Wednesday 24 June 2015

MASHINE ZA BVR ZAGEUKA BIASHARA JIJINI ARUSHA

 MASHINE ZA BVR ZAGEUKA BIASHARA JIJINI ARUSHA  


Kinamama wakifanyabiashara ya mama ntilie katika kituo cha kupiga kura cha kata ya Sombetini ,vituo vya kujiandikisha vinakabiliwa na idadi kubwa
ya watu hali inayopelekea foleni ndefu na watu kukesha kwenye vituo.

Zoezi la Uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura  kwa mfumo
wa kisasa wa BVR umechukua sura mpya kutokana na baadhi ya watu
kuwauzia watu nafasi za kuingia katika vituo vya kujiandikishia hivyo
kugeuka biashara  kwa wanaokwepa foleni ndefu na kukesha katika vituo.


Wananchi wa Kata ya Sinoni jijini hapa  Hussein Issa na Swalehe
Ramadhani wameeleza kuwepo kwa baadhi ya vijana ambao wamekwisha
kujiandikisha lakini hufika kituoni hapo na kushika nafasi za mbele
ambazo wanawauzia watu wengine mchezo ambao umekithiri katika vituo
vingi.

Issa alisema kuwa nafasi moja huuzwa kati ya shilingi 15000 hadi 10000
kwa mtu mmoja  nafasi hizo hugombaniwa na watu wengi  .

“Watu  wamegeuza BVR kama biashara wanashika nafasi na kuwauzia watu
jambo ambalo linakwamisha zoezi wengi wasiokuwa na kitu cha kutoa
wanakaa kwenye foleni kwa muda mrefu bila mafanikio” Alisema Issa

Polpodia Massawe mkazi wa Esso analalamikia mfumo huo kuwa bado
haujaweza kukidhi idadi kubwa ya watu kwani imemlazimu kuacha shughuli
za kujiingizia kipato na kupanga foleni kwa muda wa siku 4 bila
mafanikio.

Aliasema kuwa watu wengine wamekua wakikesha na kulala vituoni hapo
ili kuwahi nafasi hadi kinamama wenye watoto wadogo hivyo ameitaka
serikali iongeze nguvu hasa kwenye vituo vya mijini vyenye idadi kubwa
ya watu.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Filex Ntibenda aliyetembelea kituo hicho
amekaripia vikali tabia ya watu kuuza nafasi maarufu kama ploti kwani
ni kinyume cha utaratibu pia amewataka wanasiasa kutoingilia suala la
uandikishaji na kuishia kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi.

habari picha kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog   Habari na: http://rweyunga.blogspot.com

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR, MAALIM SEIF AHITIMISHA ZIARA YA KUWATEMBELEA WAGONJWA UNGUJA

 MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR, MAALIM SEIF AHITIMISHA ZIARA YA KUWATEMBELEA WAGONJWA UNGUJA 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akihitimisha ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Wilaya ya Magharibi "A" na "B".


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa na Sheikh Habibu Ali Kombo wakiitia dua baada ya kumjuilia hali. (Picha na Salmin Said, OMKR)
Habari toka: http://rweyunga.blogspot.com

Moto waunguza Msikiti wa Omary Bin Hatwah uliopo karibu na jengo la Yanga

      Baada ya Msikiti kuwa umeungua na huyu raia mwema akiwa anaangalia na kujaribu kukagua vizuri vitu vilivyoungua.

Msikiti uliopo jijini Dar es Salaam eneo la kariakoo mtaa wa jangwani na twiga  umeungua moto leo mnamo majira ya saa kumi na moja kasoro.

Chanzo cha moto huo hakikufahamika mara moja ingawa watu wengi waliuwa wanahisi kwamba pengine utakuwa umesababishwa na umeme.

Moto huo umeleta madhala makubwa ikiwa pamoja na kuunguza matanki ya maji, vitabu vya dini, makapeti, mabati, feni, na mtu mmoja alionekana kupata majeraha ya moto mguuni, vioo vya madilisha vilivunjwa ili kuokoa baadhi ya vifaa vya msikitini. 

Watu wa zima moto walichelewa kufika ingawa ofisi zao zipo karibu na eneo la tukio walitumia kama dakika 45.

Watu waliokuwepo eneo la tukio waliokuwa wanasaidia kuzima moto walitoa lawama zao kwa zima moto kwa kuchelewa kufika na kwa raia ambao sio wema waliokuwa wakijaribu kuiba badala ya kuokoa.

Habari hii imeletwa kwenu na Hatasisitupo.blogspot.com