Monday 25 May 2015

Wimbi la Joto lawaua watu 430 India

Takriban watu 430 wamekufa kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India. 


Takriban watu 430 wamekufa kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.
Watafiti wamesajili kiwango cha juu mno cha nyuzijoto 48'C katika maeneo mengi nchini humo.
Vifo vingi zaidi vimeripotiwa katika majimbo ya kusini ya Telangana na Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha yao kuanzia jumamosi wimbi hilo la joto lilipotokea.
Mji wa Allahabad ulioko Uttar Pradesh ulisajili vipimo vya nyuzijoto 48C huku wakaazi wa mji mkuu wa India New Delhi ukistahimili kiwango cha nyuzijoto 44C .


Watafiti wamesajili kiwango cha juu mno cha nyuzijoto 48'C katika maeneo mengi nchini humo.
Maafisa wa utawala nchini humo wameanza kampeini ya kuwahamasisha wanainchi kukaa majumbani mwao na kuwashauri wanye waji mengi.
Yamkini viwango vya joto vimekuwa juu zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita lakini vifo vimeanza kuripotiwa mwishoni mwa juma.
Jimbo la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu wengi zaidi ikiwa na jumla ya watu 246 waliopoteza maisha yao kuanzia juma lililopita.


Jimbo la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu wengi zaidi ikiwa na jumla ya watu 246
"asilimia kubwa ya wale waliopoteza maisha ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 walioshinda nje ya majumba yao.'' alisema kamishna wa kupambana na majanga katika jimbo la Andhra Pradesh.
Wakfu wa waandishi wa habari wanasema kuwa watu 186 wameaga katika wilaya 10 za jimbo la Telangana.
Watu 58 wamekufa kuanzia siku ya jumamosi.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa hali hiyo ya joto kuendelea kwa siku kadha zijazo.


Wenyeji wameshauriwa kukaa ndani na kunywa maji mengi
Watu wengine kumi walpoteza maisha yao katika jimbo la Magharibi mwa Bengal.
Waendesha teksi ambazo hazina kiyoyozi hawataruhusiwa kuhudumu kwa saa tano katika mji mkuu wa Kolkata. Hii inafuatia vifo vya madereva wawili.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa inasema kuwa hali hiyo ya juu ya joto inatokana na ukosefu wa mvua.

Familia ya mtoto aliyegongwa na fuso na kukatwa miguu anaomba msaada wa kisheria


Naibu Kamanda wa UVCCM ,Innocent Melleck akiwa na mama mzazi wa mtoto Felista ,Beatrice Shirima mara baada ya kukabidhi kiti cha walemavu cha magurudumu kwa ajili ya kusaidia kutoka eneo moja hadi jingine.
Naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Melleck akikabidhi Pempers kwa mama wa mtoto Felista ,Beatrice Shirima kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo aliyepata ulemavu wa miguu miwli baada ya kugongwa na gari aina ya Fuso.(Na Dixon Busagaga).
Naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini ,Innocent Melleck akiwa amembeba mtoto Felista Shirima(3) aliyekatwa miguu yote miwili baada ya kugongwa na gari aina ya Fuso jirani na nyubani kwao.

Akizungumzia sakata la mtoto huyo Naibu kamanda huyo alisema kuwa ataumia kila aina ya uwezo na nguvu zake kwa kushirikiana na ofisi ya umoja wa vijana wa chama chama mapinduzi UVCCM ili kuhakikisha kuwa  haki ya mtoto huyo inapatikana.
Awali akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msaada wa baiskeli  ya magurudumu matatu na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki saba na kamanda huyo, mama mzazi wa mtoto huyo Beatrice Kelvin,aliiomba serikali na wadau mbalimbali kujitokeza na kumsaida mwanae ili kuhakikisha haki inapatikana. 

Alisema kesi iliyokuwepo mahakama kwa ajili ya kudai haki za msingi za mwanae imeisha bila haki yake kupatikana licha ya kuhangaika sehemu mbalimba na kuomba vyombo husika vinavyo jishughulisaha na haki za binadamu kuingilia kati suala hilo hatua ambayo itasaida kupata haki.
                                                         Chanzo cha habari ni: Jiachie


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yatoa Ratiba Rasmi ya Uchaguzi Mkuu.

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ratiba rasmi kwa vyama vya Siasa na wananchi wote itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali  unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo  Jaji wa Rufaa (Mst.) Damian  Lubuva imesema kuwa kwa Mamlaka waliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,  Sura ya 343, shughuli za uchaguzi zinatarajia kuanza hivi karibuni.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa  Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani unatarajia kufanyika Agosti 21, 2015, na  kampeni za Uchaguzi kwa wagombea hao zitatarajia kuanza Agosti 22 mpaka - Oktoba 24 mwaka huu.
Halikadhalika siku ya kupiga kura kwa wananchi wote inatarajiwa kuwa Oktoba 25, 2015 kwa wale waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.
Chanzo ni Michuzi Jr

             MHE.MWIGULU NCHEMBA   AJIUZULU..SABABU KUBWA NI HII HAPA


Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba
----
Aliyekua Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara,Mwigulu Nchemba amejiuzulu wadhifa huo.

Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha,ametangaza kujiuzulu nafasu hiyo  jana Jioni katika kikao cha Halmashauri Kuu ya ya Taifa ya CCM,Mjini Dodoma

Akithibiths tukio hilo,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye amesema,Mwigulu ameamua kujiuzulu nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara kutokana na nia yake ya kutaka kuomba kuwania Urais kwa tiketi ya CCM  katika Uchaguzi utakaofanyika Octoba Mwaka huu

"Mwigulu alishamwambia nia hiyo Mwenyekiti wa Chama  Rais Jakaya Kikwete,nae Rais akamkubalia, na sasa  katika kikao ameomba rasmi kujiuzulu na Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete amemkubalia Mbele ya wajumbe wa NEC".amesema Nape

Nape amesema kufuatia uamuzi wa mwigulu  kujiuzulu, Mwenyekiti wa Chama Rais Jakaya Kikwete amemteua Msaidizi wake wa maswala ya siasa,Rajabu Ruhavi kuwa Mjumbe wa NEC na Wakati huohuo kamteua kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara Kushika nafasi iliyoachwa na Mwigulu Nchemba 
Chanzo ni Masama Blog