Monday, 10 August 2015

Nina Uhakika Hujaona Matukio Katika Picha Hizi Lowassa Akifanya Kufuru CUF Makao Makuu

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhkzTWMfIVvtp9uDhwshAm5g-SzJF6bqwtIoT1FLkka-cKWisCqZysdw9ye_OSLhSwus1Cf5T9D19Imah6iw6OJ9lh28BPOq1qKPBatIeuAc1D5NhA1SyPDNBwLlfZicLdWoMi9I5tfZDw/s1600/MMGL0309.jpg

LOWASSA AHUDHULIA MKUTANO WA BARAZA KUU LA CHAMA CHA WANANCHI CUF, JIJINI DAR LEO

 Sehemu ya Wafuasi na Wanachama wa Chama cha Wananchi CUF, wakiwa wamejipanga Barabarani tayari kwa kumlaki, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, alipokuwa akielekea Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Wanachama wa Chama cha Wananchi CUF wakifurahia Ugeni huo.
 Sehemu ya Viongozi wakuu wanaounda UKAWA, wakiongozwa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi, Mh. James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi, wakimsuburia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungua Wanachama na Wafuasi wa Vyama UKAWA waliofurika kwenye Makao Makuu ya CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akikumbatiana na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kabla ya kuelekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia na Dkt. Emmanuel Makaidi wakitembelea kuelekea Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakiwapungia wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakati wakielekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. Wengine walioambatana nao ni Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia na Dkt. Emmanuel Makaidi.

Umati wa Watu ukiwapokea Viongozi wao.
Umati nje ya Makao Makuu ya CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakati wakielekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.

Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasili kwenye Makao Mkuu ya CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi,Mh. James Mbatia  akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi akimpongeza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa mara baada ya kuhutubia.
Wakielekea kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Mh. Magdalena Sakaya wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho, uliofanyika August 9, 2015, kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjncsZ8bfYS53wrf4ppSYcvomEac_OMyz2lOHUgafvc2rGg3R3tKvOARPzI58bs9gIu69XrkR70dBU6VOqlPZ2oZ-A679nECXhW7U5HsA9amJotj-O2-OnZx0jr268oUAA7xUkOzm7av9g/s1600/MMGL0373.jpg



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEilOxn0iiYkJGj9Uic4sBsSthCwf7QMJRva-RYGRgtrfsuZ6kVm-7-TwZv7RQy4ocRR8_iIZnoxEp8nBtaSoRPEwYAhVnWO2MhLd5jWoh1P1_XQRYS3LZ9r9hyphenhyphenHlX3c4WKeAULRlqrCxG0/s1600/MMGL0172.jpg




https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjFrd9GJkT8ykfuj7DWv0DObGZwKpyd9xhJneo4M1uDcMAWTYTwEZUV_gaDxUKvGI-XRyu28loYj__NamnDkBUJxZDhLN6paXVzlOLjnWx9-zLgDIpea9QCy9nc6yAdbnOpPkAx1D7yAyc/s1600/MMGL0473.jpg
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahimu Lipumba amepotea kwenye uwanja wa siasa. Anaandika Pendo Omary wa Mwanahalisi Online
Hali hiyo imejitokeza leo asubuhi wakati mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa alipotembelea Ofisi Kuu ya CUF Bunguruni, Dar es Salaam kwa mara ya kwanza.
Katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu, Lowassa anawakilisha vyama vinne vinavyounda UKAWA ambavyo ni Chadema yenyewe, CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na NLD.
Lowassa alifika kwenye ofisi za CUF saa 12.40 mchana lengo likiwa ni kuzungumza na viongozi wa chama hicho akiwa ni mwakilishi wao kupitia UKAWA.
Katika Safari hiyo walikuwepo pia wenyeviti wenza wa UKAWA -Freeman Mbowe (Chadema), James Mbatia (NCCR- Mageuzi) na Emanuel Makaidi (NLD).
Viongozi wengine ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif; Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya; Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu; Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu na wabunge wanaotoka vyama vinavyounda UKAWA.
Tofauti na ilivyotarajiwa kwamba, kujiuzuru kwa Prof. Lipumba kungesababisha mpasuko ndani ya CUF, badala yake maelfu ya wanachama wa CUF walifurika katika ofisi za chama hicho mapema leo kuanzia saa tatu asubuhi.
Hakukuwa na vikundi vya watu katika majadiliano kuashiria kujadili kuhusu kuondoka kwa Prof. Lipumba, badala yake nyimbo za kumsifu Lowassa na Ukawa zilitawala.
Baada ya Lowassa kukaribishwa na mwenyeji wake Maalim Seif, alisema, “…kwanza nawapa pole kwa Lipumba kuondoka,” kauli hiyo iliyopokelewa na maelfu ya wanachama wa CUF waliofurika katika ofisi hizo kwa kusema “Hatumtakiii…..Lipumba aende zake.”
Lowassa aliendelea “nilikuwa sijamaliza kusema. Nawapongeza kwa uvumivu wenu na umoja wenu katika kipindi hiki baada ya kuondoka Lipumba.
“Nimepata faraja sana kujiunga na Ukawa japo kumekuwa na misukosuko ndani ya UKAWA. Ni lazima tuwe wamoja, mtunze kadi zenu za kupigia kura. Mwaka huu lazima tushinde tena kwa kura asilimia 90 ili wakiiba asilimia 10 tusisikie,” amesema Lowassa.
Hata hivyo Maalim Seif amesema, “tumepata faraja kubwa sana kutembelewa na Lowassa. Hii ni kuthibitisha UKAWA bado tupo pamoja. Hakuna kurudi nyuma, mbele kwa mbele mpaka Lowassa aingie Ikulu. Zanzibar tupo tayari Maalim Seif ndiye rais. Tunasubili aapishwe.”
Kwa upande wake Duni amesema, wagombea wa UKAWA hawapo kwa nia ya kusaka madaraka peke yake kama ambavyo inaelezwa bali kuhakikisha CCM inaondoka madarakani na kila Mtanzania anapata haki sawa katika kunufaika na rasilimali za nchi yake.
“Kama mnavyojua, nilikuwa waziri serikalini. Juzi nimeamua kuachia madaraka baada ya kushauriana na viongozi wangu wa CUF ili nijiunge na Chadema kuhakikisha CCM inaondoka madarakani. Tayari nimeandika barua kwa rais ya kuachia madaraka. Na juzi tu nimetoka kumuaga rasmi,” amesema Duni huku akishangiliwa na ummati.
Hata hivyo, katika mkutano huo Mbowe amewaambiwa wananchi na wafuasi wa UKAWA kuwa, “hii safari ya mabadiliko tumeipigania kwa miaka 25. Wapo waliopoteza maisha, kuachika, kufilisiwa, vilema na wenye kesi katika safari hii. Imekuwa ngumu. Akitoka kiongozi kati yetu akaona malengo yetu hayaendani nae. Huyo hatufai.
“Leo tuna wagombea waliojiunga na Chadema hivi karibuni na wanagombea urais na umakamu. Chadema hatugombei vyeo. Tupo tayari kufanya kazi na wenzetu bila kujali wamejiunga lini na chama.”
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kwenye mkutano huo amewatoa hofu wananchi kuhusu uvumi unaoenezwa kwenye mitandao kwamba “mgombea urais na mgombea mwenza wake ni lazima wawe wanachama kupitia vyama wanavyogombea kwa muda wa miezi mitatu.”
“Katiba zote mbili za Tanzania na Zanzibar ninazo hapa. Hakuna Katiba wala Sheria inayosema mgombea wa urais na makamo wake ni lazima watimize muda wa miezi mitatu tangu kujiunga na chama wanachokiwakilisha katika uchaguzi huu. Huu ni uzushi.”
Lissu amesema, masharti yanayotolewa na katiba hizo ni kwamba, mgombea wa urais na makamu wake ni lazima wateuliwe na chama cha siasa chenye usajili wa kudumu.

LOWASSA ACHUKUA FOMU NEC

Tuesday, 28 July 2015

Lowassa na mkewe wakabidhiwa kadi rasmi za chama cha chadema


Waziri mkuu mstaafu Mh: Lowasa leo amekabidhiwa kadi ya uanachama wa chama cha chadema katika hoteli ya bahari beach, kadi hizo zimetolewa kwa lowasa pamoja na mkewe, na mheshimiwa lowasa amesema yeye hana mpango wa kulipa kisasi kama watu wengine wanavyohisi badala yake amesema kama kunamtu anahisi kwamba anamakosa na anaogopa lowasa atalipa kisasi asiogope na badala yake aende mbele za Mungu na kuomba asamehewe. Viongozi wote wa UKAWA wamelizia kunpokea Lowasa.

Rich Mond:
Kwa suala la RICHMOND amesema kwa mtu yeyote mwenye ushahidi na tuhuma hizo ampeleke mahakamani na aache kupiga kelele.

SALAMU:
Dr Makaidi: Anaanza kwa kutoa Salamu kwa , MBowe, Lipumba, Mbatia na Lowasa ambazo zimetoka chama cha chake Cha NLD, na kutaka LOwasa asahau mambo ya CCM na kufuata ya UKAWA.

Makamu / mwenyekiti CUF, Anaanza kwa kutoa Salamu kwa , MBowe, Makaidi, Mbatia na Lowasa na kusema amepigwa na butwaa na kusema ukawa wamepata jembe.
 NCCR MAGEUZI: Anaanza kwa kutoa Salamu kwa , MBowe, Lipumba, Makaidi na Lowasa na kusema wataendelea kulinda hazi za Mh: Lowasa za kuwa waziri mkuu mstaafu na kusema CCM haina haki miliki ya kuimiliki TANZANIA.
 CHADEMA: MBOWE:  Anaanza kwa kutoa Salamu kwa watu wote na kwa, Lipumba, Mbatia na Lowasa, Kwaniaba ya chadema anamkaribisha LOWASA na Familia na watanzania katika Familia ya CHADEMA, Anasema ujio wa Lowasa umezua hofu CCM, anasema alipigiwa simu na watu wa CCM nakuambiwa akimkaribisha Lowasa atakiharibu chama, na anaanza kuwatoa hofu wanachadema kwa kusema hasemi Lowasa ni mtakatifu bali pia chadema sio mahakama ya kuhukumu mtu bila ya ushaidi.

                                     Habari na www.hatasisitupo.blogspot.com

BASI LAGONGA TRENI YA MIZIGO NA KUUA WANNE - TABORA MJINI




Askari Polisi wakifanya ukaguzi kwa maiti zilizokutwa eneo la ajali hiyo

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Juma Bwire akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio la ajali mbaya iliyotokea eneo la kata ya Malolo manispaa ya Tabora ambapo watu wanne walikuwa wamepanda basi hilo la kampuni ya Dont Worry ambapo lilisababisha ajali hiyo baada ya kugonga treni ya mizigo,watu kadhaa wamejeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete.
Eneo la chini la basi hilo la kampuni ya Dont Worry ambalo lilisababisha ajali hiyo ambapo mbali na uzembe wa dereva lakini basi hilo lililokuwa likifanya safari zake kutoka Tabora mjini kwenda Ufuluma wilaya ya Uyui limeonekana sehemu hiyo ya chini imefungwa kamba za mipira kuzuia vyuma vinavyunganishwa na usukani visichomoke kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa maisha ya wasafiri.

Thursday, 23 July 2015

Mauzauza ya BVR yahamia Dar


Fundi wa mashine za Biometric Voters
Fundi wa mashine za Biometric Voters Registration (BVR) zinazotumika kuandikisha wananchi kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura, Neema Mbwambo akiirekebisha moja ya mashine hizo katika kituo kilichopo Shule ya Sekondari ya Zawadi, Tabata Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory 
By Waandishi Wetu
Dar es Salaam. Kasoro za uandikishaji wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura zilizokuwa zikitokea katika mikoa mbalimbali nchini, zimejitokeza pia jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya kwanza ya kazi hiyo.
Mwananchi ilipita katika maeneo mbalimbali jana na kushuhudia wananchi wengi wakiwa wamekutana na changamoto kadhaa kwenye baadhi ya vituo ikiwamo ya kukosekana mashine za Biometric Voters Registration (BVR).
Wananchi hao walisema licha ya kwamba Dar es Salaam imepewa siku 10 ya uandikishaji, kama changamoto hizo hazitachukuliwa hatua kazi hiyo inaweza isikamilike kwa wakati.
Miongoni mwa changamoto nyingine ni kuharibika kwa mashine zilizopo, ukosefu wa umeme, uchache wa watendaji na kuelemewa na watu, mtandao usio wa uhakika na nani aanze kuandikishwa kati ya wenye mahitaji maalumu na wasionayo.
Katika kituo cha uandikishaji cha Shule ya Msingi Oysterbay ambako kuna vituo vidogo vitano, wakala wa uandikishaji, Margereth Galway alisema mwitikio wa vijana umekuwa mkubwa kiasi kwamba inakuwa shida kuwapa nafasi ya upendeleo wazee, viongozi, walemavu au wajawazito na wanaonyonyesha.
“Eneo hili lina wazee na viongozi wengi wa chama na Serikali. Mwitiko mkubwa wa vijana unatufanya tushindwe kuwasaidia watu hao,” alisema Galway.
Alisema wasimamizi wote wa kituo hicho wamekubaliana kuwa kuanzia leo, wateue mashine moja na itengwe kwa ajili ya wenye mahitaji maalumu ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi wanaokuwa wamesimama kwenye foleni muda mrefu.
“Tayari wameshakuja Warioba (Jaji Joseph), Msekwa (Pius) na Butiku (Joseph) wakiwa na wake zao na kujiandikisha. Pamoja na kufahamika kwao bado vijana hawakuwa radhi kuwapisha wakitaka wajipange jambo ambalo ni gumu kulitekeleza.
“Kama tutafanikiwa kuwashawishi waandikishaji basi foleni za watu wa kawaida zitakuwa nne na moja itaachwa kwa ajili ya wenye mahitaji muhimu,” alisema.
Katika Kituo cha Shule ya Msingi Kawe A, wazee wengi walikutwa wamekaa kwenye madawati, nje ya madarasa wakisubiri kuandikishwa baada ya vijana kutokubali kuwapisha wakidai waandaliwe utaratibu ambao hautoingilia foleni iliyopoo.
Katika Shule ya Msingi Hekima iliyopo wilayani Kinondoni, kulikuwa na malalamiko kama hayo na wananchi wakaiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuweka utaratibu maalumu.
Mmoja wa waliofika kujiandikisha, Mwanaidi Abdallah alisema katika uandikishaji huo wanawake wamekuwa wakipata shida kutokana na utaratibu mbovu.
Alisema inachukua muda mrefu kupata huduma kwa sababu baadhi ya vijana wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kujiandikisha.
Katika kituo cha Mtendaji kilichopo Mtaa wa Mzimuni, Kata ya Kawe, wananchi walikutwa wakiwa nje saa 8:00 mchana wakisubiri mashine ili uandikishaji uanze licha ya kutangaziwa kazi hiyo ingeanza asubuhi.
Kitu pekee kilichokuwa kinaendelea ni wananchi kujiorodhesha kwenye daftari na kupewa namba ya foleni hadi mashine zitakapoletwa.
Mkazi wa Ununio Beach, Joseph Mrisho alisema licha ya wananchi kujitokeza kwa wingi kuna vituo viwili mashine ziligoma kufanya kazi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ununio Beach, Mwijuma Mwinyihija alisema usumbufu waliokumbana nao wananchi umesababisha malalamiko na wengine wamekataa tamaa na kuamua kuondoka kwenda kwenye shughuli zao za kujitafutia kipato.
Katika Kata ya Wazo Mtaa wa Salasala eneo la IPTL, hadi saa 9:00 alasiri wananchi walikuwa hawajaandikishwa kutokana na mashine kugoma.
Mkazi wa eneo hilo, Blandina Hizza alisema alilazimika kurudi nyumbani mara kadhaa akijipa matumaini huenda mashine hiyo itatengemaa ili aandikishwe, lakini hadi muda huo hakufanikiwa.
Frank Etta alisema: “Hatuelewi imekuwaje hadi sasa wahusika hawajaleta mashine.”
Kituo cha Shule ya Msingi Mlimani kilichopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambacho kinastahili kuwa na vituo vidogo vitatu, kina mashine moja tu iliyopelekwa.
Mwandikishaji Msaidizi katika kituo hicho, Isabella Mkumbwa alisema mwitikio wa watu ni mkubwa, lakini uandikishaji unakwenda taratibu kwa sababu watu wote wanatakiwa kusubiri mashine moja.
“Baadhi ya watu wameondoka ili wakaendelee na kazi zao. Tunasubiri mashine nyingine mbili ziongezwe wakati tukiendelea kuitumia hii iliyopo,” alisema msimamizi huyo.
Kituo cha Shule ya Sekondari Zawadi kiliyopo Tabata, uandikishaji ulikuwa haujaanza hadi saa 4:00 asubuhi wakati gazeti hili lilipotembelea kituoni hapo na kukuta mashine ikitengenezwa.
“Niliwahi kufika na nikapewa namba 23 ila tumeelezwa kuwa walimu wataanza kuandikisha pindi mashine zitakapotengamaa. Wamesema kuwa zimegoma kutokana na mtikisiko wa kusafirishwa kutoka mikoani,” alisema James Mwandumbya aliyefika kujiandikisha.
Maeneo ya Pugu Kigogo Fresh (Stesheni) waandikishaji walielemewa na wingi wa watu na kulazimika kutoa namba ili wengine waende siku nyingine.
Katika kituo cha Shule ya Msingi Mtambani, Kinondoni, wananchi walilalamika gharama za uendeshaji ambazo wameombwa wachangie ili kufanikisha uandikishaji uendelee kama ulivyopangwa.
Katika Kituo cha Shule ya Msingi Makuburi, Ofisa mwandikishaji, Karim Mweneghoha alisema walikumbwa na changamoto ya umeme iliyochangiwa na kukosekana kwa waya za kuunganisha kutoka kwenye soketi kwenda kwenye mashine.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Julius Mallaba alikiri kupokea taarifa kutoka katika baadhi ya maeneo na kudai kuwa tayari ufumbuzi umepatikana.
“Kuna taarifa nilipokea asubuhi kwamba uandikishaji unaendelea, ngoja niwasiliane na ofisa uandikishaji ili nijue (changamoto) ndipo niweze kuzungumzia vyema jambo hili,” alisema. Awali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambayo ndiyo inahusika na shughuli hiyo ilisema mashine zaidi ya 8,000 zitatumika ili kufanikisha shughuli hiyo baada ya kukamilika uandikishaji mikoani.
Imeandikwa na Beatrice Moses, Julius Mathias, Bakari Kiango na Colnely Joseph.
               Habari toka: http://www.mwananchi.co.tz

Mbowe: Watanzania Mtuvumilie


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Magomeni, jijini Mwanza jana. Picha na Michael Jamson 
By Waandishi wetu
Mwanza/Dar. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema chama chake kimeshindwa kumtangaza mgombea wake wa urais kama ilivyotarajiwa jana, badala yake kikawaomba Watanzania kutokuwa na haraka, wasiwasi wala mihemko na kuwa muda ukifika kitamtangaza.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Magomeni jijini hapa, Mbowe aliwaomba wananchi kuuvumilia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa sababu viongozi wake wanaendelea na majadiliano na watakapokubaliana watamtangaza mgombea wao.
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema ilikuwa wamtangaze mgombea urais kama ilivyoripotiwa na gazeti hili, lakini wenzao wa CUF wamewaomba kuwa wanaendelea na vikao vyao vya chama.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema: “Wengi wana hamu ya kutaka kujua mgombea urais wa Chadema, naomba niseme kwamba tumekuja Mwanza kwa mambo mawili, kuja kuwapokea makamanda hawa wawili na kuitokomeza CCM.
“Ukawa itamsimamisha mgombea urais ambaye Oktoba lazima aiondoe CCM madarakani, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Magdalena Sakaya) ametuomba tena tusubiri hadi tarehe 25 (Jumamosi), kwani watakuwa na kikao cha Baraza Kuu la chama hicho, hivyo tunawasubiri wenzetu.”
Mbowe aliyetumia mkutano huo kuwakabidhi kadi wanachama wapya waliotoka CCM na kujiunga Chadema, Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya, aliweka msisitizo:
“Muungano wetu wa Ukawa ni wa msingi sana, kuna changamoto, tunaomba wananchi muwe wavumilivu, tuache mihemko ili tufikie uamuzi sahihi.
“Tunaomba mtuvumilie, hatuwezi kumtangaza mgombea wetu kwa sababu tu CCM wametangaza wa kwao, hapana! Tutamtangaza mgombea wetu na nyote mtafurahi,” alisema Mbowe huku akishangaliwa na maelfu ya wananchi.
Alisema, Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi alikuwa ahudhurie mkutano huo lakini kutokana na foleni za Dar es Salaam alishindwa kuwahi ndege na kwamba, viongozi wengine wa CUF na NCCR Mageuzi walialikwa lakini walikuwa na vikao vya vyama vyao.
Mbowe alisema Ukawa ni mpango wa wananchi, siyo wa viongozi na kwamba ulianzishwa Dodoma na viongozi wote wa upinzani na Kundi la Wabunge 201 wa Bunge Maalumu la Katiba walihudhuria, lakini baadhi yao walipenyezewa ‘kitu kidogo’ wakaondoka hivyo kubaki vyama vinne vya siasa.
Udini, ukabila wamkera
Mbowe alionyesha kusikitishwa na kauli alizodai kutolewa na viongozi wa CCM, kumnadi mgombea wao kwa ukabila na kuwataka wananchi kuwakataa wanaotumia mbinu hizo kwani hali hiyo inaweza kusababisha machafuko.
“Nafurahishwa sana na kauli zinazotolewa na viongozi wa CCM, tunampata kiongozi kwa ukabila! Ukawa hatutamchagua mgombea wetu kwa misingi ya ukabila wala udini, huo ni upumbavu,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Msikubali kurudisha ukabila wala udini, hapa uwanjani tupo makabila mengi, Wasukuma mpo! Wahaya, Wachaga, (Ezekiel) Wenje (Mbunge wa Nyamagana) ni Mjaluo yupo hapa.”
Alisema Watanzania wanataka mabadiliko na kwamba hali hiyo imeshuhudiwa wakati wa uandikishaji wa daftari la wapigakura.
Aonya wizi wa kura
Mbowe alisema hawatakuwa na tatizo iwapo ushindi utapatikana kwa njia za haki, lakini hawatakuwa na suluhu iwapo utatumika wizi wa kura kumuingiza mgombea madarakani.
“Hatutapiga magoti na kuomba, kama ushindi utapatikana kwa njia halali hatuna tatizo, lakini tukiona mambo yanakwenda ndivyo sivyo tunasema polisi mtatusamehe, mabomu hayatatosha,” alisema Mbowe.
Lembeli, Bulaya waombewa msamaha
Mbowe alisema Chadema kina maadili yake na kwamba Lembeli na Bulaya waliokuwa CCM wametenda mengi lakini anawaombea msamaha.
“Naomba muwasamehe. Wangapi wanasema tuwasamehe?” alihoji Mbowe huku akiitikiwa kwa sauti, “Woteee”.
Alisema viongozi hao ni miongoni mwa wengi wanaokaribia kutimka CCM na kuwapongeza kwa ujasiri wao makini walioonyesha.
Aahidi kutaifisha viwanja vya CCM
Baada ya kueleza jinsi alivyompigia simu bila mafanikio Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo kuomba kutumia Uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya mkutano huo, Mbowe alisema Serikali ya Ukawa ikiingia madarakani itahakikisha viwanja vyote vilivyojengwa na wananchi vinavyohodhiwa na CCM vinarejeshwa kwenye halmashauri.
“Chadema kwa kushirikiana na Ukawa, viwanja vyote vilivyojengwa na wananchi vitarejeshwa kwenye halmashauri ili vitumiwe na wananchi wote,” alisema baada ya baadhi ya wanawake kuzidiwa na kuanguka kutokana na wingi wa watu na ufinyu wa uwanja wa Magomeni.
Wagombea kulishwa yamini
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa aliwata wagombea ubunge waliopitishwa ambao wana mawazo ya kuuza nafasi zao kwa CCM kujiengua mapema kabla chama hakijawachukulia hatua.
Pia, Dk Slaa alisema chama hicho kitatoa fomu maalumu ambazo zitasainiwa na wagombea ubunge mahakamani ili kiweze kuwachukulia hatua za kinidhamu watakaokwenda kinyume na taratibu za chama hicho.
“Majimbo 157 yamekamilisha leo (jana), sisi Chadema hakuna jimbo ambalo mgombea atapita bila kupingwa kama wanavyofikiri CCM,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Tutatoa fomu za uteuzi ambazo wote waliopitishwa kugombea ubunge watasainishwa mahakamani, naomba niseme atakayeuza jimbo atashughulikiwa, kama mtu anataka kujitoa ajitoe mapema.”
Dk Slaa alisema miaka 10 iliyopita wananchi waliahidiwa maisha bora kwa kila Mtanzania, lakini yamegeuka na kuwa kinyume, sasa ni maisha magumu kwa kila Mtanzania.
“Waswahili wanasema ukiumwa na nyoka hata jani likikugusa unakimbia, miaka 10 mliahidiwa maisha bora kwa kila Mtanzania, leo ni maisha magumu kwa kila Mtanzania. Cha kwanza tunachokisimamia Chadema ni kurudisha nchi kwa wananchi, CCM wamepoka madaraka ya wananchi na kuyaweka mikononi mwa wachache, tunawaambia mwisho wao ni Oktoba,” alisema Dk Slaa.
Lembeli afunguka
Akizungumza kwenye mkutano huo, Lembeli alisema: “Nakumbuka tarehe 16 nilisali nikiwa kijijini kwetu na mama yangu mzazi, nikamwomba Mungu anitoe nchi ya laana anipeleke nchi ya matumaini.
Tarehe 17 nikafanya uamuzi, sasa nipo uwanjani, naomba niwaambie sijaja Mwanza hivihivi nimekamilika, nilipotoka nimeaga.”
Lembeli aliongeza: “Nimezoea kusema msemo wangu huu, hebu kunja ngumi... koroga... peoples,” umati wa watu uliitikia “Power”.
Kabla hajahutubia, Lembeli alibisha hodi Mwanza kwa kusema: “Hodi…hodi, aliitikiwa kwa sauti na umati uliohudhuria: “Karibu baba, karibu.”
Bulaya ampa salamu Wasira
Akihutubia baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama, Buyala alianza kwa kuwauliza wananchi: “Nikamtoe? Nauliza, nikamtoe? Nikamtoe nani?” wananchi walijibu kwa sauti kubwa: “Wasira... kamtoe Wasira.”
Bulaya alisema ni bora kama Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Stephen Wasira anamsikia akaondoka kama alivyomshauri Makongoro Nyerere.
“Makongoro Nyerere alisema, awamu ya kwanza upo, awamu ya pili upo, ya tatu upo ya nne upo ya tano mwisho wake umefika sasa,” alisema Bulaya.
Alisema kwa Mkoa wa Mara yupo mwenyekiti wake, Vicent Nyerere ambaye atafanya naye kazi kwa karibu na kwamba yeye na wenzake wa Chadema ni muziki mnene na jeshi kubwa.
Lissu na kabila la CCM
Akihutubia kwenye mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliwalinganisha, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Andrew Chenge na Spika Anne Makinda kwamba hawana tofauti na mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli, kwa sababu wote ni kabila moja la CCM.
“Nimefanya mikutano mingi, kila mahala nilipokwenda nilikuwa naambiwa Dk Magufuli kabila lake ni Msukuma, wengine Msubi na wapo waliosema Mzinza, mimi naomba niwaambie kwamba kabila moja la CCM ndilo la Dk Magufuli,” alisema Lissu.
Alisema Dk Magufuli ndiye aliyeuza nyumba za Serikali nchi nzima, kauli ambayo ilitiliwa mkazo na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari ambaye alisema watumishi wa umma wanaishi kwenye nyumba za vichochoroni kutokana na Dk Magufuli kuuza nyumba za Serikali.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Chadema, Arcado Ntagazwa ambaye aliwahi kuwa waziri na naibu waziri kwa miaka 15 alisema: “Safari hii kwa Chadema na washirika wao wa Ukawa ni moja kwa moja Ikulu.
Goli la mkono laibuka
Ntagazwa alisema: “Mambo ya kusema goli la mkono, watambue kwamba Oktoba ndiyo mwisho wa ufisadi,”
Kauli hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye alisema mwaka huu goli la mkono litawageukia wao... “Wakijifanya wao ni watoto wa kihuni makamanda wa Chadema ni wahuni zaidi yao.”
Kuhusu kucheza rafu, Mwalimu alisema wanaotarajia kucheza rafu kwenye uchaguzi mkuu ni wazi kwamba wameshindwa kucheza uwanjani.
“CCM kutangaza kushinda hata kwa goli la mkono ni wazi kwamba wameshindwa kucheza uwanjani sasa sisi tutawafuata hukohuko nje ya uwanja na tutawabana,” alisema Mwalimu.
Wenje, Kiwia watamba
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje na Highness Kiwia, walisema kwa sasa wapo likizo ya miezi miwili na wanatarajia kuapishwa tena kuwa wabunge baada ya uchaguzi.
Kiwia alisema: “Mimi ndiye rais wa Jamhuri ya watu wa Ilemela, sina shaka tumemaliza kura za maoni sasa nasubiri tena kuwa Mbunge wa Ilemela.”
Akihutubia, Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini, alisema kazi inaendelea na kinachofanyika sasa ni kuhakikisha CCM inaondoka madarakani Oktoba.
Leo viongozi hao wa Chadema watakuwa na mkutano mwingine mjini Mbeya na baadaye Arusha na Jumatatu ni Dar es Salaam.
Imeandikwa na Midraji Ibrahim, Aidan Mhando na Fidelis Butahe.
            Habari kutoka: Mwananchi