Thursday, 29 January 2015

PROFESA LIPUMBA HOI AKIWA MAHAKAMANI, AKIMBIZWA HOSPITALI.....KESI YAKE YAAHIRISHWA

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof.Ibrahimu Lipumba hali yake 
kiafya sinzuri baada ya kubadilika gafla wakati akiwa katika mahakama kuu ya
Kisutu Jijini Dar es Salaam na hivyo kukimbizwa katika Hospitali ya UN 
kinondoni DSM.
Lipumba alifikshwa mahakamani  hapo na kusomewa mashitaka ya kuongoza 
 maandamano haramu.Profesa huyo  akiwa na wafuasi wake wameachiwa kwa 
 dhamana na kesi yao itasomwa tena tarehe 26 February Mwaka 2015
 
Ikumbukwe  kwamba, Lipumba  alikamatwa  jana  na  jeshi  la  polisi  kanda
  maalumu  ya  Dar  es  salaam  wakati alipokuwa akielekea eneo la 
Zakhem, Mbagala, kulikokuwa kumeandaliwa mkutano wa hadhara, kutoa
 taarifa kwa wafuasi waliokuwa wamekusanyika, kuwa mkutano na
 maandamano yamezuiliwa na Polisi.

No comments:

Post a Comment