Thursday 19 May 2016

ALIKIBA - AJE (Official Video)

Tuesday 12 January 2016

...SHEIN AJIBU MAPIGO, ASEMA ‘JIANDAENI KWA UCHAGUZI’

                      ...SHEIN AJIBU MAPIGO, ASEMA ‘JIANDAENI KWA UCHAGUZI’


Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein      
Kuna kila dalili kwamba mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mkwamo wa kisiasa Zanzibar yamevurugika baada ya wahusika wakuu wa pande mbili, kuzungumza hadharani na kutoa misimamo tofauti.

Wakati Maalim Seif Sharif Hamad wa CUF akiitisha mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kusema chama chake hakipo tayari kuona uchaguzi unarudiwa, Dk Ali Mohamed Shein wa CCM amewataka wafuasi wa chama hicho kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio.
Akihutubia mkutano maalumu wa CCM wa maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar, uliofanyika Viwanja vya Maisara Suleiman, mjini hapa, Dk Shein amewataka wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio pindi Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) itakapotangaza tarehe.
Rais huyo wa Zanzibar alisema jana kwamba huo ndiyo msimamo wa chama chake na hakijatafuna maneno tangu ZEC ilipotangaza uamuzi wa kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015

SHIDA YA MAJI VIJINI TANZANIA.


http://mwanahalisionline.com/wp-content/uploads/2014/12/IMG_04491.jpg
                                              Tabu ya maji kijiji cha Ilota Mbeya Vijijini 
Moja ya visima vinavyotumiwa na wanawake kuteka 
             Tatizo la maji Vijijini je Linachangia kwa kiasi gani kudumaza uchumi wa inchi yetu? 
 


Bidhaa ya maji ni hadimu sana iwe vijijini na hata mjini katika Wilaya ya Newala. Pichani mwanamke akiwa na madumu manne akielekea kusaka maji kwa ajili ya ...
Wananchi wa Namkongo walipata shida ya kutafuta maji hii picha inaonyesha aina ya visima ambavyo wananchi wanavitumia.

                                      

Tukishirikiana tutaweza kupunguza tatizo hili.

Monday 11 January 2016

NJAA YAWAKUMBA WAATHIRIKA WA BOMOABOMOA


                                NJAA YAWAKUMBA WAATHIRIKA WA BOMOABOMOA

              

❖ Wakazi wa bonde la Mkwajuni Manispaa ya Kinondoni jijini hapa, waliobomolewa nyumba zao wanaomba msaada wa chakula kutoka kwa wasamaria wema.

Image result for Bomoa bomoa jangwani
❖ Wakiwa katika vifusi vilivyotokana na nyumba zao kuvunjwa, waathirika hao walisema wanashindia maji na uji huku wengine wakilala na njaa kutokana na kukosa fedha za kununulia chakula.
Askari wa jeshi la Polisi wakisimamaia suala la usalama mtaa wa Bwawani wakati wa bomoa bomoa ikiendelea katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar mapema leo.