Tuesday, 12 January 2016

...SHEIN AJIBU MAPIGO, ASEMA ‘JIANDAENI KWA UCHAGUZI’

                      ...SHEIN AJIBU MAPIGO, ASEMA ‘JIANDAENI KWA UCHAGUZI’


Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein      
Kuna kila dalili kwamba mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mkwamo wa kisiasa Zanzibar yamevurugika baada ya wahusika wakuu wa pande mbili, kuzungumza hadharani na kutoa misimamo tofauti.

Wakati Maalim Seif Sharif Hamad wa CUF akiitisha mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kusema chama chake hakipo tayari kuona uchaguzi unarudiwa, Dk Ali Mohamed Shein wa CCM amewataka wafuasi wa chama hicho kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio.
Akihutubia mkutano maalumu wa CCM wa maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar, uliofanyika Viwanja vya Maisara Suleiman, mjini hapa, Dk Shein amewataka wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio pindi Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) itakapotangaza tarehe.
Rais huyo wa Zanzibar alisema jana kwamba huo ndiyo msimamo wa chama chake na hakijatafuna maneno tangu ZEC ilipotangaza uamuzi wa kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015

1 comment:

 1. Habari..
  Nimepitia katika blog yako na nmegundua kwamba kuna upungufu wa baadhi ya vitu muhimu
  na blog yako sio ya kuvutia sana wasomaji wako. Rangi zilizotumika sio nzuri yaani kwaujumla blog haiko katika muonekano mzuri.
  TECH4GENIUS PRIMIER CO.LTD tunatoa huduma mbalimbali za IT hivyo tunashauri kwamba ni vizuri website yako iwe na muonekano mzuri na wa kuwavutia wasomaji ili wasichoke kusoma kila ulichokiandika kila siku katika site yako. Sisi tunatoa huduma hiyo ya WEBSITE (or blog)design na kuifanya blog yako iwe more attractive, modern,responsive and User friend. Utawekewa features nzuri za kuvutia ambazo hazipo.
  Huduma hii ni kwa gharama ndogo tu ya US $40.
  Huduma nyingine ni kama: CCTV INSTALLATION, GPS CAR TRACKING INSTALLATION, GRAPHIC DESIGN,WAITER CALLING SYSTEM INSTALLATION, COMPUTER MAINTENANCE na nyingine nyingi.
  Kwa mawasiliano : 0768760710, 0652001711. Email: infotech4genius@gmail.com ,
  Das es salaam tunapatika Magomeni.

  Asante ,siku njema

  ReplyDelete