Friday, 5 June 2015

UJENZI WA BARABARA YA MAKONDE,MAWENGI WILAYAN LUDEWA WAZINDULIWA RASMI

UJENZI WA BARABARA YA MAKONDE,MAWENGI WILAYANI LUDEWA WAZINDULIWA RASMI

                            Filikunjombe akizindua rasmi ujenzi wa barabara ya Mawengi kwenda Makonde                                                       mtambo ukiwa kazini


                                    Filikunjombe akikagua barabara mpya ya Mawengi Makonde

Filikunjombe akiwa amechoka kutembea kutoka kata ya Mawengi kuelekea kata ya Makonde,nyuma yake ni katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw.Onoratus Mgaya
                              Hii ndiyi barabra inayotoka kata ya Mawengi kuelekea kata ya Makonde

                   Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.Willium Waziri akiongea na wananchi


 Filikunjombe akiongea na wananchi wa kata za Makonde,Lifuma na Mawengi mara baada ya uzinduzi

Ujenzi wa barabara ya kijiji cha Mawengi kwenda kata za Makonde na Lifuma  mwambao wa ziwa Nyasa wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kwa kiwango cha changalawe umezinduliwa rasmi jana na mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe


Akizindua ujenzi wa barabara hiyo inayofadhiriwa na ubalozi wa Japani Filikunjombe alisema kwa miaka mingi wananchi wa kata za mwambao wa ziwa Nyasa wamekuwa wakitumia usafiri wa majini katika shughuri zao mbalimbali lakini Serikali ya chama cha mapinduzi imekisikia kilio cha watu wa mwambao hivyo imeona ni bora kutoboa barabara inayofuka katika kata hizo ili kurahisisha maisha ya wananchi.


Filikunjombe alisema kuwa wananchi wa mwambao wa ziwa nyasa wamekuwa wakipata mahitaji yao kupitia wilaya jirani ya Kyela kutokana na kutokuwa na barabra ya gari inayoweza kuwafikisha katika makao makuu ya wilaya yao hivyo ujenzi wa barabara hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa kata za Makonde na Lifuma.


Hata hivyo aliwataka wakandarasi wa mradi huo wa barabara kuwa waaminifu na kufanya kazi kwa umakini mkubwa kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi na wakandarasi kutokuwa waaminifu kwa kuiba vipuli na mafuta ya mitambo hali ambayo inarudisha maendeleo nyuma. 


Filikunjombe alisema imekuwa ni tabia mbaya inayoendelea kuzoeleka nchini ya wizi wa mafuta wakati Serikali imepanga bajeti ya kutosha katika matengenezo ya barabara mbalimbali lakini baadhi ya watu hutumia miradi hiyo kujinufaisha kwa kuiba vipuli na mafuta hivyo atakayebainika katika ujenzi wa barabara zote wilayani Ludewa Sheria itachukua mkoando wake.


“Leo tunazindua ujenzi wa barabara ya Mawengi kwenda Makonde ni barabara ambayo inaumuhimu mkubwa kwa wananchi wa mwambao lakini wako watu wanafikiria kuiba mafuta ya mitambo na vipuli,nawaomba tabia hiyo ikome mara moja kwani serikali imeona ilifanye hili ili kuwaletea maendeleo wananchi wa maeneo haya hivyo nalioamna jeshi la polisi yeyote atakayebainika akamatwe na afikishwe mbele ya sheria lakini nawaomba wananchi kuwa walinzi wa miradi yenu ili ikamilike haraka”,alisema Filikunjombe.


Barabara hiyo ambayo itaziunganisha kata tatu na vijiji vingi vya mwambao wa Ziwa Nyasa inakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo kutokana na wananchi wengi kuwa na shauku ya kufanya biashara ya samaki kwa kiasi kikubwa tofauti na awali walikuwa wakibeba samaki kwa kichwa na kutembea umbali kwa kilomita 34 hadi mawengi kwaajili ya kuziuza na kujipatia kipato.


Aidha Bw.Erasto Magombola mkazi wa kijiji cha mawengi alisifu Serikali kwa kuiangalia barabara hiyo kutokana na wananchi wa maeneo ya mwambao kusafirisha wagonjwa hadi kijiji cha mawengi kwa kuwabeba katika mchela hivyo barabara hiyo ni ukombozi mkubwa kwao.


Bw.Magombola alisema kuwa kutokana na ujenzi wa barabara baadhi ya wafanya biashara wa sanmaki na maharage watapata fulsa ya kufanya biashara hiyo kwa urahisi kwani samaki wa ziwa Nyasa wamekuwa wakiuzwa zaidi wilaya ya Kyela wakati wavuvi wako wilaya ya Ludewa haya yote yalisababishwa na ubovu wa barabara.


Kuhusu wizi wa mafuta Bw.Mgombola alisema kuwa yeye kama mwananchi na muhasibu wa kijiji cha Mawengi atashirikiana na uongozi wa kijiji na kata kuwazibiti wezi hapo na hawatawafumbia macho mafanyakazi wa mradi huo ambao watakwenda kinyume na maadili ya kazi zao.


Mwisho. Tukio hili lilifanyika Tarehe 14 mwezi wa tano 2015. 
                                               Habari na Habari Ludewa Blog

No comments:

Post a Comment