Monday 24 August 2015

UN KUBORESHA VYOO VYA SHULE 10 KILIMANJARO

IMG_4176
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na walimu mara baada ya kuwasili katika shule ya msingi Kiboriloni kwa ajili ya kushiriki zoezi la kuweka msingi kwenye ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo. Kulia kwake ni Afisa Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya. (Picha zote na Zainul Mzige)
IMG_4174
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem aliyeambatana na Alvaro Rodriguez akisalimiana na walimu wa shule ya msingi Kiboriloni.
IMG_4181
Maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwasili kwenye eneo la tukio ikiwa ni shamra shamra za kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_4625
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kuweka msingi wa ujenzi wa vyoo 18 ikiwa ni sehemu ya kuboresha mazingira bora ya kusomea sambamba na maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_4602
Sehemu ya wanafunzi wa shule msingi Kiboriloni wakifurahi habari za kujengewa vyoo.
IMG_4159
Wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni wakinawa mikono yao kwa sababu mara baada ya kutoka msalani kama walivyokutwa na camera ya modewjiblog
IMG_4569
Baadhi ya vyumba vya vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Kiboriloni.
IMG_4184
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (kulia) akiwapungia wanafunzi wa shule msingi Kiboriloni (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili shuleni hapo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
IMG_4192
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akiweka maji wakati wa maandalizi ya kutengeneza zege kwa ajili ya kuweka msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakisubiri kuchanganya zege.
IMG_4198
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) wakianza matayarisho ya kuchanganya zege huku Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Martha Ofunguo akimwaga maji kwenye mchangayiko huo.
IMG_4207
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakiendelea na zoezi la kuchanganya zege.
IMG_4210
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakishiriki zoezi la kubeba maji na kokoto kwa ajili ya kuchanganya zege la msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni.
IMG_4215
IMG_4217
 Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akishuhudia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakati akimwaga zege waliloandaa kwenye ujenzi wa msingi wa vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni.
IMG_4225
Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Titus Osundina (kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem wakishiriki zoezi la kumwaga zege katika msingi huo.
IMG_4252
Hapa ni kazi tu.....; Ni maneno ya Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu wakati akishiriki zoezi la kuchanganya zege katika shule msingi Kiboriloni. Kwa matukio zaidi Bofya hapa 
 
Na Mwandishi Wetu, Moshi

MASHIRIKA ya Umoja wa Mataifa nchini, yatasaidia kuboresha vyoo katika shule 10 zilizopo katika manispaa ya Moshi na wilaya ya Moshi vijijini.

Hayo yalisemwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, kwenye hafla ya kuweka msingi kwa ajili ya ujenzi wa matundu 18 ya choo katika shule ya msingi Kiboriloni.

Alisema pamoja na mashirika hayo kusaidia uboreshaji huo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, amewataka watoto kukumbuka kutunza mazingira na miili yao kama sehemu ya mazingira hayo.

Aidha aliwataka wanafunzi kuhakikisha kwamba wanajenga mshikamano mkubwa na wenye upendo kila kundi likithamini kundi jingine kwa ajili ya ustawi wa taifa .

Alisema wasichana kwa wavulana kuheshimiana kwani katika hilo wataweza kutengeneza taifa linaloheshimiana na hivyo kulinda msingi wa maisha wa amani unaowezesha maendeleo na ustawi wa jamii.

Aliwataka wanafunzi hao kushikilia ndoto zao na kusaidia kutambua kwamba wanahitajika kutunza mazingira na kujali afya zao.
 
 
Akimkaribisha Mratibu huyo kuzungumza na wanafunzi mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Kiboriloni Salehe Msuya alisema kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1946 eneo la Msaranga na kuitwa kwa jina hilo na baadae kuhamishiwa Kiboriloni ambako kulikuwa na makazi ya Mangi mwaka 1955 inakabiliwa na ukosefu wa matundu 18 ya choo, maktaba na bwalo la chakula.

Alisema ingawa shule ilianzishwa ikiwa na wanafunzi 12 ilipohamishiwa Kiboriloni 1955 na kupewa jina hilo mwaka 1990, sasa ina wanafunzi 613 kuanzia darasa la awali hadi la 7 na kukabiliwa na changamoto za matundu.

Shule hiyo inahitaji kuwa na matundu 32 lakini yaliyopo sasa ni 14.

Mwalimu huyo aliishukuru UN kwa kuwasaidia kutengeneza matundu yaliyobaki na kuwaomba pia kusaidia kuboresha mazingira ya kusomea katika kuwa na maktaba na bwalo la kulia chakula.

Kwa sasa shule hiyo inatoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wake na hawana mahali pa kulia.

Pamoja na taaluma kuzidi kuimarika shuleni hapo, shule haina maktaba.
Habari na:http://rweyunga.blogspot.com

Saturday 15 August 2015

UJENZI WA MRADI WA UMEME KILONDO WALETA MATUMAINI

     Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiangalia Power House katika kijiji cha Kilondo
                                 huu ndio mtaro wa maji kwaajili ya kufua umeme kata ya Kilondo


                                  Filikunjombe akipata maelezo kuhusiana na ujenzi wa mradi huo





Ujenzi wa mradi wa umeme wa kutumia maji kwa ufadhiri wa REA katika kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoa wa Njombe umeanza kuleta matumaini baada ya hatua ya awali kukamilika ambayo ni ujenzi wa njia ya maji na nyumba ya kufunga mtambo wa kufua umeme kukamilika.

Hivi karibuni mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe aliweza kutembelea mradi huo ambao uko mwambao wa ziwa Nyasa na kujionea maendeleo yake ambapo aliweza kuwashukuru wananchi kwa kushirikiana na wakandarasi wa mradi huo.

Filikunjombe alisema kuwa wakati wa utawala wake yeye kama mbunge Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeweza kuanzisha miradi ya umeme katika vijiji 67 wakati wilaya ya Ludewa inajumla ya vijiji 77 hivyo ni vijiji 10 tu ndivyo vitakuwa havina nishati ya umeme lakini juhudi za kukamilisha miradi hiyo na kuhakikivijiji vyote vya wilaya ya Ludewa vinakuwa na nishati hiyo zinaendelea.

Aidha aliwataka wananchi wa wilaya ya Ludewa katika vijiji hivyo 67 kushirikiana kikamirifu na wawekezaji hasa wataalamu wa miradi hiyo ili kuhakikisha miradi hiyo inakamirika haraka kwa muda uliopangwa na Serikali.

“nawaomba wananchi wa jimbo langu kushirikiana kikamirifu bila kujari itikadi za vyama vyenu kufanya kazi na wawekezaji hasa hawa wataalamu wa miradi hii ya umeme ambao wanafanya kazi ngumu katika maeneo yetu na tuondoe dhana potofu ya kuwa hizi kazi ni za Serikali wakati umeme tutautumia sisi wananchi ambao ndio Serikali yenyewe”,alisema Filikunjombe.

Naye mmoja wa wananchi wa kata hiyo Bw.George Mwakipokile alisema kuwa wananchi wamekuwa wakishirikiana kikamirifu na  mafundi wa kazi hiyo katika kila hatua kwani ni jambo la kimaendeleo kupata nishati hiyo Kilondo awali hakuna hata mtu mmoja ambaye alifikiria siku moja kata ya Kilondo ingeweza kuwa na umeme.

Bw.Mwakipokile alisema kuwa wananchi wanamshukuru mbunge wao ambye ni Filikunjombe kwa kushirikiana na Bw.Mwambeleko kubuni mradi huo wenye tija kwa jamii ya wanaludewa kwani mradi huo ni mkubwa na unauwezo wa kusambaza umeme huo katika kata zote za mwambao wa ziwa Nyasa.

Mwisho.
                                Habari na:http://habariludewa.blogspot.com

Mtoto apata mtoto Paraguay

Kampeni imeanzishwa kupinga ubakaji kwasababu ya kisa cha binti huyo.
Binti wa miaka kumi na mmoja nchini Paraguay aliyedai kubakwa na baba yake wa kambo amejifungua mtoto wa kike baada ya mamlaka nchini humo kumzuia asitoe ujauzito aliokua nao.
Madaktari katika mji mkuu wa Asuncion wamesema binti huyo na mtoto wake aliyejifungua kwa njia ya upasuaji wanaendelea vizuri.
Tukio hilo limesababisha utata mkubwa nchini Paraguay na katika mitandao ya kijamii, Paraguay ni taifa linaloamini zaidi katika Ukatoliki ambapo mwanamke anaruhusiwa kutoa mimba pale tu afya yake inapokuwa hatarini.
Binti huyo alibakwa alipokua na umri wa miaka kumi pekee na Baba yake wa kambo mwenye miaka arobaini na miwili yupo rumande akisubiria kutajwa kwa kesi yake wakati huo huo baba huyo amekanusha kuhusika katika tukio hilo.
                                  Habari na: BBC

Lowassa: Sitaki mchezo


Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowasa akiwapungia mkono wafuasi wa chama hicho baada ya kuwasili katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya jana. Picha na Godfrey Kahango. 


By Lauden Mwambona na Godfrey Kahango, , Mwananchi
Mbeya. Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa jana alipokewa na maelfu ya watu mjini hapa ambao kwenye uwanja wa Ruanda, Nzovwe, aliwaambia wananchi kuwa hatataka mchezo katika serikali atakayoiongoza.
Pamoja na Jeshi la Polisi kutangaza kuzuia msafara wakati wa ziara ya waziri huyo mkuu wa zamani, hali ilikuwa tofauti jana wakati zaidi ya magari 20 yalimsindikiza kutoka Uwanja wa Ndege wa Songwe huku wananchi wakijitokeza barabarani kumshangilia hadi kwenye uwanja huo, ulio nje kidogo ya mji wa Mbeya ambako alihutubia.
Polisi walinda msafara
Msafara wa Lowassa uliwasili mjini hapa kwa kutumia ndege mbili, ya kwanza ikiwa imebeba waandishi wa habari wapatao 10 na nyingine iliyombeba mbunge huyo wa Monduli ambayo iliwasili saa  8:20.
Umati wa watu ulikuwa ukimsubiri nje ya uwanja huo na alipotoka ilianza safari ya kuelekea katikati ya jiji na msafara wa zaidi ya magari 20 pamoja na pikipiki.
Polisi walitanda barabarani, huku vijana wa Red Brigedi waliovalia sare nyeusi na miwani wakiwa wamesambazwa barabara yote.
Maeneo ambayo msafara ulipita kwa shida kutokana na umati wa watu kufurika ni Mbalizi, Mafiati Mwanjelwa, lakini polisi walifanya kazi ya ziada kuwaondoa watu waliokuwa wakitaka kuandamana kuusindika msafara huo.
Lowassa aliambatana na mgombea mwenza, Juma Haji Duni, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na kulakiwa na viongozi wa mkoa pamoja na mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina la Sugu.
Akizungumza baada ya kukaribishwa kuhutubia na Duni Haji,  Lowassa alianza kwa kibwagizo cha “mchakamchaka  chinja” na kabla ya kuwashukuru wananchi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa kufurika hadi pomoni kwenye uwanja huo.
“Sitaki mchezo,” alisema Lowassa ambaye amekuwa akizungumzia uendeshaji wa Serikali kwa mtindo wa mchaka mchaka.
“Nataka maendeleo. Nataka Jiji la Mbeya liwe la kimataifa wakati wa Serikali yangu na litakuwa kama nchi ya Swaziland,’’ alisema akilifananisha jiji hilo na nchi hiyo ndogo iliyozungukwa pande zote na Afrika Kusini.
“Nitahakikisha Uwanja wa Ndege wa Songwe unakuwa wa kimataifa.”
Lowassa, ambaye alipata zaidi ya watu 50,000 mjini hapa wakati alipokuwa akisaka wadhamini wa urais kwa tiketi ya CCM, alisema Serikali yake pia itawajali walimu na wakulima, huku akisisitiza kwamba watakaochelewesha pembejeo watakiona cha moto.
Akizungumza polepole, Lowassa alisema katika Serikali yake hatataka mchezo katika kazi  na kwamba mawaziri wake watachapa kazi saa 24  kuwahudumia wananchi.
Kuhusu kiu ya wananchi waliotaka kujua kauli yake kwa polisi, alisema polisi wanatenda kazi huku wakitaka mabadiliko ya kupata mshahara mnono na kwamba ataboresha mahitaji ya wafanyakazi kwa ujumla.
Awali akiwakaribisha wageni, Sugu aliwashukuru wakazi wa Mbeya kwa kile alichokieleza kuwa ni kuleta mizuka kwenye uwanja huo kutokana na kufurika watu wengi. “Karibu Mbeya wageni, hapa siyo mafuriko ni gharika... kilichobaki ni kupiga kura ya kukuchagua wewe Rais Lowassa,’’ alisema.
Sugu alisema goli la mkono la CCM litazuiwa na beki makini Lowassa  na kutoa onyo kwamba CCM wasidiriki kutumia kadi bandia za wapiga kura.
Naye Mbatia  alisisitiza suala la Watanzania kulinda amani na upendo na kuwasihi wakazi wa Mbeya wasikubali kufanya vurugu katika kipindi chote cha kampeni na uchaguzi.
Wabunge wawili wajiunga Chadema.
Wakati Lowassa akipata wadhamini, Chadema ilipata neema tena wakati wabunge wawili wa CCM,  Dickson Kilufi  wa Mbarali na Luckson Mwanjale wa Mbeya Vijijini walipotangazwa kujiunga na chama hicho kikuu cha upinzani.
Hata hivyo, Mbowe alimkabidhi kadi Kilufi pekee baada ya Mwanjale kutofika eneo hilo licha ya kuonekana uwanja wa ndege.
             Habari kutoka:http://www.mwananchi.co.tz