Saturday, 15 August 2015

Mtoto apata mtoto Paraguay

Kampeni imeanzishwa kupinga ubakaji kwasababu ya kisa cha binti huyo.
Binti wa miaka kumi na mmoja nchini Paraguay aliyedai kubakwa na baba yake wa kambo amejifungua mtoto wa kike baada ya mamlaka nchini humo kumzuia asitoe ujauzito aliokua nao.
Madaktari katika mji mkuu wa Asuncion wamesema binti huyo na mtoto wake aliyejifungua kwa njia ya upasuaji wanaendelea vizuri.
Tukio hilo limesababisha utata mkubwa nchini Paraguay na katika mitandao ya kijamii, Paraguay ni taifa linaloamini zaidi katika Ukatoliki ambapo mwanamke anaruhusiwa kutoa mimba pale tu afya yake inapokuwa hatarini.
Binti huyo alibakwa alipokua na umri wa miaka kumi pekee na Baba yake wa kambo mwenye miaka arobaini na miwili yupo rumande akisubiria kutajwa kwa kesi yake wakati huo huo baba huyo amekanusha kuhusika katika tukio hilo.
                                  Habari na: BBC

No comments:

Post a Comment