Friday 5 June 2015

UJENZI WA BARABARA YA MAKONDE,MAWENGI WILAYAN LUDEWA WAZINDULIWA RASMI

UJENZI WA BARABARA YA MAKONDE,MAWENGI WILAYANI LUDEWA WAZINDULIWA RASMI

                            Filikunjombe akizindua rasmi ujenzi wa barabara ya Mawengi kwenda Makonde



                                                       mtambo ukiwa kazini


                                    Filikunjombe akikagua barabara mpya ya Mawengi Makonde

Filikunjombe akiwa amechoka kutembea kutoka kata ya Mawengi kuelekea kata ya Makonde,nyuma yake ni katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw.Onoratus Mgaya
                              Hii ndiyi barabra inayotoka kata ya Mawengi kuelekea kata ya Makonde

                   Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.Willium Waziri akiongea na wananchi


 Filikunjombe akiongea na wananchi wa kata za Makonde,Lifuma na Mawengi mara baada ya uzinduzi

Ujenzi wa barabara ya kijiji cha Mawengi kwenda kata za Makonde na Lifuma  mwambao wa ziwa Nyasa wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kwa kiwango cha changalawe umezinduliwa rasmi jana na mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe


Akizindua ujenzi wa barabara hiyo inayofadhiriwa na ubalozi wa Japani Filikunjombe alisema kwa miaka mingi wananchi wa kata za mwambao wa ziwa Nyasa wamekuwa wakitumia usafiri wa majini katika shughuri zao mbalimbali lakini Serikali ya chama cha mapinduzi imekisikia kilio cha watu wa mwambao hivyo imeona ni bora kutoboa barabara inayofuka katika kata hizo ili kurahisisha maisha ya wananchi.


Filikunjombe alisema kuwa wananchi wa mwambao wa ziwa nyasa wamekuwa wakipata mahitaji yao kupitia wilaya jirani ya Kyela kutokana na kutokuwa na barabra ya gari inayoweza kuwafikisha katika makao makuu ya wilaya yao hivyo ujenzi wa barabara hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa kata za Makonde na Lifuma.


Hata hivyo aliwataka wakandarasi wa mradi huo wa barabara kuwa waaminifu na kufanya kazi kwa umakini mkubwa kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi na wakandarasi kutokuwa waaminifu kwa kuiba vipuli na mafuta ya mitambo hali ambayo inarudisha maendeleo nyuma. 


Filikunjombe alisema imekuwa ni tabia mbaya inayoendelea kuzoeleka nchini ya wizi wa mafuta wakati Serikali imepanga bajeti ya kutosha katika matengenezo ya barabara mbalimbali lakini baadhi ya watu hutumia miradi hiyo kujinufaisha kwa kuiba vipuli na mafuta hivyo atakayebainika katika ujenzi wa barabara zote wilayani Ludewa Sheria itachukua mkoando wake.


“Leo tunazindua ujenzi wa barabara ya Mawengi kwenda Makonde ni barabara ambayo inaumuhimu mkubwa kwa wananchi wa mwambao lakini wako watu wanafikiria kuiba mafuta ya mitambo na vipuli,nawaomba tabia hiyo ikome mara moja kwani serikali imeona ilifanye hili ili kuwaletea maendeleo wananchi wa maeneo haya hivyo nalioamna jeshi la polisi yeyote atakayebainika akamatwe na afikishwe mbele ya sheria lakini nawaomba wananchi kuwa walinzi wa miradi yenu ili ikamilike haraka”,alisema Filikunjombe.


Barabara hiyo ambayo itaziunganisha kata tatu na vijiji vingi vya mwambao wa Ziwa Nyasa inakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo kutokana na wananchi wengi kuwa na shauku ya kufanya biashara ya samaki kwa kiasi kikubwa tofauti na awali walikuwa wakibeba samaki kwa kichwa na kutembea umbali kwa kilomita 34 hadi mawengi kwaajili ya kuziuza na kujipatia kipato.


Aidha Bw.Erasto Magombola mkazi wa kijiji cha mawengi alisifu Serikali kwa kuiangalia barabara hiyo kutokana na wananchi wa maeneo ya mwambao kusafirisha wagonjwa hadi kijiji cha mawengi kwa kuwabeba katika mchela hivyo barabara hiyo ni ukombozi mkubwa kwao.


Bw.Magombola alisema kuwa kutokana na ujenzi wa barabara baadhi ya wafanya biashara wa sanmaki na maharage watapata fulsa ya kufanya biashara hiyo kwa urahisi kwani samaki wa ziwa Nyasa wamekuwa wakiuzwa zaidi wilaya ya Kyela wakati wavuvi wako wilaya ya Ludewa haya yote yalisababishwa na ubovu wa barabara.


Kuhusu wizi wa mafuta Bw.Mgombola alisema kuwa yeye kama mwananchi na muhasibu wa kijiji cha Mawengi atashirikiana na uongozi wa kijiji na kata kuwazibiti wezi hapo na hawatawafumbia macho mafanyakazi wa mradi huo ambao watakwenda kinyume na maadili ya kazi zao.


Mwisho. Tukio hili lilifanyika Tarehe 14 mwezi wa tano 2015. 
                                               Habari na Habari Ludewa Blog
 Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe akipokelewa na wananchi wa kata ya Ibumi kwa shangwe kubwa baada ya kufanya makubwa ya kimaendeleo wilayani Ludewa
                                               hawa ni baadhi ya wananchi waliokuja kumshangilia
                        Barabaea za Mitaa ya Ludewa mjini zikiwa zimejengwa kwa kiwango cha Lami


     Filikunjombe hupokelewa na mabango ya namna hii anapotembelea jimbo la Ludewa na vijiji vyake



                 hizi ni picha za ujenzi wa barabra za lami katika mji wa Ludewa unaoendelea hivi sasa
Wananchi wa wilaya ya Ludewa wamekiri misemo ya vijana wa wilaya hiyo ya Ludewa tuitakayo kutokana na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kufanikisha kuubadirisha mji wa Ludewa kwa kipindi cha mika mitano ya uongozi wake kama mbunge

wilaya ya Ludewa ni moja ya wilaya zilizosahaulika kwa kipindi cha miaka mingi lakini kupitia Filikunjombe wilaya hiyo imekuwa na maendeleo ya haraka tofauti na miaka mingine  kwani mtu yeyote aliyewahi kuishi katika wilaya hiyo miaka mitano iliyopita akifika sasa ataona mabadiriko makubwa yaliyojitokeza kwa muda mchache.

Hata hivyo Filikunjombe amekuwa akipokewa na mabango yenye jumbe balimbali zinazoonesha kumuunga mkono katika juhudi zake za kimaendeleo zikiambatana na kumchangia fedha kwaajili ya kuchukulia fomu ya kugombea ubunge kwa awamu nyingine tena.
                                                        Habari na Habari Ludewa Blog:

LOWASSA: SINA MPANGO WA KUSHINDWA,AFUNGUKA MAZITO..HEBU MSIKIE HAPA

LOWASSA: SINA MPANGO WA KUSHINDWA,AFUNGUKA MAZITO..HEBU MSIKIE HAPA

Lowassa, amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku akisema hana mpango wa kushindwa.

Lowassa aliwasili katika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana saa 10:20 jioni akiambatana na mkewe, Regina huku akisindikizwa na wabunge mbalimbali pamoja na wanachama wa CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wanachama waliokuwapo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mara baada ya kuchukua fomu, Lowassa alisema hawezi kuzungumzia upande wa kushindwa katika safari yake.

“Swali rahisi sana, sina mpango wa kushindwa,” alisema Lowassa alipokuwa akijibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari kama atashindwa katika kinyang’anyoro hicho.

Alipoulizwa kuhusu hali ya nchi kuwa na watu wanaoshambuliwa, Lowassa alisema atajenga Serikali itakayojali utu na uhuru wa vyombo vya habari.

“Kwanza nimpe pole yule mwandishi aliyeteswa. Sikubaliani na mambo ya kuingilia uhuru wa watu kuteswa. Serikali yangu itaheshimu uhuru wa vyombo vya habari,” alisema Lowassa huku akishangiliwa na wanachama wa CCM waliokuwa wamefurika ndani na nje ya ukumbi huo.

Alipoulizwa kwanini anahusishwa na vitendo vya ufisadi, Lowassa aliyekuwa akijibu maswali kwa ufupi, alisema kama kuna mtu ana ushahidi na tuhuma hizo amtaje jina.

“Kama hawakunitaja hawakunihusisha… Mtu anayejiamini aseme, na anitaje. Nachoka na siasa za tuhuma, hatupimi viongozi kwa rekodi za matusi ila tutawapima kwa matendo yao,” alisema.

Kada huyo wa CCM alivitaka vyombo vya habari kutoshabikia tuhuma zisizo na ushahidi, huku akisisitiza kuwa kila mtu apimwe kwa rekodi yake.

Kuhusu uteuzi wa mawaziri, Lowassa hakutaka kulizungumzia akisema bado hajavuka daraja.
“Nitavuka daraja nitakapolifikia,” alisema.

Kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alisema ni sera ya CCM iliyotekelezwa baada ya kutokea mgogoro kati ya vyama vya CCM na CUF.

“Angalieni kule Marekani, vyama vya Democrat na Republican, vinashindana kwa kura chache sana. Hata sisi tunapishana kwa kura chache, mimi nadhani kama hatupishani sana hivyo hilo ndilo suluhisho,” alisema.

Awali Lowassa aliwashukuru wana CCM waliofurika katika ukumbi huo akisema anajua kero za chama hicho na atakapokuwa rais atazishughulikia.

“Nawashukuru kwa kunileta nyumbani, nimeitumikia CCM kwa muda mrefu. Nilieleza Dodoma na Arusha nia yangu. Naelewa matatizo wanayopata watumishi wa CCM, nayaelewa. Mishahara midogo, hawakopesheki, hawana fedha za likizo na hawana uchumi mzuri. Wakati wengine wanajengewa nyumba na mikopo wenyewe hawapati,” alisema Lowassa.

Hata hivyo, alimsifu Rais Jakaya Kikwete kwa kuimarisha uchumi ndani ya chama hicho, lakini akasema akiwa rais atafanya zaidi.

“Tunaweza kufanya zaidi, tusiwe ombaomba. Nilipokuwa mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini tumejenga jengo la ghorofa 22 Dar es Salaam. Tuna viwanja na maeneo mengi. Nikichaguliwa kuwa rais na mwenyekiti nitaangalia hilo…Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba,” alisema.

Baada ya mkutano huo, Lowassa alikwenda kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma kupata udhamini wa chama hicho ambapo Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi alikuwa miongoni mwa wanachama waliomdhamini, akiwamo mlemavu wa miguu, Idd Omari.

Baadhi ya vigogo waliokuwa ukumbini ni pamoja na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba na Mbunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah.

Akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Dodoma Mjini baada ya kuchukua fomu, Lowassa alisema vigelele na makofi anavyopigiwa sasa haviwezi kumpeleka Ikulu isipokuwa wananchi wanapaswa kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura ili iwe njia rahisi ya yeye kuwa mkuu wa nchi.

“Naomba watu wajiandikishe, hakikisheni watoto wenu, wajomba na hata washikaji zetu wanajiandikisha katika Daftari la Wapigakura na nitarudi tena kwenu kuomba kura,” alisema.

Huku akishangiliwa na mamia ya wakazi wa Dodoma, Lowassa aliwaambia amekwenda kuomba wadhamini na si kuomba kura, kwani amebanwa na sheria na utaratibu wa chama chao.

Alisema ameguswa na mapokezi waliyompa na kuwashukuru wadhamini wake kwa kumwamini na kusisitiza kuwa atarudi tena kuomba kura.

“Leo siombi kura, naweka akiba ya maneno hata wakihesabu nina kampeni potelea mbali, lakini nilipokuwa waziri mkuu nilianza kuijenga Ikulu mnayoiona mpaka leo haijakamilika, nitakuja kuikamilisha, maana yake nini, nahamia Ikulu Dodoma,” alisema mbunge huyo wa Monduli huku akishangiliwa na mamia ya wananchi hao.
Habari na Masamablog.