Behind the scene; kifo cha betty.!
Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa itamuudhi kila mtu
anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa wengine. Lakini siku
zote ninaamini katika busara hii: kuuchukia ukweli hakubadilishi ukweli
kuwa uongo. Ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa
uongo, na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli. Kamwe asilani. Wakati
tunaomboleza kifo cha ndugu yetu betty ndejembi watu wamesema mengi, na
yameandikwa mengi. Kila mmoja kwa namna alivyoguswa. Zitto kabwe
ametweet hivi asubuhi "justice for betty", akitoa rai haki ipatikane
kwenye kifo cha betty.
Jokate mwegelo nae ametweet kuomba msaada wa kuchunguza kifo cha betty.
Na watu wengine maarufu kila mmoja kasema neno, labda kwa sababu betty
alikua maarufu in one way or another. Lakini hatuwezi kukwepa ukweli
kwamba siku chache kabla ya kifo chake, alinyanyaswa mno kwenye mtandao
wa kijamii wa twitter.
Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa moja uhusiano kati ya
unyanyasaji huo na kifo chake, lakini mtu akinyanyaswa masaa kadhaa
kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha flani. Saa chache kabla ya
kifo chake betty alitweet kua "pinda hawezi kuwa rais". Baada ya kutweet
hakuonekana tena hadi alipookotwa mtaroni kesho yake asubuhi akiwa
amefanyia vitendo vya kikatili na akiwa amepoteza fahamu.
Lakini kabla hata ya kutweet hivyo, betty alikua anaandamwa sana
mtandaoni huko twitter. Kuna watu walianzisha team ya kumtukana, kumjibu
hovyo na kumprovoke kwa kila alilofanya. Naomba ieleweke kuwa simlaumu
mtu kwa sababu sina mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala hii ni
rambirambi zangu kwa betty kuzungumzia tatizo la unyanyasaji mtandaoni,
sambamba na suala zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususani cha mtu
maarufu. Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni.
Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi,
wambeya, wanafiki. Wanaochafua wenzao, kutishia wenzao kwa kujifanya
askari jkt, kusengenya na kupost majungu.... Aina ya binaadamu
wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza.
Kwenye hii mitandao, matusi imekuwa njia ya mkato ya kupata umaarufu.
Kuna wenzetu wengi tu wenye 'umaarufu' huko twitter, facebook na
instagram lakini ukidadisi chanzo cha 'umaarufu' huo, utaambiwa 'ah huyu
ana matusi si mchezo!' Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda
mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si
kusherehesha unyanyasaji huo. Marehemu betty ni victim wa yote hayo.
Alitukanwa sana, na aliitwa majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya
kukutana na mauti. Kuna waliomwita di maria, superstar uchwara etc.. and
i hope hao waliomuita hivyo wanajifahamu na wengine wananisoma hapa.
Japo sijui chanzo cha 'ugomvi' wao, lakini naamini kuna watu wengi tu
waliokuwa katika nafasi ya kuzima moto huo kwa vile walikuwa
wakizifahamu pande zote mbili za 'ugomvi' husika lakini kwa sababu ya
unafiki wakapalilia moto maana wanafurahi watu wakigombana.
La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza wakati wa maombolezo haya
ni unafiki. Watu walewale waliodiriki kumwandama marehemu wakati wa uhai
wake watageuka kuwa wenye uchungu mkubwa baada ya kifo chake. Hii
inanikumbusha suala ambalo nimeshawahi kulizungumzia mara kadhaa kwamba
'wakati muafaka wa kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye misiba: watu
walewale waliokuwa wakikuchukia kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu
mkubwa kwa kifo chako.' Ukiangalia baadhi ya tweets za mwisho za
marehemu ni wazi kuwa binti huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa
wanaomjali. Mojawapo ya tweet za mwishomwisho za marehemu alisema hivi
"do i have a sister to support me? No.
Do i have a dad/mom to run to or support me. No. Im hurting and wanna cry? Yes.
But i know god is watching" haihitaji degree ya saikolojia kujua kuwa
betty alikua kwenye kipindi kigumu mno na alihitaji msaada kwa watu
waliokua karibu yake. Betty anauliza"nina dada wa kunisaidia? Hapana.
Nina baba au mama wa kumkimbilia? Hapana. Nimeumizwa/nina uchungu na
ninahitaji kulia (lakini nitamlilia nani?). Ila najua mungu anaona" kwa
bahati mbaya betty hakuwa na baba, hakuwa na mama, hakuwa na dada wala
kaka. Wote walishatangulia mbele ya haki.
Alibaki peke yake, peke yake na mungu wake. Lakini binadamu wasivyo na
aibu wala huruma wakazidi kumtukana na kumsimanga, huku wengine
wakiporomosha matusi mazito. Hawakujua yaliyokua moyoni mwake.
Wakamtambia kwa maisha mazuri wanayoishi na namna walivyobarikiwa. Betty
akiwa katika maumivu makali ya hisia akapost hivi "thank you all for
the names i was called, luck y'all have such a perfect life.! No hard
feelings.. Im alive still.! Endeleeni kuongea" kwa tafsiri isiyo rasmi
betty alisema "asanteni kwa majina yote mliyoniita. Mmebarikiwa kuwa na
maisha mazuri.! Hamuumizwi na hisia kama mimi.
Ila bado ninaishi, endeleeni kuongea" kwa bahati mbaya hakuna
aliyejali, hadi juzi asubuhi (jumatano) betty alipookotwa kwenye mtaro
akiwa amefanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na akiwa amepoteza fahamu. Kifo
cha betty ni miongoni mwa vifo vya kikatili sana kuwahi kutokea nchini.
Nashauri wanaharakati ea haki za wanawake wapambane kuhakikisha haki
inapatikana.
Akina annanilea nkya, hellen kijobisimba watafute haki ya binti huyu
kzma zitto kabwe alivyosema "justice for betty" imagine mtu aliyekua
kwenye maumivu makali ya hisia, anatekwa na genge la wahuni. Bila kujali
kipindi kigumu alichokua anapitia, bila kujali hakua na wazazi, bila
kujali psychological toacher aliyokua nayo still wanamfanyia unyanyasaji
wa kijinsia hadi anapoteza fahamu.
Betty aliokotwa mtaroni na kupelekwa hospitali. Jana (alhamisi) aliweza
kufungua macho, lakini hakuweza kuongea lolote hadi saa 3 usiku wa
kuamkia leo, mauti ilipomkuta. Kwaheri betty, kwaheri classmate wangu
(majengo sec), kwaheri rafiki, kwaheri ndugu. Umeondoka dunia bado
inakuhitaji. Naumia u have gone too young, lakini naumia zaidi coz
umekufa kikatili mmno.
Japo sijui nitakufaje, lakini nadiriki kusema hukustahili kifo cha aina
hii. Nakumbuka sms yako ya mwisho kwangu uliniambia hivi "malisa blv me,
only youths can change this country". Leo nilipopata taarifa ya kifo
chako nimerudia kuisoma sms yako mara mbilimbili.
Sikujua kua sms hiyo ndo ulikua unaniaga. Umeniaga kwa kutuachia vijana
wosia, kuwa vijana pekee ndio wenye uwezo wa kuibadilisha nchi hii.
Nitakua nimekusaliti ikiwa sitautendea kazi wosia huu. I promise to
fight and motivate other youths to liberate this country for ur
dedication. Umekwenda kumfuata mama yako, umemfuata baba yako. Wazazi
wako walitangulia, leo wewe umewafuata. Hatimaye familia nzima mmekutana
paradiso.
Pumzika kwa amani betty.!`

By
Malisa Godlisten
Okey. Hii habari nimeiandika mimi. Bila shaka
aliyeiweka hapa ameitoa kwenye ukurasa wangu wa facebook. Betty alikua
schoolmate wangu Majengo sekondari, baadae akaenda UDOM nami SAUT.
Nimeona baadhi ya maswali yaliyojitokeza na possibly aliyeiweka mada
hapa ameshindwa kujibu though ukweli mada ipo wazi. Kuhusu alipookotwa
Betty ni Mikocheni. Kuhusu utaratibu wa kuagwa ni kesho Muhimbili,
kuhusu maziko yatafanyika Dodoma. Kuhusu waliokua wanamharass kwny
social media ni pamoja na Diva wa Clouds fm (nimeattach post ya Diva
inayoonesha as if kafurahia kifo cha Betty).
Kuhusu umaarufu alikua mwanamitindo wa Swahili fashion together with
Mustapha Hassanali na Jokate Mwegelo. Na ofcoz alishaanza kuwa maarufu
kwny hayo mambo ya mitindo.
Anyway kama mnataka kujua umaarufu wake alikua mwanamitindo wa Swahili
Fashion na partners wake wakiwa Mustapha Hassanali and Jokate Mwegelo.
Waliouliza may be sio wafuatiliaji wa masuala ya fashion ndo maana
hawamjui, but wengi wanaofuatilia issues za mitindo they know her.
Hatahivyo sijaandika makala hii kwa ajili ya umaarufu wake. Nimeandika
coz nimeguswa sana na kifo chake. She was my schoolmate at Majengo, and
last year she graduated UDOM, B.A International Relations bt akaamua
kujikita kwny mambo ya modeling.
However sidhani kama ni sahihi kujua mtu ni nani ndo umtetee. Wote
mliouliza huyu dada ana umaarufu gani, did u mean ktk kutetea haki
inatakiwa kwanza umjue mtu? Km ndivyo mlivyomaanisha i think mmekosea.
Either mnamjua Betty au hamumjui itz not an issue. The issue ni
aliyofanyiwa. Je alistahili?
Tusiposema sisi tulio hai kwa kuwa tu hatumjui, nani atasema? Je mnataka
Betty aibuke kutoka kwny mauti aje kutetea haki yake? Kumbukeni the
dead cannot cry out for justice. It is a duty of the living to do so for
them.!
So hata kama Betty angekua a mere citizen ktk nchi hii asiyejulikana na
yeyote we could still plee for her justice. We could still shout
"JUSTICE FOR BETTY"
Im here to answer anymore question kwa ambaye hajaelewa Makala yangu.
MALISA GJ.!

Makala hii imeandikwa na By
Malisa Godlisten