Thursday, 9 October 2014

JANGA:WANAFUNZI WACHOMA MOTO SHULE , SERIKALI YAIFUNGA KWA MUDA WA MWEZI MMOJA

JANGA:WANAFUNZI WACHOMA MOTO SHULE , SERIKALI YAIFUNGA KWA MUDA WA MWEZI MMOJAKamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Njombe, Fulgence Ngonyani akiangalia bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari Njombe ambalo limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia Jana.
 
Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Njombe wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Njombe (Njosi) wakati wakisubiri kupelekwa kituo cha polisi.

Askari akimwangalia mmoja wa wanafunzi ambaye anapelekwa kupakizwa kwenye gari kwa ajili ya kwenda kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.

Na Michael Ngilangwa NJOMBE

Kamishna wa Elimu Nchini Ameifunga Shule ya Sekondari ya Njombe (NJOSS) Kwa Muda wa Mwezi Mmoja Kutokana na Vurugu Zilizotokea Katika Shule Hiyo na Kusababisha Hasara ya Zaidi ya Shilingi Milioni Moja.

Akifunga Shule Hiyo Kwa niaba ya Kamishna wa Elimu Nchini, Afisa Elimu Shule za Sekondari Mkoani Njombe Said Nyasiro Amesema Wameifunga Shule Hiyo Kutokana Uharibifu Uliofanywa na Wanafunzi Ikiwemo Kuchoma Jengo la Bweni na Karakana Pamoja Kupisha Uchunguzi Juu ya Tukio Hilo.

Aidha Afisa Elimu Huyo Ameongeza Kuwa Kila Mwanafunzi Atatakiwa Kurejea Shuleni Hapo Akiwa na Mzazi Ama Mlezi Wake Pamoja na Shilingi Laki Moja na Elfu Hamsini Kwa Ajili ya Kufidia Mali Zilizoharibiwa .

Akizungumzia Chanzo cha Tukio Hilo Mkuu wa Shule ya NJOSS  Benard William Amesema Huenda Likahusishwa na Maamuzi ya Bodi ya Shule Hiyo Iliyokutana  Oktoba 7 Mwaka Huu na Kuwasimamisha Masomo Wanafunzi Waliotoroka Nyakati za Usiku na Kwenda Kwenye Disko Katika Chuo cha Maendeleo Mjini  NJombe, Huku Akisema Kuwa Uchunguzi Bado Unaendelea Kuhusiana na Tukio Hilo.

Hata Hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Linawashikilia Kwa Mahojiano ya Kina Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Njombe NJOSS  Wanaosadikiwa Kuhusika Katika Tukio Hilo.

Mwanzoni Mwa Mwaka Huu Kulitokea Ajali ya Moto Katika Shule ya Sekondari Njombe na Kusababisha Uharibifu wa Baadhi ya Majengo Wakati Wanafunzi Wakiwa Katika Masomo ya Usiku PrepO.

ANGALIA CUF YAAMUA KUKIRI KUWA NI VIGUMU SANA KUIONDOA CCM MADARAKANI BILA YA KUWA NA UMOJA

ANGALIA CUF YAAMUA KUKIRI KUWA NI VIGUMU SANA KUIONDOA CCM MADARAKANI BILA YA KUWA NA UMOJAhttp://3.bp.blogspot.com/-DeHBW9E_wl0/UZ45-oeJmKI/AAAAAAAAAB8/kjq6GyXXrXI/s1600/SOMA+ZAIDI.gif 


Chama cha Wananchi (CUF) kimekiri kwamba ni vigumu kuondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) maradakani bila kuwa na umoja na mshikamano baina ya wanachama na viongozi.


Aidha chama hicho kimesema CCM ni chama kilichokaa madarakani kwa muda mrefu hivyo kama kweli wanataka kukiondoa, ni lazima kuwe na mipango madhubuti ya kisiasa ikiwa ni pamoja na wanachama kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mbalimbali.


Akihutubia juzi wanachama pamoja na wananchi wilayani Masasi waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wa ndani, mjini hapa, Mwenyekiti Taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema wakati umefika kwa wanachama kuacha maneno badala yake wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wawe na sifa za kupiga kura.


Alisema bila umoja na mshikamano ni sawa na kuota ndoto za alinacha kuiondoa CCM madarakani.


Alisema ni vyema wanachama wakajenga mtandao imara mikoa yote nchini ili katika uchaguzi mbalimbali, waishinde CCM.


Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, vijana ni nguvu kazi ya taifa ambao wengi wao huwa hawajihusishi moja kwa moja na masuala ya siasa, badala yake wanaishia kulaumu Serikali kuwa haiwaletei maendeleo.


Alisema kama wote wangeipigia Cuf kura ilikuwa ni rahisi kuiondoa CCM.


“Ndugu zangu, wanachama wenzangu kazi ya kuiondoa CCM madarakani si lelemama kama mnavyodhani…hivyo kama hamtajitokeza kujiandikisha pamoja na kupiga kura kwenye chaguzi mbalimbali itakuwa kazi bure,” alisema.


Alisema CUF ina nia ya dhati kuiondoa CCM lakini changamoto kubwa iliyo mbele yao ni ushiriki mdogo wa vijana ambalo ni kundi kubwa.


Alisema Desemba mwaka huu ni Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo aliwataka wanachama kujitokeza kwa wingi kupiga kura huku akisema hiyo ndiyo silaha pekee ya kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani.


Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba aliongoza harambee ya kuchangia ununuzi wa uwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya chama hicho Wilaya ya Masasi ambapo jumla ya Sh 430,000 taslimu zilipatikana huku ahadi ikiwa ni Sh 270,000.

HABARILEO

These mountains are dangerous!
http://4.bp.blogspot.com/-fNPET8BnPzg/VDVNACkq7oI/AAAAAAAAWkA/UlRCQuzH6AY/s1600/IMG_0815.JPG
.