu wanne walikuwa
wamepanda basi hilo la kampuni ya Dont Worry ambapo lilisababisha ajali
hiyo baada ya kugonga treni ya mizigo,watu kadhaa wamejeruhiwa vibaya na
kulazwa hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete.
Eneo
la chini la basi hilo la kampuni ya Dont Worry ambalo lilisababisha
ajali hiyo ambapo mbali na uzembe wa dereva lakini basi hilo lililokuwa
likifanya safari zake kutoka Tabora mjini kwenda Ufuluma wilaya ya Uyui
limeonekana sehemu hiyo ya chini imefungwa kamba za mipira kuzuia vyuma
vinavyunganishwa na usukani visichomoke kitu ambacho ni hatari kwa
usalama wa maisha ya wasafiri.
Fundi wa mashine za Biometric Voters Registration (BVR) zinazotumika
kuandikisha wananchi kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura, Neema
Mbwambo akiirekebisha moja ya mashine hizo katika kituo kilichopo Shule
ya Sekondari ya Zawadi, Tabata Dar es Salaam jana. Picha na Venance
Nestory
Kwa ufupi
Mwananchi ilipita katika maeneo
mbalimbali jana na kushuhudia wananchi wengi wakiwa wamekutana na
changamoto kadhaa kwenye baadhi ya vituo ikiwamo ya kukosekana mashine
za Biometric Voters Registration (BVR).
By Waandishi Wetu
Dar es Salaam. Kasoro za
uandikishaji wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura zilizokuwa
zikitokea katika mikoa mbalimbali nchini, zimejitokeza pia jijini Dar es
Salaam ikiwa ni siku ya kwanza ya kazi hiyo.
Mwananchi
ilipita katika maeneo mbalimbali jana na kushuhudia wananchi wengi
wakiwa wamekutana na changamoto kadhaa kwenye baadhi ya vituo ikiwamo ya
kukosekana mashine za Biometric Voters Registration (BVR).
Wananchi
hao walisema licha ya kwamba Dar es Salaam imepewa siku 10 ya
uandikishaji, kama changamoto hizo hazitachukuliwa hatua kazi hiyo
inaweza isikamilike kwa wakati.
Miongoni mwa changamoto
nyingine ni kuharibika kwa mashine zilizopo, ukosefu wa umeme, uchache
wa watendaji na kuelemewa na watu, mtandao usio wa uhakika na nani aanze
kuandikishwa kati ya wenye mahitaji maalumu na wasionayo.
Katika
kituo cha uandikishaji cha Shule ya Msingi Oysterbay ambako kuna vituo
vidogo vitano, wakala wa uandikishaji, Margereth Galway alisema mwitikio
wa vijana umekuwa mkubwa kiasi kwamba inakuwa shida kuwapa nafasi ya
upendeleo wazee, viongozi, walemavu au wajawazito na wanaonyonyesha.
“Eneo
hili lina wazee na viongozi wengi wa chama na Serikali. Mwitiko mkubwa
wa vijana unatufanya tushindwe kuwasaidia watu hao,” alisema Galway.
Alisema
wasimamizi wote wa kituo hicho wamekubaliana kuwa kuanzia leo, wateue
mashine moja na itengwe kwa ajili ya wenye mahitaji maalumu ili
kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi wanaokuwa wamesimama kwenye
foleni muda mrefu.
“Tayari wameshakuja Warioba (Jaji
Joseph), Msekwa (Pius) na Butiku (Joseph) wakiwa na wake zao na
kujiandikisha. Pamoja na kufahamika kwao bado vijana hawakuwa radhi
kuwapisha wakitaka wajipange jambo ambalo ni gumu kulitekeleza.
“Kama
tutafanikiwa kuwashawishi waandikishaji basi foleni za watu wa kawaida
zitakuwa nne na moja itaachwa kwa ajili ya wenye mahitaji muhimu,”
alisema.
Katika Kituo cha Shule ya Msingi Kawe A, wazee
wengi walikutwa wamekaa kwenye madawati, nje ya madarasa wakisubiri
kuandikishwa baada ya vijana kutokubali kuwapisha wakidai waandaliwe
utaratibu ambao hautoingilia foleni iliyopoo.
Katika
Shule ya Msingi Hekima iliyopo wilayani Kinondoni, kulikuwa na
malalamiko kama hayo na wananchi wakaiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) kuweka utaratibu maalumu.
Mmoja wa waliofika
kujiandikisha, Mwanaidi Abdallah alisema katika uandikishaji huo
wanawake wamekuwa wakipata shida kutokana na utaratibu mbovu.
Alisema inachukua muda mrefu kupata huduma kwa sababu baadhi ya vijana wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kujiandikisha.
Katika
kituo cha Mtendaji kilichopo Mtaa wa Mzimuni, Kata ya Kawe, wananchi
walikutwa wakiwa nje saa 8:00 mchana wakisubiri mashine ili uandikishaji
uanze licha ya kutangaziwa kazi hiyo ingeanza asubuhi.
Kitu
pekee kilichokuwa kinaendelea ni wananchi kujiorodhesha kwenye daftari
na kupewa namba ya foleni hadi mashine zitakapoletwa.
Mkazi
wa Ununio Beach, Joseph Mrisho alisema licha ya wananchi kujitokeza kwa
wingi kuna vituo viwili mashine ziligoma kufanya kazi.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Ununio Beach, Mwijuma Mwinyihija alisema
usumbufu waliokumbana nao wananchi umesababisha malalamiko na wengine
wamekataa tamaa na kuamua kuondoka kwenda kwenye shughuli zao za
kujitafutia kipato.
Katika Kata ya Wazo Mtaa wa
Salasala eneo la IPTL, hadi saa 9:00 alasiri wananchi walikuwa
hawajaandikishwa kutokana na mashine kugoma.
Mkazi wa
eneo hilo, Blandina Hizza alisema alilazimika kurudi nyumbani mara
kadhaa akijipa matumaini huenda mashine hiyo itatengemaa ili
aandikishwe, lakini hadi muda huo hakufanikiwa.
Frank Etta alisema: “Hatuelewi imekuwaje hadi sasa wahusika hawajaleta mashine.”
Kituo
cha Shule ya Msingi Mlimani kilichopo katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam ambacho kinastahili kuwa na vituo vidogo vitatu, kina mashine
moja tu iliyopelekwa.
Mwandikishaji Msaidizi katika
kituo hicho, Isabella Mkumbwa alisema mwitikio wa watu ni mkubwa, lakini
uandikishaji unakwenda taratibu kwa sababu watu wote wanatakiwa
kusubiri mashine moja.
“Baadhi ya watu wameondoka ili
wakaendelee na kazi zao. Tunasubiri mashine nyingine mbili ziongezwe
wakati tukiendelea kuitumia hii iliyopo,” alisema msimamizi huyo.
Kituo
cha Shule ya Sekondari Zawadi kiliyopo Tabata, uandikishaji ulikuwa
haujaanza hadi saa 4:00 asubuhi wakati gazeti hili lilipotembelea
kituoni hapo na kukuta mashine ikitengenezwa.
“Niliwahi
kufika na nikapewa namba 23 ila tumeelezwa kuwa walimu wataanza
kuandikisha pindi mashine zitakapotengamaa. Wamesema kuwa zimegoma
kutokana na mtikisiko wa kusafirishwa kutoka mikoani,” alisema James
Mwandumbya aliyefika kujiandikisha.
Maeneo ya Pugu
Kigogo Fresh (Stesheni) waandikishaji walielemewa na wingi wa watu na
kulazimika kutoa namba ili wengine waende siku nyingine.
Katika
kituo cha Shule ya Msingi Mtambani, Kinondoni, wananchi walilalamika
gharama za uendeshaji ambazo wameombwa wachangie ili kufanikisha
uandikishaji uendelee kama ulivyopangwa.
Katika Kituo
cha Shule ya Msingi Makuburi, Ofisa mwandikishaji, Karim Mweneghoha
alisema walikumbwa na changamoto ya umeme iliyochangiwa na kukosekana
kwa waya za kuunganisha kutoka kwenye soketi kwenda kwenye mashine.
Mkurugenzi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Julius Mallaba alikiri kupokea taarifa
kutoka katika baadhi ya maeneo na kudai kuwa tayari ufumbuzi
umepatikana.
“Kuna taarifa nilipokea asubuhi kwamba
uandikishaji unaendelea, ngoja niwasiliane na ofisa uandikishaji ili
nijue (changamoto) ndipo niweze kuzungumzia vyema jambo hili,” alisema.
Awali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambayo ndiyo inahusika na
shughuli hiyo ilisema mashine zaidi ya 8,000 zitatumika ili kufanikisha
shughuli hiyo baada ya kukamilika uandikishaji mikoani.
Imeandikwa na Beatrice Moses, Julius Mathias, Bakari Kiango na Colnely Joseph. Habari toka: http://www.mwananchi.co.tz
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia katika mkutano wa
hadhara uliofanyika Magomeni, jijini Mwanza jana. Picha na Michael
Jamson
Kwa ufupi
Akihutubia mkutano wa hadhara katika
Viwanja vya Magomeni jijini hapa, Mbowe aliwaomba wananchi kuuvumilia
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa sababu viongozi wake wanaendelea
na majadiliano na watakapokubaliana watamtangaza mgombea wao.
By Waandishi wetu
Mwanza/Dar. Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe amesema chama chake kimeshindwa kumtangaza
mgombea wake wa urais kama ilivyotarajiwa jana, badala yake kikawaomba
Watanzania kutokuwa na haraka, wasiwasi wala mihemko na kuwa muda
ukifika kitamtangaza.
Akihutubia mkutano wa hadhara
katika Viwanja vya Magomeni jijini hapa, Mbowe aliwaomba wananchi
kuuvumilia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa sababu viongozi wake
wanaendelea na majadiliano na watakapokubaliana watamtangaza mgombea
wao.
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar),
Salum Mwalimu alisema ilikuwa wamtangaze mgombea urais kama
ilivyoripotiwa na gazeti hili, lakini wenzao wa CUF wamewaomba kuwa
wanaendelea na vikao vyao vya chama.
Naibu Katibu Mkuu
wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema: “Wengi wana hamu ya kutaka kujua
mgombea urais wa Chadema, naomba niseme kwamba tumekuja Mwanza kwa
mambo mawili, kuja kuwapokea makamanda hawa wawili na kuitokomeza CCM.
“Ukawa
itamsimamisha mgombea urais ambaye Oktoba lazima aiondoe CCM
madarakani, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Magdalena Sakaya) ametuomba tena
tusubiri hadi tarehe 25 (Jumamosi), kwani watakuwa na kikao cha Baraza
Kuu la chama hicho, hivyo tunawasubiri wenzetu.”
Mbowe
aliyetumia mkutano huo kuwakabidhi kadi wanachama wapya waliotoka CCM na
kujiunga Chadema, Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mbunge wa Viti
Maalumu, Ester Bulaya, aliweka msisitizo:
“Muungano
wetu wa Ukawa ni wa msingi sana, kuna changamoto, tunaomba wananchi muwe
wavumilivu, tuache mihemko ili tufikie uamuzi sahihi.
“Tunaomba
mtuvumilie, hatuwezi kumtangaza mgombea wetu kwa sababu tu CCM
wametangaza wa kwao, hapana! Tutamtangaza mgombea wetu na nyote
mtafurahi,” alisema Mbowe huku akishangaliwa na maelfu ya wananchi.
Alisema,
Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi alikuwa ahudhurie mkutano huo
lakini kutokana na foleni za Dar es Salaam alishindwa kuwahi ndege na
kwamba, viongozi wengine wa CUF na NCCR Mageuzi walialikwa lakini
walikuwa na vikao vya vyama vyao.
Mbowe alisema Ukawa
ni mpango wa wananchi, siyo wa viongozi na kwamba ulianzishwa Dodoma na
viongozi wote wa upinzani na Kundi la Wabunge 201 wa Bunge Maalumu la
Katiba walihudhuria, lakini baadhi yao walipenyezewa ‘kitu kidogo’
wakaondoka hivyo kubaki vyama vinne vya siasa.
Udini, ukabila wamkera
Mbowe
alionyesha kusikitishwa na kauli alizodai kutolewa na viongozi wa CCM,
kumnadi mgombea wao kwa ukabila na kuwataka wananchi kuwakataa
wanaotumia mbinu hizo kwani hali hiyo inaweza kusababisha machafuko.
“Nafurahishwa
sana na kauli zinazotolewa na viongozi wa CCM, tunampata kiongozi kwa
ukabila! Ukawa hatutamchagua mgombea wetu kwa misingi ya ukabila wala
udini, huo ni upumbavu,” alisema Mbowe na kuongeza:
Alisema Watanzania wanataka mabadiliko na kwamba hali hiyo imeshuhudiwa wakati wa uandikishaji wa daftari la wapigakura.
Aonya wizi wa kura
Mbowe
alisema hawatakuwa na tatizo iwapo ushindi utapatikana kwa njia za
haki, lakini hawatakuwa na suluhu iwapo utatumika wizi wa kura
kumuingiza mgombea madarakani.
“Hatutapiga magoti na
kuomba, kama ushindi utapatikana kwa njia halali hatuna tatizo, lakini
tukiona mambo yanakwenda ndivyo sivyo tunasema polisi mtatusamehe,
mabomu hayatatosha,” alisema Mbowe.
Lembeli, Bulaya waombewa msamaha
Mbowe alisema Chadema kina maadili yake na kwamba Lembeli na Bulaya waliokuwa CCM wametenda mengi lakini anawaombea msamaha.
“Naomba muwasamehe. Wangapi wanasema tuwasamehe?” alihoji Mbowe huku akiitikiwa kwa sauti, “Woteee”.
Alisema viongozi hao ni miongoni mwa wengi wanaokaribia kutimka CCM na kuwapongeza kwa ujasiri wao makini walioonyesha.
Aahidi kutaifisha viwanja vya CCM
Baada
ya kueleza jinsi alivyompigia simu bila mafanikio Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo kuomba kutumia Uwanja wa CCM Kirumba kwa
ajili ya mkutano huo, Mbowe alisema Serikali ya Ukawa ikiingia
madarakani itahakikisha viwanja vyote vilivyojengwa na wananchi
vinavyohodhiwa na CCM vinarejeshwa kwenye halmashauri.
“Chadema
kwa kushirikiana na Ukawa, viwanja vyote vilivyojengwa na wananchi
vitarejeshwa kwenye halmashauri ili vitumiwe na wananchi wote,” alisema
baada ya baadhi ya wanawake kuzidiwa na kuanguka kutokana na wingi wa
watu na ufinyu wa uwanja wa Magomeni.
Wagombea kulishwa yamini
Katibu
Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa aliwata wagombea ubunge
waliopitishwa ambao wana mawazo ya kuuza nafasi zao kwa CCM kujiengua
mapema kabla chama hakijawachukulia hatua.
Pia, Dk Slaa
alisema chama hicho kitatoa fomu maalumu ambazo zitasainiwa na wagombea
ubunge mahakamani ili kiweze kuwachukulia hatua za kinidhamu
watakaokwenda kinyume na taratibu za chama hicho.
“Majimbo
157 yamekamilisha leo (jana), sisi Chadema hakuna jimbo ambalo mgombea
atapita bila kupingwa kama wanavyofikiri CCM,” alisema Dk Slaa na
kuongeza:
“Tutatoa fomu za uteuzi ambazo wote
waliopitishwa kugombea ubunge watasainishwa mahakamani, naomba niseme
atakayeuza jimbo atashughulikiwa, kama mtu anataka kujitoa ajitoe
mapema.”
Dk Slaa alisema miaka 10 iliyopita wananchi
waliahidiwa maisha bora kwa kila Mtanzania, lakini yamegeuka na kuwa
kinyume, sasa ni maisha magumu kwa kila Mtanzania.
“Waswahili
wanasema ukiumwa na nyoka hata jani likikugusa unakimbia, miaka 10
mliahidiwa maisha bora kwa kila Mtanzania, leo ni maisha magumu kwa kila
Mtanzania. Cha kwanza tunachokisimamia Chadema ni kurudisha nchi kwa
wananchi, CCM wamepoka madaraka ya wananchi na kuyaweka mikononi mwa
wachache, tunawaambia mwisho wao ni Oktoba,” alisema Dk Slaa.
Lembeli afunguka
Akizungumza
kwenye mkutano huo, Lembeli alisema: “Nakumbuka tarehe 16 nilisali
nikiwa kijijini kwetu na mama yangu mzazi, nikamwomba Mungu anitoe nchi
ya laana anipeleke nchi ya matumaini.
Tarehe 17 nikafanya uamuzi, sasa nipo uwanjani, naomba niwaambie sijaja Mwanza hivihivi nimekamilika, nilipotoka nimeaga.”
Lembeli aliongeza: “Nimezoea kusema msemo wangu huu, hebu kunja ngumi... koroga... peoples,” umati wa watu uliitikia “Power”.
Kabla
hajahutubia, Lembeli alibisha hodi Mwanza kwa kusema: “Hodi…hodi,
aliitikiwa kwa sauti na umati uliohudhuria: “Karibu baba, karibu.”
Bulaya ampa salamu Wasira
Akihutubia
baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama, Buyala alianza kwa kuwauliza
wananchi: “Nikamtoe? Nauliza, nikamtoe? Nikamtoe nani?” wananchi
walijibu kwa sauti kubwa: “Wasira... kamtoe Wasira.”
Bulaya
alisema ni bora kama Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Stephen
Wasira anamsikia akaondoka kama alivyomshauri Makongoro Nyerere.
“Makongoro
Nyerere alisema, awamu ya kwanza upo, awamu ya pili upo, ya tatu upo ya
nne upo ya tano mwisho wake umefika sasa,” alisema Bulaya.
Alisema
kwa Mkoa wa Mara yupo mwenyekiti wake, Vicent Nyerere ambaye atafanya
naye kazi kwa karibu na kwamba yeye na wenzake wa Chadema ni muziki
mnene na jeshi kubwa.
Lissu na kabila la CCM
Akihutubia
kwenye mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu
aliwalinganisha, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Andrew Chenge
na Spika Anne Makinda kwamba hawana tofauti na mgombea urais wa CCM, Dk
John Magufuli, kwa sababu wote ni kabila moja la CCM.
“Nimefanya
mikutano mingi, kila mahala nilipokwenda nilikuwa naambiwa Dk Magufuli
kabila lake ni Msukuma, wengine Msubi na wapo waliosema Mzinza, mimi
naomba niwaambie kwamba kabila moja la CCM ndilo la Dk Magufuli,”
alisema Lissu.
Alisema Dk Magufuli ndiye aliyeuza
nyumba za Serikali nchi nzima, kauli ambayo ilitiliwa mkazo na Makamu
Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari ambaye alisema watumishi
wa umma wanaishi kwenye nyumba za vichochoroni kutokana na Dk Magufuli
kuuza nyumba za Serikali.
Mwenyekiti wa Baraza la
Wadhamini wa Chadema, Arcado Ntagazwa ambaye aliwahi kuwa waziri na
naibu waziri kwa miaka 15 alisema: “Safari hii kwa Chadema na washirika
wao wa Ukawa ni moja kwa moja Ikulu.
Goli la mkono laibuka
Ntagazwa alisema: “Mambo ya kusema goli la mkono, watambue kwamba Oktoba ndiyo mwisho wa ufisadi,”
Kauli
hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye alisema mwaka
huu goli la mkono litawageukia wao... “Wakijifanya wao ni watoto wa
kihuni makamanda wa Chadema ni wahuni zaidi yao.”
Kuhusu kucheza rafu, Mwalimu alisema wanaotarajia kucheza rafu kwenye uchaguzi mkuu ni wazi kwamba wameshindwa kucheza uwanjani.
“CCM
kutangaza kushinda hata kwa goli la mkono ni wazi kwamba wameshindwa
kucheza uwanjani sasa sisi tutawafuata hukohuko nje ya uwanja na
tutawabana,” alisema Mwalimu.
Wenje, Kiwia watamba
Mbunge
wa Nyamagana, Ezekia Wenje na Highness Kiwia, walisema kwa sasa wapo
likizo ya miezi miwili na wanatarajia kuapishwa tena kuwa wabunge baada
ya uchaguzi.
Kiwia alisema: “Mimi ndiye rais wa Jamhuri
ya watu wa Ilemela, sina shaka tumemaliza kura za maoni sasa nasubiri
tena kuwa Mbunge wa Ilemela.”
Akihutubia, Nyerere
ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini, alisema kazi inaendelea na
kinachofanyika sasa ni kuhakikisha CCM inaondoka madarakani Oktoba.
Leo viongozi hao wa Chadema watakuwa na mkutano mwingine mjini Mbeya na baadaye Arusha na Jumatatu ni Dar es Salaam.
Imeandikwa na Midraji Ibrahim, Aidan Mhando na Fidelis Butahe. Habari kutoka: Mwananchi
Wakili Paulo Kalomo mgombea ubunge jimbo la Ludewa
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo wilayani Ludewa kimeendeleana na mtifuano mkali katika
kumsaka mgombea mmoja wa ubunge wilayani hapa ambapo kila mgombea amekuwa
akipita huku na kule kusaka kura kwa wajumbe wa Chama hicho huku baadhi yao
wakituhumiana kutumia pesa zaidi.
Akiongea na
waandishi wa habari jioni ya leo Wakili Paulo Kalomo ambaye ni miongoni mwa
wagombea wa nafasi hiyo akitokea mwambao wa ziwa Nyasa alisema kuwa mpaka sasa
kuna wagombea wanne hivyo yeye amekuwa na mvuto zaidi kwa wajumbe hali ambayo
inawafanya wagombea wenzake kukata tamaa na kuwarubuni wajumbe.
Wakili
Kalomo alisema kuwa akifanikiwa kuchukua nafasi hiyo atakibadirisha chama cha
demokrasia na maendeleo wilayani Ludewa kwa kujijenga kuanzia vijijini hadi
ngazi ya wilaya hivyo amewataka wajumbe wa chama hicho kutorubuniwa na baadhi
ya wagombea katika kura za maoni zinazotarajiwa kupigwa leo tarehe 23/7/2015
katika makao makuu ya wilaya kwani yeye anamipango endelevu kwa wilaya ya
Ludewa.
Baadhi ya wazee wa wilaya ya Ludewa wakimpa baraka za mwisho za kuanza kugombea kwa awamu ya pili Mh.Deo Filikunjombe
Filikunjombe akisikiliza nasaha za Wazee
msafara wa kumsikindikiza kutangaza nia ya kugombea ubunge Deo Filikunjombe ukiingia viwanja vya mpira wa miguu Ludewa mjini
Filikunjombe akiwasalimia mamia ya wanachama wa ccm wilayani Ludewa ambao walikuja kumuunga mkono
wasanii wa kikundi cha IVA YOUTH GROUP ambacho ni kikundi cha uhamasishaji wilayani hapa wakifanya yaliyo yao
mamia ya washabiki wa ccm wakimraki Filikunjombe
Filikunjombe akiongea na wananchi wa wilaya ya Ludewa kata ya Ludewa mjini wakati akitangaza nia ya kugombea ubunge
msanii wa IVA youth Group Seleman Chikuti akionesha umahiri wake katika sanaa
Seleman Chikuti toka kundi la IVA youth group linalopatikana Ludewa
mjini akifanya vitu vyake wakati Deo Filikunjombe akitangaza rasmi nia
ya kugombea ubunge wa jimbo la Ludewa
Zaidi ya Wazee 300 wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wamefanya
maandamano ya kumuunga mkono mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo
Filikunjombe na kumchukulia fomu ya kugombea nafasi ya ubunge wa
jimbo hilo kwa awamu ya pili ili aweze kuliongoza tena kwa kauli ya
kuwa wameridhishwa na utendaji wake ambao hauna mashaka.
Akizungumza kwa niamba ya wazee wenzake mzee Laurent Mtweve alisema
kuwa jimbo la Ludewa limekuwa na umaarufu mkubwa wa kubadili
wabunge kila baada ya miaka mitano kutokana na utendaji
usioridhisha lakini safari hii hakuna haja tena ya kufanya hivyo
kutokana na mafanikio makubwa yaliyofanyika katika kipindi cha
Filikunjombe.
Mzee Mtweve alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2010 HADI 2015
wilaya ya Ludewa imepata mabadiriko makubwa katika kila sekta kwani
wakati mwingine Filikunjombe hakuweza kuisubiri bajeti ya Serikali
alilazimika kutoa fedha za posho yake ili kufanikisha na kutatua
matatizo yanayowakabiri wananchi wake.
Naye Bi.Mariam Nyandoa alisema kuwa katika moja ya kazi ambayo
Filikunjombe anapaswa kuendelea na uongozi ni ile ya kuhakikisha
kila hospitari,zahanati,dispensari kunakuwa na watumishi pamoja na
vitanda vya kujifungulia hali ambayo imekuwa ni kilio cha wanawake
wilayami Ludewa kwa muda mrefu.
Bi.Mariam alisema kuwa kwa sasa hakuna shida tena kama ilivyokuwa
awali kwani unapokwenda hospitari unauhakika wa kupata huduma nzuri
hivyo wazee wote wakaona wachange fedha za kumchukulia fomu ya
kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Ludewa na pia wanaandaa
sherehe ya kumpongeza kwa uongozi wake mzuri ambao ameuonesha.
"Sisi kama wazee katufanyia mengi katika kipindi cha uongozi wake
na yamekuwa ya mafanikio kwa wilaya ya Ludewa kumpata mbunge kijana
na ambaye anatumika akitumwa hivyo tunampango wa kumfanyia sherehe
licha ya kuwa tumemchukulia fomu hivyo hatuna mpango wa kuwa na
mbunge mwingine zaidi yake",alisema Bi.Nyandoa.
Akiongea na umati wa wananchi wa wilaya ya Ludewa katika viwanja
vya michezo Ludewa Mjini wakati akitangaza nia ya kungombea nafasi
ya ubunge Mh.Deo Filikunjombe alisema kuwa mafanikio yote
yaliyopatikana sio juhudi zake binafsi bali ni ushirikiano
alioupata toka kwa wananchi wa jimbo lake.
Filikunjombe alisema kuwa katika kipindi cha uongozi wake ni kweli
kumekuwa na mafanikio makubwa lakini wananchi ndio waliokuwa
wakimsukuma kufanya hayo na wakati mwingine alikuwa mkali Bungeni
kutokana na halia halisi ya ugumu wa maisha ya wananchi wa wilaya
ya Ludewa.
Alisema kuwa anamshukuru rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa
kuitendea haki wilaya ya Ludewa kwani katika kipindi cha uongozi wa
ke Ludewa imekuwa ikisikilizwa kupitia yeye hali ambayo
imeharakisha maendeleo wilayani Ludewa.
Anasema katika ubunge wake wa miaka mitano Ludewa imeweza kupata
kipande cha lami na hatimaye barabara za mitaa ya Ludewa mjini
zimeweza kung'ara kwa lami ikiwa ni juhudi zake kwani kabla ya
kuingia katika ubunge wilaya ya Ludewa haikuwa hata na kipande
kimoja cha lami.
Alisema kuwa licha ya Lami lakini barabara za vijijini vimefunguka
mfano barabara ya Lupingu ambapo kwa sasa kuna gari za abiria
zinafika huko wakati awali haikuwezekana pia barabara ya Mawengi
makonde ambako kwa sasa samaki wabichi wa ziwa nyasa wanafika
mapema Ludewa mjini.
Pia katika nishati ya umeme alivikuta vijiji vitatu vta
Mavanga,Mawengi na Ludewa mjini ndivyo vilikuwa na umeme lakini kwa
sasa kunamiradi ya umeme katika vijiji 67 ikiwa wilaya ya Ludewa
inajumla ya vijiji 77 hivyo anatangaza nia ya kugombea tena nafasi
hiyo ili aweze kukamilisha vijiji vilivyobaki.
Filikunjombe alibainisha kuwa wilaya ya Ludewa inatakiwa
kubadirishwa haraka na haya machache ambayo wananchi wanayaona kama
ni mabadiriko makubwa kwake ni machache sana kwani Ludewa imekuwa
nyuma kimaendeleo kwa miaka mingi hivyo katika mipango yake ya
ujenzi wa lami barabara kuu tayari Serikali imeshatoa fedha ya
kujenga barabara hiyo na awamu ya kwanza itajengo kilomita 50.
Alisema ujenzi wa barabara hiyo unaanza mapema mwezi ujao ambapo
Dkt.John Pombe Magufuli atakuja kabla ya kuanza ujenzi ili kujionea
mafanikio aliyoyafanya kwa wananchi wa wilaya ya Ludewa katika
sekta ya miundombinu na baadaye atakuja Rais Dkt.Kikwete kuweka
jiwe la msingi la ujenzi wa viwanda vya chuma cha Liganga na makaa
ya mawe Nchuchuma.
Aliwataka wananchi wa wilaya ya Ludewa kumuunga mkono mgombea wa
nafasi ya urais kupitia chama cha mapinduzi Dkt.Magufuli kwani ni
kiongozi makini na anayeipenda wilaya ya Ludewa kwa ni bila yeye
hata barabara za lami wilayani hapa tusingezipata hivyo wananchi wa
wilaya ya Ludewa wanahaki ya kujivunia kwa kuteuliwa Dkt Magufuli.
Filikunjombe alisema kuwa hivi sasa Serikali imepitisha bajeti ya
ujenzi wa daraja la mto ruhuhu ili kuunganisha wialaya ya Ludewa na
ile ya Nyasa hivyo wananchi wanatakiwa kujiandaa na fulsa ya
kibiashara watakayoweza kufanya na mkoa jirani wa Ruvuma.
Mwisho. Habari na: http://habariludewa.blogspot.com
Wanachama wa Chadema wilaya ya Mbeya Vijijini wakitoka nje ya ukumbi
baada ya msimamizi wa uchaguzi wa kura za maoni za kumpata mgombea
ubunge jimbo la Mbeya Vijijni kutokomea kusikojulikana wakati wa
kuhesabu kura jana na kusababisha uchaguzi huo kuvunjika. Picha na
Godfrey Kahango
In Summary
Lyimo alianguka baada ya
kupata kura 32 nyuma ya Mustafa Muro aliyepata kura 47. Wengine ni Rose
Moshi (8), Agrey Mkwama (6), Gemeral Kaduma (4) na Francis Nyerere (0).
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa alisema tayari
uchaguzi umefanyika katika majimbo matano.
By Waandishi Wetu, Mwananchi
Dar/mikoani. Kura za maoni
ndani ya Chadema zimeanza kuwa chungu kwa baadhi ya wabunge. Mbunge wa
Mbulu, Mustapha Akoonay na mwingine wa Viti Maalumu, Susan Lyimo
(Kinondoni) jana waliangukia pua, huku mwenzao wa Karatu, Mchungaji
Israel Natse akitangaza kuachana na ubunge na kurejea katika Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
“Jumatano (leo),
nitawaaga rasmi wananchi wangu, binafsi niliombwa na Dk (Willibrod)
Slaa kugombea jimbo hili kwa miaka mitano,” alisema.
Lyimo
alianguka baada ya kupata kura 32 nyuma ya Mustafa Muro aliyepata kura
47. Wengine ni Rose Moshi (8), Agrey Mkwama (6), Gemeral Kaduma (4) na
Francis Nyerere (0). Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa
alisema tayari uchaguzi umefanyika katika majimbo matano.
Alisema
Mbulu Mjini, kulikuwa na wagombea wawili, Akoonay alipata kura 108
dhidi ya 132 alizopata Diwani wa Mbulu, Michael Sulle.
Golugwa
alisema, Joseph Selasini ametetea nafasi yake katika Jimbo la Rombo
baada ya kupata kura 313 akiwaacha mbali wapinzani wake Ben Sanane
aliyepata kura 26 na wengine kura mojamoja.
Babati
Mjini, Mbunge wa Viti Maalumu, Paulina Gekur ameibuka kidedea kwa kura
88 akiwatupa nje wapinzani wake, akiwamo mkuu wa wilaya wa zamani,
Gabriel Kimolo na wenzake.
Mbulu Vijijini, Aman Gaseri alishinda kwa kura 76 huku Michael Aweda akipata 75.
Jimbo la Same Magharibi: Jonas Kadeghe alishinda kwa kura 68 akifuatiwa na Christ Mbanjo aliyepata kura 49 na Gervas Mgonja kura 30.
Muleba Kaskazini:
Najim Kasange alipata kura 247 na kumshinda mwandishi wa habari
mkongwe, Ansbert Ngurumo aliyepata kura 55. Mgombea mwingine, Christina
Mwainunu alijitoa.
Jimbo la Ukonga, Nickson Tugara
alishinda kwa kura 59 hivyo kuwaacha kwa mbali wagombea wenzake 14.
Alifuatiwa na Waitara Mwikwabe aliyepata kura 49, Elly Dallas (15),
Deogratias Munishi (8), Lucas Otieno (6), Asia Msangi na Deogratias
Mramba waliopata kura tano kila mmoja na Gasto Makwetta (1). Wengine
saba hawakuambulia kura hata moja.
Butiama:
Yusuf Kazi aliibuka kifua mbele baada ya kujikusanyia kura 202 na
kuwapiku Adam Taya (39) na Issa Yusuf (31), Daniel Obeiya (3), Annicent
Marwa (2) na Lucas Ossoo na Marto Yohana waliopata kura moja kila
mmoja. Nyamagana: Wenje aliibuka kidedea kwa kupata kura 194 na Patrick Masagati (32).
Msalala:
Paulo Ndundi alishinda kwa kura 113 akiwashinda Peter Machanga (49) na
Ezekiel Kazimoto (48). Wengine ni Emmanuel Mbise (43), Francis Makune
(15), Vincent Manoni Mhagwa (10) na Richard Mabilika aliyepata kura moja
na Stephen Bundala (0).
Sumbawanga:
Shadrack Malila aliibuka na ushindi wa kura 277 dhidi ya Kassian Kaegele
(28), Musa Ndile (9) na Matokeo Lyimo (1), Eliud Mwasenga na James
Kusula (0).
Nkasi Kusini: Alfred
Sotoka aliongoza kwa kupata kura 70 akifuatiwa na Kaminga Hyporito (39),
Emmanuel Sungura (9), Edson Ndasi (4) na Joseph Kitakwa (2).
Nkasi Kaskazini: Keissy Sudi alishinda kwa kura 158 na kufuatiwa na Triphone Simba (70) na Stanley Khamsini (5).
Kwela:
Daniel Ngogo aliwabwaga wenzake kwa kura 151 akifuatiwa na James
Mwamlyela (117), Ameri Nkulu (27), Alstidi Maufi (13) na Michael Moka
(4).
Mlalo: Kelvin Shemboko alipata kura 56 akifuatiwa na Lewis Kopwe (31), Jumanne Pazia (15) na Mkazeni Mkazeni (0).
Mabadiliko ya ratiba
Wakati
kukiwa na sintofahamu na wanachama wanaojiunga na Chadema huku kipindi
cha kurejesha kikiwa kimekwisha, chama hicho kimetangaza mabadiliko
kwenye ratiba ya kurudisha fomu hasa katika majimbo mapya yaliyotangazwa
na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Julai 12.
Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema jana: “Fomu za
kugombea kwenye majimbo hayo zitaendelea kutolewa na hata kura ya maoni
watapiga tofauti na majimbo yaliyokuwapo.”
Alisema hata
katika majimbo mengine, Sikukuu ya Eid el Fitr iliingilia ratiba
iliyopangwa awali na kwamba uongozi wa chama umeona kuwa ipo haja ya
kuongeza siku ili kutenda haki kwa wale waliokosa kulipia fomu benki
kutokana na sherehe hizo.
“Kinachotakiwa sasa ni katibu
wa wilaya kutuma mapendekezo ya kuongeza siku atakazoona zitafaa kwa
zoezi hilo na makao makuu itaidhinisha hilo,” aliongeza.
Msimamizi ‘aingia mitini’
Uchaguzi
wa mgombea ubunge Mbeya Vijijini ulikwama baada ya msimamizi wa kura za
maoni wa Chadema, Christopher Mwamsiku kutokomea kusikojulikana katika
hatua za mwisho.
Kitendo hicho kiliwafanya wajumbe wa
Kamati ya Siasa Mbeya Vijijini na mawakala kubaki njiapanda wasijue cha
kufanya huku wengine wakidai kuwa hizo ni njama za kutaka kumbeba mmoja
wa wagombea.
Mwenyekiti wa Chadema wilayani hapo,
Jackson Mwasenga alishindwa kutoa maelezo ya tukio hilo huku akimtaka
katibu wake kuzungumza.
Katibu huyo, James Mpalaza alisema: “Hata sisi hapa kama unavyotuona tumeduwaa hatujui ni kwa nini ameondoka.”
Alipotafutwa
kwa simu, Mwamsiku alijibu kwa kifupi: “Sijakimbia, nimeondoka kwa
utaratibu mzuri tu… lakini siwezi kukwambia ni kwa nini kamuulize
Mwasenga anayo majibu yote niache nipumzike.”
Dalili za
kuvurugika kwa uchaguzi huo zilianza wakati wa kuhesabu kura baada ya
Mwenyekiti wa Bavicha, Mbeya Vijijini kuingia ndani ya chumba hicho
akidaiwa hahusiki jambo lililozua mzozo mkubwa uliodumu kwa takriban
dakika tano hadi alipotoka.
Wengine wajitokeza Chadema
Tabora Mjini: Peter Mkufya, Nhombar Imajamasallah, Elifuraha Kisangi, Said Mwakasekela na Raymond Maganga.
Kaliua: Anthony Mwakammoja, Godluck Jilinga, Prosper Guga, Peter Msazya na Wilson Lukobe.
Ulyankulu: Dk Deus Kitapondya.
Igalula: Mustapha Kado na James Kabepele.
Tabora Kaskazini: Daud Nteminyanda.
Igunga: Joseph Kashindye, Ngasa Mbojenamba na Gw’igulu Darushi.
Manonga: Ally Halfan Nguzo, Athanas Shija Michael na Simon Seleli.
Nzega Vijijini: Albino Mayani Simbila na Nicholaus Zakaria.
Nzega Mjini: Gisberth Kabamba, Daniel Simba, Boniface Masasi, Charles Mabula, Monica Nsaro, Ally Ndee na Mary Atonga.
Bukene: Alex Mpugi, Lumola Kahumbi, Elias Machibya, Dickson Kagembe na Emmanuel Ntobi.
Rorya):
Mtatiro Sanya, Evangel Dea, Kevin Makooko, Matiko Seruka, Emmanuel
Werema, Ezekiel Kachare, Steven Owawa, Opiyo Nalo, Herman Odemba,
Thomas Risa na Ochora Ndira.
Tarime Vijijini: John Heche, Peter Busene, Moses Yomami, Prosper Nyamuhanga, Johanes Manko na Fabiani Mwita.
Tarime Mjini: Ester Matiko, Lucas Ngoto, Christopher Chomete, Charles Werema na Martinus Joseph.
Waliojitokeza CCM
Arumeru Mashariki: Elirehema Kaaya, Jackson Ezekiel, John Sakaya. Angela Palangyo, William Sarakikya, Dk Daniel Pallangyo na Siyoi Sumari.
Longido:
Philip Kitesho, Dk Stivin Kiluswa, Lee Mamaseta, Daniel Marari, Lesioni
Mollel, Joseph Kulunju, Lemayani Logoliye na Emmanuel Sirikwa.
Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba, David Jairo, Juma Kilimba na Amon Gyuda.
Singida Mjini: Hassan Mazala, Amani Rai, Mussa Sima, Leah Samike, Philemon Kiemi na Juma Kidabu.
Singida Kaskazini: Lazaro Nyalandu, Amosi Makiya, Justin Monko, Michael Mpombo, Sabasaba Manase, Yahana Sinton, Mugwe na Aron Mgogho.
Imeandikwa
na Robert Kakwesi, Dinna Maningo, Mussa Juma, Filbert Rweyemamu, Gaspar
Andrew na Mussa Juma, Joseph Lyimo, Mussa Mwangoka, Godfrey Kahango na
Julius Mathias. Habari kutoka:http://www.mwananchi.co.tz
Wafuasi wa Chadema wakiwa katika moja ya mikutano ya hadhara ya chama hicho. Picha na Maktaba
In Summary
Wakati wabunge hao
wakikubali kumpokea, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa
amesema wananchi wasubiri mambo yatakapokuwa tayari badala ya kutegemea
mitandao ya kijamii.
By Florence Majani, Mwananchi
Dar es Salaam. Baadhi ya
wabunge wa Chadema wamezungumzia taarifa zinazosambaa zikieleza kuwapo
mkakati wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia katika chama
hicho, wengi wao wakimkaribisha.
Wakati wabunge hao
wakikubali kumpokea, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa
amesema wananchi wasubiri mambo yatakapokuwa tayari badala ya kutegemea
mitandao ya kijamii.
“Nitazungumza pale mambo
yatakapokuwa sawa, siwezi kuzungumza sasa, subirini… sasa hivi mambo
mengi yanazungumzwa kwenye mitandao,” alisema Dk Slaa ambaye pia
anatajwa kuwa mgombea wa chama hicho ndani ya Ukawa.
Msemaji
wa Lowassa, Aboubakary Liongo alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa mpango huo
alisema hawezi kulizungumzia hilo kwa kuwa ni suala la mtu binafsi. Hata
hivyo, jitihada za kumpata Lowassa jana hazikufanikiwa kwani simu yake
iliita pasi na kupokewa.
Hivi karibuni, idadi kubwa ya
madiwani wa CCM walirudisha kadi zao na kujiunga na Chadema wakisema
sababu ni kutoridhishwa na kukatwa kwa jina Lowassa kati ya wagombea
urais wa CCM.
Kadhalika, mtandao wa kijamii uliokuwa
ukimuunga mkono mbunge huyo wa Monduli unajulikana kwa jina la 4U
Movement ulitangaza kuhamia Chadema hali inayoashiria kuwa kuna dalili
ya Lowassa pia kujiunga nao.
Wakiandika katika akaunti
ya Twitter ya 4U Movement, wafuasi hao walisema: “Ukimya ni hekima na
ukimya ni busara. Ukimya wa Edward Lowassa ni kutafakari Safari ya
Matumaini... Tuungane kuyapata mabadiliko nje CCM.”
Chadema ni kanisa la wokovu
Akizungumzia
taarifa hizo, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa
alikifananisha chama hicho na kanisa ambalo kwa kawaida halikatai mtu,
bali linawapokea wenye dhambi na kuwaongoza kufanya toba.
“Chadema
ni kama kanisa, hakataliwi mtu, tunahubiri habari njema ya wokovu,
ukija hapa unatubu unaendelea kufanya kazi,” alisema.
Kuhusu
viongozi wa CCM kuhamia Chadema, Msigwa alisema inawezekana kasi hiyo
inachagizwa na Lowassa kukosa nafasi aliyoitaka ndani ya chama hicho.
“Unapokuwa
mwanasiasa unakuwa na wafuasi, inawezekana wengine wanaohamia Chadema
ni watu wake ambao wameona mtu wao amekosa nafasi aliyoitaka ndiyo maana
wanakihama chama,” alisema.
Msigwa alisema Chadema
ilikuwa inakusanya wanachama wapya kwa muda mrefu hata kabla ya vuguvugu
la Lowassa na chama chake kuibuka na ushindi na wanaohamia wanafanya
hivyo kwa sababu wanakipenda chama na wameichoka CCM.
Huenda akatimiza safari ya matumaini
Akizungumzia
ujio wa Lowassa kwenye chama hicho, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema alisema iwapo Lowassa atahamia Chadema anakaribishwa na huenda
akaitimiza safari yake ya matumaini.
“Namkaribisha Lowassa Chadema, huenda safari yake ya matumaini ikaishia huku, akawa mwanachama au hata kiongozi,” alisema.
Alisema
hakuna shaka kuwa mbunge huyo wa Monduli ana nguvu ndani ya CCM ndiyo
maana viongozi wengi wa chama hicho wanakihama wakati huu.
“Hiyo
ilijionyesha kuanzia kwenye Kamati Kuu ya CCM, Halmashauri Kuu, Lowasa
amekamata wajumbe kwa asilimia 80 na hiyo ni ishara kuwa ameishika CCM,”
alisema.
Lema aliongeza kuwa wanaoihama CCM hawaihami kwa bahati mbaya, bali wameona mtu wao waliyemtarajia ameondoka.
“Ni
wengi wanaohamia Chadema, kwa sasa kadi zimetuishia na hiyo ni ishara
kuwa CCM inakufa, ripoti za mikoa yote tunazo,” alisema.
Mbunge
wa Viti Maalumu, Lucy Owenya alisema wanaoihama CCM kwa sasa
wamegundua kuwa chama pekee kinachoweza kutetea wananchi ni Chadema.
“Sisi
tunawakaribisha kwa mikono miwili, waje tuchape kazi, ilimradi
wanafuata kanuni na taratibu za chama, basi. Wamejionea wenyewe kuwa
CCM hakuna chochote,” alisema.
Alisema CCM waliamua
kupitisha katiba bila kuwapo kwa Ukawa, lakini sasa wameona kuwa
walichokifanya ni makosa na wameanza kurudi Chadema ambako wanaamini
kuna demokrasia ya kweli.
Mbunge wa Viti Maalumu,
Cecilia Paresso alisema: “Tunamkaribisha kwa mikono miwili.
Tumekinyooshea CCM vidole kwa muda mrefu kuwa kuna rushwa na makundi na
hilo linajidhihirisha sasa. Lakini wale wote wanaokuja Chadema,
tunawakaribisha ili mradi wafuate kanuni na taratibu zetu.”
Paresso
alisema hana tathmini ya kina kuhusu wafuasi wa Lowassa wanaoihama CCM,
bali wanaokihama chama hicho wameona kina matatizo.
Atakiwa akidhi vigezo na masharti
Licha
ya kuonyesha kumkaribisha, katika chama hicho, baadhi ya wabunge
walimtaka Lowassa afuate kanuni ili awe mwanachama mwenye sifa.
Mbunge
wa Mbozi Magharibi, David Silinde alisema anakaribishwa lakini hana
budi kufuata sheria na kanuni za chama... “Anatakiwa afuate taratibu za
chama, milango ipo huru, lakini afuate kanuni… asije akafikiri ataleta
taratibu zake hapa, sitakubali.”
Silinde alisema
wanaohamia Chadema hawajapendezwa na mwenendo mzima wa uteuzi wa mgombea
wa urais na hivyo wameifuata demokrasia ya kweli ndani ya chama hicho.
Mbunge
wa Kawe, Halima Mdee hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hilo lakini
alisema endapo atajiunga, chama hicho kitampokea kulingana na vigezo na
taratibu.
“Akihamia Chadema nitatoa maoni yangu lakini
ninachoweza kusema ni kuwa kila mtu ana haki ya kwenda chama chochote
ili mradi ana tija,” alisema.
Mdee alisema wanaCCM wanaohamia Chadema wamesoma alama za nyakati na kuona kuwa CCM haiendani na ahadi zake.
Mbunge
wa Viti Maalumu, Susan Lyimo alisema, Lowassa ni binadamu wa kawaida
kwa hiyo kuhamia kwake Chadema si kitu cha ajabu ilimradi afuate
kanuni... “Cha muhimu afuate masharti ya chama, kanuni na taratibu,
kama watu wanahama vyama vingine yeye ni nani asihame CCM?”
Lyimo alisema wanaCCM wengine wanakaribishwa kujiunga kwa sababu kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.
Mbunge
wa Viti Maalumu, Pauline Gekul, aliwataka wana CCM na Lowasa kuhamia
zaidi Chadema ili kuunganisha nguvu na kuichukua nchi.
“Mfikishie salamu Lowassa mwambie karibu kwenye jeshi la ukombozi,” alisema.
Katibu wa CCM amuonya
Akizungumza
na waandishi wa habari jana katika Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma, Katibu
wa CCM mkoa huo, Albert Mgumba alisema ingawa kuhama chama ni hiari ya
mtu, Lowassa hapaswi kuchukua uamuzi wa hasira kiasi hicho badala yake
awe mstari wa mbele kuhamasisha umoja ndani ya chama.
Alimtaka
kutothubutu kuihama CCM na endapo afanya uamuzi huo atambue kuwa hawezi
kukisababishia pengo lolote zaidi ya kujipunguzia hadhi yake ya
kisiasa.
“Mgombea tuliyempata sasa ni makini kuliko, anapendwa, utendaji wake unajulikana kila mahali,” alisema Mgumba.
Mgumba
alisisitiza kuwa badala ya Lowassa kuwa na mawazo ya kuihama CCM,
anapaswa kutuliza fikra na kuonyesha ukomavu wake kisiasa kwa kuwa
mstari wa mbele kuwaonya na kuwatuliza wote waliokuwa wakimuunga mkono
ili wabaki kwa utulivu ndani ya chama na si vinginevyo.
“CCM
siyo Mgumba, ni taasisi iliyosimama. Lowassa anapaswa kutambua hilo,
atulie na awe mstari wa kwanza kuwaonya wanachama wachanga kisiasa,
wasiokuwa na uzalendo ndani ya chama kwa kumfikiria mtu badala ya chama
na masilahi ya Taifa” alisema Mgumba.
Habari na: http://www.mwananchi.co.tz
Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa pili
kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza majimbo
mapya ya uchaguzi katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
leo. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza majimbo 26 mapya ya uchaguzi
ambayo yatakuwa na wagombea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25
mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema
kukata kwa majimbo hayo wamezingatia idadi ya watu pamoja na Jiografia
katika majimbo mapya.
Amesema katika upande wa Zanzibar majimbo yamebaki kuwa 50 kama awali hiyo inatokana vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.
Majimbo
yaliongezwa ni Handeni Mjini, Nanyamba, Makambako, Butiama, Tarime
Mjini, Tunduma, Msimbo, Kavu, Geita Mjini, Mafinga Mjini, Ushetu, Nzega
Mjini, Kahama Mjini, Kondoa Mjini, Newala Mjini, Bunda Mjini, Mbulu
Mjini, Ndanda, Madaba, Mbinga Mjini, Mbagala,
Kibamba,Vwawa,Monongo,Mlimba, Pamoja na Uliambulu.
Jaji Lubuva
amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakiingia katika Halmashauri mbili
hiyo kuweka mipaka katika maeneo ili mbunge aweze kushiriki katika
Halmashauri moja tu.
Amesema baadhi majimbo yamebadilishwa majina na kuendelea kuwepo kwa majimbo hayo kisheria.You might also like:
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa
pamoja na familia ya Bw. Saleh Juma Saleh (mwenye mtoto), yenye watoto
sita wenye ulemavu wa aina tofauti, huko nyumbani kwao Kinyasini
Mkarafuuni Wilaya ya Wete. (Picha na OMKR)
Na: Hassan Hamad, OMKR
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo
ameitembelea na kuifariji familia ya Bw. Saleh Juma Saleh yenye watoto
sita wenye ulemavu.
Akizungumza
na familia hiyo nyumbani kwao Kinyasini Mkarafuuni Wilaya ya Wete
Pemba, katika mfululizo wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa
wa Kaskazini Pemba, Maalim Seif ameitaka kuwa na subra na upendo kwa
watoto hao wakielewa kuwa huo ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Amemuagiza
Mkuu Mkuu wa Wilaya ya Wete kukutana na familia hiyo, ili kuandaa
mipango itakayoweza kuwasaidia katika kuendesha maisha yao na shughuli
zao za kila siku.
Baba
mzazi wa watoto hao Bw. Saleh Juma Saleh amesema watoto wake wanashindwa
kusoma kutokana na kukosa nyenzo kwa vile wote sita hawawezi kutembea.
Amesema
watoto hao wakiwemo wanne wa kike na wawili wa kiume wanasikia vizuri,
wanazungumza na wanafahamu wanachoambiwa, ingawaje baadhi ya wakati
wanapoteza uelewa kutokana na hali ya ulemavu wao.
Amefahamisha
kuwa iwapo watapatiwa nyenzo wataweza kwenda skuli na kusoma kama
wenzao wengine, na kuiomba serikali na wasamaria wema kuwapatia misaada
inayostahiki, ili nao waweze kwenda skuli.
Kwa muda mrefu wahudumu wa afya ya masuala ya ngono wamesisitiza
matumizi ya mipira ya kondomu kama mbinu bora zaidi dhidi ya maambukizi
ya virusi vya ukimwi.
Lakini tabia moja hatari ya kutumia madawa ya kulevya na wapenzi wa jinsia moja inazidi kuibua wasiwasi.
kumekuwa
na njia nyingi za kinga dhidi ya virusi vya ukimwi, lakini kuna dawa
moja mpya - Pre-Exposure Prophylaxis (PrEP) - ambayo inaweza kutoa kinga
dhidi ya maambukizi ya ukimwi iwapo itatumika kabla ya kushiriki ngono.
Utafiti
unaofanywa na daktari Sheena McCormack kutoka chuo kikuu cha London,
unasema kwamba unapomeza dawa hiyo, inazuia maambukizi ya ukimwi kwa
kuzuia ongezeko la virusi, hii ni baada ya majaribio kufanyiwa kundi
moja la wapenzi wa jinsia moja, ambao wamo katika hatari kubwa zaidi ya
maambukizi
Shirika la afya duniani limetambua kwamba dawa hiyo ya tembe inaweza kupunguza maambukizi kwa kiwango kikubwa.
Baadhi ya wakosoaji wanasema kuwa dawa ya aina hii inahamasisha watu wengi kushiriki ngono bila kutumia mipira ya kondomu
Hata
hivyo matumizi ya dawa hii haizuii maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama
vile kisonono na kaswende, je, kukubalika kwa matumizi ya dawa hii
duniani kunamaanisha ongezeko la magonjwa ya zinaa.
Habari na: http://www.bbc.com