Monday 29 June 2015

BLACK FIRE MABINGWA KOMBE LA MBUNGE CHIKAWE JIMBO LA NACHINGWEA, MKOANI LINDI

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea akizungumza na wanamichezo (hawapo pichani) kabla ya kuanza fainali ya Kombe la Chikawe katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo na Timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa zilipambana na Timu ya Black Fire iliibuka mshindi kwa magoli 3 kwa 1. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
Kapteni wa Timu ya Black Fire, Ally Njaidi (kulia) akipokea fedha taslimu Shilingi 500,000 pamoja na Kikombe cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema, baada ya kumalizika fainali ya Kombe la Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Timu hiyo iliirarua timu ya Motisha mabao 3 kwa 1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salimu Mwalimu, naye alihudhuria fainali ya mashindano hayo ambayo yalianzishwa na Mbunge Chikawe jimboni humo kwa kushirikisha timu 178 katika jimbo hilo.
  
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea akimsalimia mchezaji wa Timu ya Black Fire, Faraji Mohamed wakati alipokuwa anaikagua timu hiyo kabla ya fainali ya Kombe la Chikawe ambayo yalifanyika katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo iliibuka kidedea baada ya kuinyuka Timu ya Motisha, Kata ya Kilimani magoli 3 kwa 1. Nyuma ya Waziri Chikawe ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.

Kapteni wa Timu ya Motisha, Saidi Chakupewa (kulia) akipokea zawadi ya ushindi wa pili, kikombe na fedha taslimu Shilingi 200,000 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema, baada ya kumalizika fainali ya Kombe la Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Timu hiyo ilifungwa na Timu ya Black Fire mabao 3 kwa 1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salimu Mwalimu, naye alihudhuria fainali ya mashindano hayo ambayo yalianzishwa na Mbunge Chikawe jimboni humo kwa kushirikisha timu 178 katika jimbo hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (aliyevaa kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Black Fire ambao ndio waliibuka washindi. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (aliyevaa kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
Msanii maarufu wa bongofleva, Seleman Jabir ‘Msaga Sumu’ akitumbuiza katika fainali ya Kombe la Chikawe lililofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Katika fainali hiyo, Timu ya Black Fire iliibuka kidedea baada ya kuifunga timu ya Motisha magoli 3 kwa 1.
Mchezaji wa timu ya Black Fire (kulia) akisakata kabumbu katika fainali ya kombe la Mbunge Chikawe lililofanyika katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu hiyo ya Black Fire iliinyuka timu ya Motisha magoli 3 kwa 1. Picha zote na Felix Mwagara.

No comments:

Post a Comment