Tuesday, 28 July 2015

Lowassa na mkewe wakabidhiwa kadi rasmi za chama cha chadema


Waziri mkuu mstaafu Mh: Lowasa leo amekabidhiwa kadi ya uanachama wa chama cha chadema katika hoteli ya bahari beach, kadi hizo zimetolewa kwa lowasa pamoja na mkewe, na mheshimiwa lowasa amesema yeye hana mpango wa kulipa kisasi kama watu wengine wanavyohisi badala yake amesema kama kunamtu anahisi kwamba anamakosa na anaogopa lowasa atalipa kisasi asiogope na badala yake aende mbele za Mungu na kuomba asamehewe. Viongozi wote wa UKAWA wamelizia kunpokea Lowasa.

Rich Mond:
Kwa suala la RICHMOND amesema kwa mtu yeyote mwenye ushahidi na tuhuma hizo ampeleke mahakamani na aache kupiga kelele.

SALAMU:
Dr Makaidi: Anaanza kwa kutoa Salamu kwa , MBowe, Lipumba, Mbatia na Lowasa ambazo zimetoka chama cha chake Cha NLD, na kutaka LOwasa asahau mambo ya CCM na kufuata ya UKAWA.

Makamu / mwenyekiti CUF, Anaanza kwa kutoa Salamu kwa , MBowe, Makaidi, Mbatia na Lowasa na kusema amepigwa na butwaa na kusema ukawa wamepata jembe.
 NCCR MAGEUZI: Anaanza kwa kutoa Salamu kwa , MBowe, Lipumba, Makaidi na Lowasa na kusema wataendelea kulinda hazi za Mh: Lowasa za kuwa waziri mkuu mstaafu na kusema CCM haina haki miliki ya kuimiliki TANZANIA.
 CHADEMA: MBOWE:  Anaanza kwa kutoa Salamu kwa watu wote na kwa, Lipumba, Mbatia na Lowasa, Kwaniaba ya chadema anamkaribisha LOWASA na Familia na watanzania katika Familia ya CHADEMA, Anasema ujio wa Lowasa umezua hofu CCM, anasema alipigiwa simu na watu wa CCM nakuambiwa akimkaribisha Lowasa atakiharibu chama, na anaanza kuwatoa hofu wanachadema kwa kusema hasemi Lowasa ni mtakatifu bali pia chadema sio mahakama ya kuhukumu mtu bila ya ushaidi.

                                     Habari na www.hatasisitupo.blogspot.com

BASI LAGONGA TRENI YA MIZIGO NA KUUA WANNE - TABORA MJINI




Askari Polisi wakifanya ukaguzi kwa maiti zilizokutwa eneo la ajali hiyo

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Juma Bwire akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio la ajali mbaya iliyotokea eneo la kata ya Malolo manispaa ya Tabora ambapo watu wanne walikuwa wamepanda basi hilo la kampuni ya Dont Worry ambapo lilisababisha ajali hiyo baada ya kugonga treni ya mizigo,watu kadhaa wamejeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete.
Eneo la chini la basi hilo la kampuni ya Dont Worry ambalo lilisababisha ajali hiyo ambapo mbali na uzembe wa dereva lakini basi hilo lililokuwa likifanya safari zake kutoka Tabora mjini kwenda Ufuluma wilaya ya Uyui limeonekana sehemu hiyo ya chini imefungwa kamba za mipira kuzuia vyuma vinavyunganishwa na usukani visichomoke kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa maisha ya wasafiri.

Thursday, 23 July 2015

Mauzauza ya BVR yahamia Dar


Fundi wa mashine za Biometric Voters
Fundi wa mashine za Biometric Voters Registration (BVR) zinazotumika kuandikisha wananchi kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura, Neema Mbwambo akiirekebisha moja ya mashine hizo katika kituo kilichopo Shule ya Sekondari ya Zawadi, Tabata Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory 
By Waandishi Wetu
Dar es Salaam. Kasoro za uandikishaji wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura zilizokuwa zikitokea katika mikoa mbalimbali nchini, zimejitokeza pia jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya kwanza ya kazi hiyo.
Mwananchi ilipita katika maeneo mbalimbali jana na kushuhudia wananchi wengi wakiwa wamekutana na changamoto kadhaa kwenye baadhi ya vituo ikiwamo ya kukosekana mashine za Biometric Voters Registration (BVR).
Wananchi hao walisema licha ya kwamba Dar es Salaam imepewa siku 10 ya uandikishaji, kama changamoto hizo hazitachukuliwa hatua kazi hiyo inaweza isikamilike kwa wakati.
Miongoni mwa changamoto nyingine ni kuharibika kwa mashine zilizopo, ukosefu wa umeme, uchache wa watendaji na kuelemewa na watu, mtandao usio wa uhakika na nani aanze kuandikishwa kati ya wenye mahitaji maalumu na wasionayo.
Katika kituo cha uandikishaji cha Shule ya Msingi Oysterbay ambako kuna vituo vidogo vitano, wakala wa uandikishaji, Margereth Galway alisema mwitikio wa vijana umekuwa mkubwa kiasi kwamba inakuwa shida kuwapa nafasi ya upendeleo wazee, viongozi, walemavu au wajawazito na wanaonyonyesha.
“Eneo hili lina wazee na viongozi wengi wa chama na Serikali. Mwitiko mkubwa wa vijana unatufanya tushindwe kuwasaidia watu hao,” alisema Galway.
Alisema wasimamizi wote wa kituo hicho wamekubaliana kuwa kuanzia leo, wateue mashine moja na itengwe kwa ajili ya wenye mahitaji maalumu ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi wanaokuwa wamesimama kwenye foleni muda mrefu.
“Tayari wameshakuja Warioba (Jaji Joseph), Msekwa (Pius) na Butiku (Joseph) wakiwa na wake zao na kujiandikisha. Pamoja na kufahamika kwao bado vijana hawakuwa radhi kuwapisha wakitaka wajipange jambo ambalo ni gumu kulitekeleza.
“Kama tutafanikiwa kuwashawishi waandikishaji basi foleni za watu wa kawaida zitakuwa nne na moja itaachwa kwa ajili ya wenye mahitaji muhimu,” alisema.
Katika Kituo cha Shule ya Msingi Kawe A, wazee wengi walikutwa wamekaa kwenye madawati, nje ya madarasa wakisubiri kuandikishwa baada ya vijana kutokubali kuwapisha wakidai waandaliwe utaratibu ambao hautoingilia foleni iliyopoo.
Katika Shule ya Msingi Hekima iliyopo wilayani Kinondoni, kulikuwa na malalamiko kama hayo na wananchi wakaiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuweka utaratibu maalumu.
Mmoja wa waliofika kujiandikisha, Mwanaidi Abdallah alisema katika uandikishaji huo wanawake wamekuwa wakipata shida kutokana na utaratibu mbovu.
Alisema inachukua muda mrefu kupata huduma kwa sababu baadhi ya vijana wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kujiandikisha.
Katika kituo cha Mtendaji kilichopo Mtaa wa Mzimuni, Kata ya Kawe, wananchi walikutwa wakiwa nje saa 8:00 mchana wakisubiri mashine ili uandikishaji uanze licha ya kutangaziwa kazi hiyo ingeanza asubuhi.
Kitu pekee kilichokuwa kinaendelea ni wananchi kujiorodhesha kwenye daftari na kupewa namba ya foleni hadi mashine zitakapoletwa.
Mkazi wa Ununio Beach, Joseph Mrisho alisema licha ya wananchi kujitokeza kwa wingi kuna vituo viwili mashine ziligoma kufanya kazi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ununio Beach, Mwijuma Mwinyihija alisema usumbufu waliokumbana nao wananchi umesababisha malalamiko na wengine wamekataa tamaa na kuamua kuondoka kwenda kwenye shughuli zao za kujitafutia kipato.
Katika Kata ya Wazo Mtaa wa Salasala eneo la IPTL, hadi saa 9:00 alasiri wananchi walikuwa hawajaandikishwa kutokana na mashine kugoma.
Mkazi wa eneo hilo, Blandina Hizza alisema alilazimika kurudi nyumbani mara kadhaa akijipa matumaini huenda mashine hiyo itatengemaa ili aandikishwe, lakini hadi muda huo hakufanikiwa.
Frank Etta alisema: “Hatuelewi imekuwaje hadi sasa wahusika hawajaleta mashine.”
Kituo cha Shule ya Msingi Mlimani kilichopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambacho kinastahili kuwa na vituo vidogo vitatu, kina mashine moja tu iliyopelekwa.
Mwandikishaji Msaidizi katika kituo hicho, Isabella Mkumbwa alisema mwitikio wa watu ni mkubwa, lakini uandikishaji unakwenda taratibu kwa sababu watu wote wanatakiwa kusubiri mashine moja.
“Baadhi ya watu wameondoka ili wakaendelee na kazi zao. Tunasubiri mashine nyingine mbili ziongezwe wakati tukiendelea kuitumia hii iliyopo,” alisema msimamizi huyo.
Kituo cha Shule ya Sekondari Zawadi kiliyopo Tabata, uandikishaji ulikuwa haujaanza hadi saa 4:00 asubuhi wakati gazeti hili lilipotembelea kituoni hapo na kukuta mashine ikitengenezwa.
“Niliwahi kufika na nikapewa namba 23 ila tumeelezwa kuwa walimu wataanza kuandikisha pindi mashine zitakapotengamaa. Wamesema kuwa zimegoma kutokana na mtikisiko wa kusafirishwa kutoka mikoani,” alisema James Mwandumbya aliyefika kujiandikisha.
Maeneo ya Pugu Kigogo Fresh (Stesheni) waandikishaji walielemewa na wingi wa watu na kulazimika kutoa namba ili wengine waende siku nyingine.
Katika kituo cha Shule ya Msingi Mtambani, Kinondoni, wananchi walilalamika gharama za uendeshaji ambazo wameombwa wachangie ili kufanikisha uandikishaji uendelee kama ulivyopangwa.
Katika Kituo cha Shule ya Msingi Makuburi, Ofisa mwandikishaji, Karim Mweneghoha alisema walikumbwa na changamoto ya umeme iliyochangiwa na kukosekana kwa waya za kuunganisha kutoka kwenye soketi kwenda kwenye mashine.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Julius Mallaba alikiri kupokea taarifa kutoka katika baadhi ya maeneo na kudai kuwa tayari ufumbuzi umepatikana.
“Kuna taarifa nilipokea asubuhi kwamba uandikishaji unaendelea, ngoja niwasiliane na ofisa uandikishaji ili nijue (changamoto) ndipo niweze kuzungumzia vyema jambo hili,” alisema. Awali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambayo ndiyo inahusika na shughuli hiyo ilisema mashine zaidi ya 8,000 zitatumika ili kufanikisha shughuli hiyo baada ya kukamilika uandikishaji mikoani.
Imeandikwa na Beatrice Moses, Julius Mathias, Bakari Kiango na Colnely Joseph.
               Habari toka: http://www.mwananchi.co.tz

Mbowe: Watanzania Mtuvumilie


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Magomeni, jijini Mwanza jana. Picha na Michael Jamson 
By Waandishi wetu
Mwanza/Dar. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema chama chake kimeshindwa kumtangaza mgombea wake wa urais kama ilivyotarajiwa jana, badala yake kikawaomba Watanzania kutokuwa na haraka, wasiwasi wala mihemko na kuwa muda ukifika kitamtangaza.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Magomeni jijini hapa, Mbowe aliwaomba wananchi kuuvumilia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa sababu viongozi wake wanaendelea na majadiliano na watakapokubaliana watamtangaza mgombea wao.
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema ilikuwa wamtangaze mgombea urais kama ilivyoripotiwa na gazeti hili, lakini wenzao wa CUF wamewaomba kuwa wanaendelea na vikao vyao vya chama.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema: “Wengi wana hamu ya kutaka kujua mgombea urais wa Chadema, naomba niseme kwamba tumekuja Mwanza kwa mambo mawili, kuja kuwapokea makamanda hawa wawili na kuitokomeza CCM.
“Ukawa itamsimamisha mgombea urais ambaye Oktoba lazima aiondoe CCM madarakani, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Magdalena Sakaya) ametuomba tena tusubiri hadi tarehe 25 (Jumamosi), kwani watakuwa na kikao cha Baraza Kuu la chama hicho, hivyo tunawasubiri wenzetu.”
Mbowe aliyetumia mkutano huo kuwakabidhi kadi wanachama wapya waliotoka CCM na kujiunga Chadema, Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya, aliweka msisitizo:
“Muungano wetu wa Ukawa ni wa msingi sana, kuna changamoto, tunaomba wananchi muwe wavumilivu, tuache mihemko ili tufikie uamuzi sahihi.
“Tunaomba mtuvumilie, hatuwezi kumtangaza mgombea wetu kwa sababu tu CCM wametangaza wa kwao, hapana! Tutamtangaza mgombea wetu na nyote mtafurahi,” alisema Mbowe huku akishangaliwa na maelfu ya wananchi.
Alisema, Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi alikuwa ahudhurie mkutano huo lakini kutokana na foleni za Dar es Salaam alishindwa kuwahi ndege na kwamba, viongozi wengine wa CUF na NCCR Mageuzi walialikwa lakini walikuwa na vikao vya vyama vyao.
Mbowe alisema Ukawa ni mpango wa wananchi, siyo wa viongozi na kwamba ulianzishwa Dodoma na viongozi wote wa upinzani na Kundi la Wabunge 201 wa Bunge Maalumu la Katiba walihudhuria, lakini baadhi yao walipenyezewa ‘kitu kidogo’ wakaondoka hivyo kubaki vyama vinne vya siasa.
Udini, ukabila wamkera
Mbowe alionyesha kusikitishwa na kauli alizodai kutolewa na viongozi wa CCM, kumnadi mgombea wao kwa ukabila na kuwataka wananchi kuwakataa wanaotumia mbinu hizo kwani hali hiyo inaweza kusababisha machafuko.
“Nafurahishwa sana na kauli zinazotolewa na viongozi wa CCM, tunampata kiongozi kwa ukabila! Ukawa hatutamchagua mgombea wetu kwa misingi ya ukabila wala udini, huo ni upumbavu,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Msikubali kurudisha ukabila wala udini, hapa uwanjani tupo makabila mengi, Wasukuma mpo! Wahaya, Wachaga, (Ezekiel) Wenje (Mbunge wa Nyamagana) ni Mjaluo yupo hapa.”
Alisema Watanzania wanataka mabadiliko na kwamba hali hiyo imeshuhudiwa wakati wa uandikishaji wa daftari la wapigakura.
Aonya wizi wa kura
Mbowe alisema hawatakuwa na tatizo iwapo ushindi utapatikana kwa njia za haki, lakini hawatakuwa na suluhu iwapo utatumika wizi wa kura kumuingiza mgombea madarakani.
“Hatutapiga magoti na kuomba, kama ushindi utapatikana kwa njia halali hatuna tatizo, lakini tukiona mambo yanakwenda ndivyo sivyo tunasema polisi mtatusamehe, mabomu hayatatosha,” alisema Mbowe.
Lembeli, Bulaya waombewa msamaha
Mbowe alisema Chadema kina maadili yake na kwamba Lembeli na Bulaya waliokuwa CCM wametenda mengi lakini anawaombea msamaha.
“Naomba muwasamehe. Wangapi wanasema tuwasamehe?” alihoji Mbowe huku akiitikiwa kwa sauti, “Woteee”.
Alisema viongozi hao ni miongoni mwa wengi wanaokaribia kutimka CCM na kuwapongeza kwa ujasiri wao makini walioonyesha.
Aahidi kutaifisha viwanja vya CCM
Baada ya kueleza jinsi alivyompigia simu bila mafanikio Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo kuomba kutumia Uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya mkutano huo, Mbowe alisema Serikali ya Ukawa ikiingia madarakani itahakikisha viwanja vyote vilivyojengwa na wananchi vinavyohodhiwa na CCM vinarejeshwa kwenye halmashauri.
“Chadema kwa kushirikiana na Ukawa, viwanja vyote vilivyojengwa na wananchi vitarejeshwa kwenye halmashauri ili vitumiwe na wananchi wote,” alisema baada ya baadhi ya wanawake kuzidiwa na kuanguka kutokana na wingi wa watu na ufinyu wa uwanja wa Magomeni.
Wagombea kulishwa yamini
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa aliwata wagombea ubunge waliopitishwa ambao wana mawazo ya kuuza nafasi zao kwa CCM kujiengua mapema kabla chama hakijawachukulia hatua.
Pia, Dk Slaa alisema chama hicho kitatoa fomu maalumu ambazo zitasainiwa na wagombea ubunge mahakamani ili kiweze kuwachukulia hatua za kinidhamu watakaokwenda kinyume na taratibu za chama hicho.
“Majimbo 157 yamekamilisha leo (jana), sisi Chadema hakuna jimbo ambalo mgombea atapita bila kupingwa kama wanavyofikiri CCM,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Tutatoa fomu za uteuzi ambazo wote waliopitishwa kugombea ubunge watasainishwa mahakamani, naomba niseme atakayeuza jimbo atashughulikiwa, kama mtu anataka kujitoa ajitoe mapema.”
Dk Slaa alisema miaka 10 iliyopita wananchi waliahidiwa maisha bora kwa kila Mtanzania, lakini yamegeuka na kuwa kinyume, sasa ni maisha magumu kwa kila Mtanzania.
“Waswahili wanasema ukiumwa na nyoka hata jani likikugusa unakimbia, miaka 10 mliahidiwa maisha bora kwa kila Mtanzania, leo ni maisha magumu kwa kila Mtanzania. Cha kwanza tunachokisimamia Chadema ni kurudisha nchi kwa wananchi, CCM wamepoka madaraka ya wananchi na kuyaweka mikononi mwa wachache, tunawaambia mwisho wao ni Oktoba,” alisema Dk Slaa.
Lembeli afunguka
Akizungumza kwenye mkutano huo, Lembeli alisema: “Nakumbuka tarehe 16 nilisali nikiwa kijijini kwetu na mama yangu mzazi, nikamwomba Mungu anitoe nchi ya laana anipeleke nchi ya matumaini.
Tarehe 17 nikafanya uamuzi, sasa nipo uwanjani, naomba niwaambie sijaja Mwanza hivihivi nimekamilika, nilipotoka nimeaga.”
Lembeli aliongeza: “Nimezoea kusema msemo wangu huu, hebu kunja ngumi... koroga... peoples,” umati wa watu uliitikia “Power”.
Kabla hajahutubia, Lembeli alibisha hodi Mwanza kwa kusema: “Hodi…hodi, aliitikiwa kwa sauti na umati uliohudhuria: “Karibu baba, karibu.”
Bulaya ampa salamu Wasira
Akihutubia baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama, Buyala alianza kwa kuwauliza wananchi: “Nikamtoe? Nauliza, nikamtoe? Nikamtoe nani?” wananchi walijibu kwa sauti kubwa: “Wasira... kamtoe Wasira.”
Bulaya alisema ni bora kama Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Stephen Wasira anamsikia akaondoka kama alivyomshauri Makongoro Nyerere.
“Makongoro Nyerere alisema, awamu ya kwanza upo, awamu ya pili upo, ya tatu upo ya nne upo ya tano mwisho wake umefika sasa,” alisema Bulaya.
Alisema kwa Mkoa wa Mara yupo mwenyekiti wake, Vicent Nyerere ambaye atafanya naye kazi kwa karibu na kwamba yeye na wenzake wa Chadema ni muziki mnene na jeshi kubwa.
Lissu na kabila la CCM
Akihutubia kwenye mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliwalinganisha, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Andrew Chenge na Spika Anne Makinda kwamba hawana tofauti na mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli, kwa sababu wote ni kabila moja la CCM.
“Nimefanya mikutano mingi, kila mahala nilipokwenda nilikuwa naambiwa Dk Magufuli kabila lake ni Msukuma, wengine Msubi na wapo waliosema Mzinza, mimi naomba niwaambie kwamba kabila moja la CCM ndilo la Dk Magufuli,” alisema Lissu.
Alisema Dk Magufuli ndiye aliyeuza nyumba za Serikali nchi nzima, kauli ambayo ilitiliwa mkazo na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari ambaye alisema watumishi wa umma wanaishi kwenye nyumba za vichochoroni kutokana na Dk Magufuli kuuza nyumba za Serikali.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Chadema, Arcado Ntagazwa ambaye aliwahi kuwa waziri na naibu waziri kwa miaka 15 alisema: “Safari hii kwa Chadema na washirika wao wa Ukawa ni moja kwa moja Ikulu.
Goli la mkono laibuka
Ntagazwa alisema: “Mambo ya kusema goli la mkono, watambue kwamba Oktoba ndiyo mwisho wa ufisadi,”
Kauli hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye alisema mwaka huu goli la mkono litawageukia wao... “Wakijifanya wao ni watoto wa kihuni makamanda wa Chadema ni wahuni zaidi yao.”
Kuhusu kucheza rafu, Mwalimu alisema wanaotarajia kucheza rafu kwenye uchaguzi mkuu ni wazi kwamba wameshindwa kucheza uwanjani.
“CCM kutangaza kushinda hata kwa goli la mkono ni wazi kwamba wameshindwa kucheza uwanjani sasa sisi tutawafuata hukohuko nje ya uwanja na tutawabana,” alisema Mwalimu.
Wenje, Kiwia watamba
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje na Highness Kiwia, walisema kwa sasa wapo likizo ya miezi miwili na wanatarajia kuapishwa tena kuwa wabunge baada ya uchaguzi.
Kiwia alisema: “Mimi ndiye rais wa Jamhuri ya watu wa Ilemela, sina shaka tumemaliza kura za maoni sasa nasubiri tena kuwa Mbunge wa Ilemela.”
Akihutubia, Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini, alisema kazi inaendelea na kinachofanyika sasa ni kuhakikisha CCM inaondoka madarakani Oktoba.
Leo viongozi hao wa Chadema watakuwa na mkutano mwingine mjini Mbeya na baadaye Arusha na Jumatatu ni Dar es Salaam.
Imeandikwa na Midraji Ibrahim, Aidan Mhando na Fidelis Butahe.
            Habari kutoka: Mwananchi

CHADEMA UBUNGE LUDEWA WAENDELEA KUMWAGA SELA ILI KUMPATA MGOMBEA MMOJA

                                 Wakili Paulo Kalomo mgombea ubunge jimbo la Ludewa


Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilayani Ludewa kimeendeleana na mtifuano mkali katika kumsaka mgombea mmoja wa ubunge wilayani hapa ambapo kila mgombea amekuwa akipita huku na kule kusaka kura kwa wajumbe wa Chama hicho huku baadhi yao wakituhumiana kutumia pesa zaidi.
Akiongea na waandishi wa habari jioni ya leo Wakili Paulo Kalomo ambaye ni miongoni mwa wagombea wa nafasi hiyo akitokea mwambao wa ziwa Nyasa alisema kuwa mpaka sasa kuna wagombea wanne hivyo yeye amekuwa na mvuto zaidi kwa wajumbe hali ambayo inawafanya wagombea wenzake kukata tamaa na kuwarubuni wajumbe.
Wakili Kalomo alisema kuwa akifanikiwa kuchukua nafasi hiyo atakibadirisha chama cha demokrasia na maendeleo wilayani Ludewa kwa kujijenga kuanzia vijijini hadi ngazi ya wilaya hivyo amewataka wajumbe wa chama hicho kutorubuniwa na baadhi ya wagombea katika kura za maoni zinazotarajiwa kupigwa leo tarehe 23/7/2015 katika makao makuu ya wilaya kwani yeye anamipango endelevu kwa wilaya ya Ludewa.

Wednesday, 22 July 2015

ZAIDI YA WAZEE 300 WAMCHANGIA NA KUMCHUKULIA FOMU YA UBUNGE FILIKUNJOMBE JIMBO LA LUDEWA. Wasema wameridhika na utendaji wake.

 Baadhi ya wazee wa wilaya ya Ludewa wakimpa baraka za mwisho za kuanza kugombea kwa awamu ya pili Mh.Deo Filikunjombe
Filikunjombe akisikiliza nasaha za Wazee

 msafara wa kumsikindikiza kutangaza nia ya kugombea ubunge Deo Filikunjombe ukiingia viwanja vya mpira wa miguu Ludewa mjini
Filikunjombe akiwasalimia mamia ya wanachama wa ccm wilayani Ludewa ambao walikuja kumuunga mkono

wasanii wa kikundi cha IVA YOUTH GROUP ambacho ni kikundi cha uhamasishaji wilayani hapa wakifanya yaliyo yao
                                       mamia ya washabiki wa ccm wakimraki Filikunjombe


Filikunjombe akiongea na wananchi wa wilaya ya Ludewa kata ya Ludewa mjini wakati akitangaza nia ya kugombea ubunge

                   msanii wa IVA youth Group Seleman Chikuti akionesha umahiri wake katika sanaa
 Seleman Chikuti toka kundi la IVA youth group linalopatikana Ludewa mjini akifanya vitu vyake wakati Deo Filikunjombe akitangaza rasmi nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Ludewa







Zaidi ya Wazee 300 wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wamefanya

maandamano ya kumuunga mkono mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo

Filikunjombe na kumchukulia fomu ya kugombea nafasi ya ubunge wa

jimbo hilo kwa awamu ya pili ili aweze kuliongoza tena kwa kauli ya

kuwa wameridhishwa na utendaji wake ambao hauna mashaka.


Akizungumza kwa niamba ya wazee wenzake mzee Laurent Mtweve alisema

kuwa jimbo la Ludewa limekuwa na umaarufu mkubwa wa kubadili

wabunge kila baada ya miaka mitano kutokana na utendaji

usioridhisha lakini safari hii hakuna haja tena ya kufanya hivyo

kutokana na mafanikio makubwa yaliyofanyika katika kipindi cha

Filikunjombe.


Mzee Mtweve alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2010 HADI 2015

wilaya ya Ludewa imepata mabadiriko makubwa katika kila sekta kwani

wakati mwingine Filikunjombe hakuweza kuisubiri bajeti ya Serikali

alilazimika kutoa fedha za posho yake ili kufanikisha na kutatua

matatizo yanayowakabiri wananchi wake.


Naye Bi.Mariam Nyandoa alisema kuwa katika moja ya kazi ambayo

Filikunjombe anapaswa kuendelea na uongozi ni ile ya kuhakikisha

kila hospitari,zahanati,dispensari kunakuwa na watumishi pamoja na

vitanda vya kujifungulia hali ambayo imekuwa ni kilio cha wanawake

wilayami Ludewa kwa muda mrefu.


Bi.Mariam alisema kuwa kwa sasa hakuna shida tena kama ilivyokuwa

awali kwani unapokwenda hospitari unauhakika wa kupata huduma nzuri

hivyo wazee wote wakaona wachange fedha za kumchukulia fomu ya

kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Ludewa na pia wanaandaa

sherehe ya kumpongeza kwa uongozi wake mzuri ambao ameuonesha.


"Sisi kama wazee katufanyia mengi katika kipindi cha uongozi wake

na yamekuwa ya mafanikio kwa wilaya ya Ludewa kumpata mbunge kijana

na ambaye anatumika akitumwa hivyo tunampango wa kumfanyia sherehe

licha ya kuwa tumemchukulia fomu hivyo hatuna mpango wa kuwa na

mbunge mwingine zaidi yake",alisema Bi.Nyandoa.


Akiongea na umati wa wananchi wa wilaya ya Ludewa katika viwanja

vya michezo Ludewa Mjini wakati akitangaza nia ya kungombea nafasi

ya ubunge Mh.Deo Filikunjombe alisema kuwa mafanikio yote

yaliyopatikana sio juhudi zake binafsi bali ni ushirikiano

alioupata toka kwa wananchi wa jimbo lake.


Filikunjombe alisema kuwa katika kipindi cha uongozi wake ni kweli

kumekuwa na mafanikio makubwa lakini wananchi ndio waliokuwa

wakimsukuma kufanya hayo na wakati mwingine alikuwa mkali Bungeni

kutokana na halia halisi ya ugumu wa maisha ya wananchi wa wilaya

ya Ludewa.


Alisema kuwa anamshukuru rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa

kuitendea haki wilaya ya Ludewa kwani katika kipindi cha uongozi wa

ke Ludewa imekuwa ikisikilizwa kupitia yeye hali ambayo

imeharakisha maendeleo wilayani Ludewa.


Anasema katika ubunge wake wa miaka mitano Ludewa imeweza kupata

kipande cha lami na hatimaye barabara za mitaa ya Ludewa mjini

zimeweza kung'ara kwa lami ikiwa ni juhudi zake kwani kabla ya

kuingia katika ubunge wilaya ya Ludewa haikuwa hata na kipande

kimoja cha lami.


Alisema kuwa licha ya Lami lakini barabara za vijijini vimefunguka

mfano barabara ya Lupingu ambapo kwa sasa kuna gari za abiria

zinafika huko wakati awali haikuwezekana pia barabara ya Mawengi

makonde ambako kwa sasa samaki wabichi wa ziwa nyasa wanafika

mapema Ludewa mjini.


Pia katika nishati ya umeme alivikuta vijiji vitatu vta

Mavanga,Mawengi na Ludewa mjini ndivyo vilikuwa na umeme lakini kwa

sasa kunamiradi ya umeme katika vijiji 67 ikiwa wilaya ya Ludewa

inajumla ya vijiji 77 hivyo anatangaza nia ya kugombea tena nafasi

hiyo ili aweze kukamilisha vijiji vilivyobaki.


Filikunjombe alibainisha kuwa wilaya ya Ludewa inatakiwa

kubadirishwa haraka na haya machache ambayo wananchi wanayaona kama

ni mabadiriko makubwa kwake ni machache sana kwani Ludewa imekuwa

nyuma kimaendeleo kwa miaka mingi hivyo katika mipango yake ya

ujenzi wa lami barabara kuu tayari Serikali imeshatoa fedha ya

kujenga barabara hiyo na awamu ya kwanza itajengo kilomita 50.


Alisema ujenzi wa barabara hiyo unaanza mapema mwezi ujao ambapo

Dkt.John Pombe Magufuli atakuja kabla ya kuanza ujenzi ili kujionea

mafanikio aliyoyafanya kwa wananchi wa wilaya ya Ludewa katika

sekta ya miundombinu na baadaye atakuja Rais Dkt.Kikwete kuweka

jiwe la msingi la ujenzi wa viwanda vya chuma cha Liganga na makaa

ya mawe Nchuchuma.


Aliwataka wananchi wa wilaya ya Ludewa kumuunga mkono mgombea wa

nafasi ya urais kupitia chama cha mapinduzi Dkt.Magufuli kwani ni

kiongozi makini na anayeipenda wilaya ya Ludewa kwa ni bila yeye

hata barabara za lami wilayani hapa tusingezipata hivyo wananchi wa

wilaya ya Ludewa wanahaki ya kujivunia kwa kuteuliwa Dkt Magufuli.


Filikunjombe alisema kuwa hivi sasa Serikali imepitisha bajeti ya

ujenzi wa daraja la mto ruhuhu ili kuunganisha wialaya ya Ludewa na

ile ya Nyasa hivyo wananchi wanatakiwa kujiandaa na fulsa ya

kibiashara watakayoweza kufanya na mkoa jirani wa Ruvuma.


Mwisho. 

Habari na: http://habariludewa.blogspot.com

Wabunge Chadema waangukia katika kura za maoni


Wanachama wa Chadema wilaya ya Mbeya Vijijini
Wanachama wa Chadema wilaya ya Mbeya Vijijini wakitoka nje ya ukumbi baada ya msimamizi wa uchaguzi wa kura za maoni za kumpata mgombea ubunge jimbo la Mbeya Vijijni kutokomea kusikojulikana  wakati wa kuhesabu kura jana na kusababisha uchaguzi huo kuvunjika. Picha na Godfrey Kahango 
By Waandishi Wetu, Mwananchi
Dar/mikoani. Kura za maoni ndani ya Chadema zimeanza kuwa chungu kwa baadhi ya wabunge. Mbunge wa Mbulu, Mustapha Akoonay na mwingine wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Kinondoni) jana waliangukia pua, huku mwenzao wa Karatu, Mchungaji Israel Natse akitangaza kuachana na ubunge na kurejea katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
“Jumatano (leo), nitawaaga rasmi wananchi wangu, binafsi niliombwa na Dk (Willibrod) Slaa kugombea jimbo hili kwa miaka mitano,” alisema.
Lyimo alianguka baada ya kupata kura 32 nyuma ya Mustafa Muro aliyepata kura 47. Wengine ni Rose Moshi (8), Agrey Mkwama (6), Gemeral Kaduma (4) na Francis Nyerere (0). Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa alisema tayari uchaguzi umefanyika katika majimbo matano.
Alisema Mbulu Mjini, kulikuwa na wagombea wawili, Akoonay alipata kura 108 dhidi ya 132 alizopata Diwani wa Mbulu, Michael Sulle.
Golugwa alisema, Joseph Selasini ametetea nafasi yake katika Jimbo la Rombo baada ya kupata kura 313 akiwaacha mbali wapinzani wake Ben Sanane aliyepata kura 26 na wengine kura mojamoja.
Babati Mjini, Mbunge wa Viti Maalumu, Paulina Gekur ameibuka kidedea kwa kura 88 akiwatupa nje wapinzani wake, akiwamo mkuu wa wilaya wa zamani, Gabriel Kimolo na wenzake.
Mbulu Vijijini, Aman Gaseri alishinda kwa kura 76 huku Michael Aweda akipata 75.
Jimbo la Same Magharibi: Jonas Kadeghe alishinda kwa kura 68 akifuatiwa na Christ Mbanjo aliyepata kura 49 na Gervas Mgonja kura 30.
Muleba Kaskazini: Najim Kasange alipata kura 247 na kumshinda mwandishi wa habari mkongwe, Ansbert Ngurumo aliyepata kura 55. Mgombea mwingine, Christina Mwainunu alijitoa.
Jimbo la Ukonga, Nickson Tugara alishinda kwa kura 59 hivyo kuwaacha kwa mbali wagombea wenzake 14. Alifuatiwa na Waitara Mwikwabe aliyepata kura 49, Elly Dallas (15), Deogratias Munishi (8), Lucas Otieno (6), Asia Msangi na Deogratias Mramba waliopata kura tano kila mmoja na Gasto Makwetta (1). Wengine saba hawakuambulia kura hata moja.
Butiama: Yusuf Kazi aliibuka kifua mbele baada ya kujikusanyia kura 202 na kuwapiku Adam Taya (39) na Issa Yusuf (31), Daniel Obeiya (3), Annicent Marwa (2) na Lucas Ossoo na Marto Yohana waliopata kura moja kila mmoja.           
  Nyamagana: Wenje aliibuka kidedea kwa kupata kura 194 na Patrick Masagati (32).
Msalala: Paulo Ndundi alishinda kwa kura 113 akiwashinda Peter Machanga (49) na Ezekiel Kazimoto (48). Wengine ni Emmanuel Mbise (43), Francis Makune (15), Vincent Manoni Mhagwa (10) na Richard Mabilika aliyepata kura moja na Stephen Bundala (0).
Sumbawanga: Shadrack Malila aliibuka na ushindi wa kura 277 dhidi ya Kassian Kaegele (28), Musa Ndile (9) na Matokeo Lyimo (1), Eliud Mwasenga na James Kusula (0).
Nkasi Kusini: Alfred Sotoka aliongoza kwa kupata kura 70 akifuatiwa na Kaminga Hyporito (39), Emmanuel Sungura (9), Edson Ndasi (4) na Joseph Kitakwa (2).
Nkasi Kaskazini: Keissy Sudi alishinda kwa kura 158 na kufuatiwa na Triphone Simba (70) na Stanley Khamsini (5).
Kwela: Daniel Ngogo aliwabwaga wenzake kwa kura 151 akifuatiwa na James Mwamlyela (117), Ameri Nkulu (27), Alstidi Maufi (13) na Michael Moka (4).
Mlalo: Kelvin Shemboko alipata kura 56 akifuatiwa na Lewis Kopwe (31), Jumanne Pazia (15) na Mkazeni Mkazeni (0).
Mabadiliko ya ratiba
Wakati kukiwa na sintofahamu na wanachama wanaojiunga na Chadema huku kipindi cha kurejesha kikiwa kimekwisha, chama hicho kimetangaza mabadiliko kwenye ratiba ya kurudisha fomu hasa katika majimbo mapya yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Julai 12.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema jana: “Fomu za kugombea kwenye majimbo hayo zitaendelea kutolewa na hata kura ya maoni watapiga tofauti na majimbo yaliyokuwapo.”
Alisema hata katika majimbo mengine, Sikukuu ya Eid el Fitr iliingilia ratiba iliyopangwa awali na kwamba uongozi wa chama umeona kuwa ipo haja ya kuongeza siku ili kutenda haki kwa wale waliokosa kulipia fomu benki kutokana na sherehe hizo.
“Kinachotakiwa sasa ni katibu wa wilaya kutuma mapendekezo ya kuongeza siku atakazoona zitafaa kwa zoezi hilo na makao makuu itaidhinisha hilo,” aliongeza.
Msimamizi ‘aingia mitini’
Uchaguzi wa mgombea ubunge Mbeya Vijijini ulikwama baada ya msimamizi wa kura za maoni wa Chadema, Christopher Mwamsiku kutokomea kusikojulikana katika hatua za mwisho.
Kitendo hicho kiliwafanya wajumbe wa Kamati ya Siasa Mbeya Vijijini na mawakala kubaki njiapanda wasijue cha kufanya huku wengine wakidai kuwa hizo ni njama za kutaka kumbeba mmoja wa wagombea.
Mwenyekiti wa Chadema wilayani hapo, Jackson Mwasenga alishindwa kutoa maelezo ya tukio hilo huku akimtaka katibu wake kuzungumza.
Katibu huyo, James Mpalaza alisema: “Hata sisi hapa kama unavyotuona tumeduwaa hatujui ni kwa nini ameondoka.”
Alipotafutwa kwa simu, Mwamsiku alijibu kwa kifupi: “Sijakimbia, nimeondoka kwa utaratibu mzuri tu… lakini siwezi kukwambia ni kwa nini kamuulize Mwasenga anayo majibu yote niache nipumzike.”
Dalili za kuvurugika kwa uchaguzi huo zilianza wakati wa kuhesabu kura baada ya Mwenyekiti wa Bavicha, Mbeya Vijijini kuingia ndani ya chumba hicho akidaiwa hahusiki jambo lililozua mzozo mkubwa uliodumu kwa takriban dakika tano hadi alipotoka.
Wengine wajitokeza Chadema
Tabora Mjini: Peter Mkufya, Nhombar Imajamasallah, Elifuraha Kisangi, Said Mwakasekela na Raymond Maganga.
Kaliua: Anthony Mwakammoja, Godluck Jilinga, Prosper Guga, Peter Msazya na Wilson Lukobe.
Ulyankulu:  Dk Deus Kitapondya.
Igalula: Mustapha Kado na James Kabepele.
Tabora Kaskazini: Daud Nteminyanda.
Igunga: Joseph Kashindye, Ngasa Mbojenamba na Gw’igulu Darushi.
Manonga: Ally Halfan Nguzo, Athanas Shija Michael na Simon Seleli.
Nzega Vijijini: Albino Mayani Simbila na Nicholaus Zakaria.
Nzega Mjini: Gisberth Kabamba, Daniel Simba, Boniface Masasi, Charles Mabula, Monica Nsaro, Ally Ndee na Mary Atonga.
Bukene: Alex Mpugi, Lumola Kahumbi, Elias Machibya, Dickson Kagembe na Emmanuel Ntobi.
Rorya): Mtatiro Sanya, Evangel Dea, Kevin Makooko, Matiko Seruka, Emmanuel Werema, Ezekiel Kachare, Steven Owawa, Opiyo Nalo, Herman Odemba,  Thomas Risa na  Ochora Ndira.
Tarime Vijijini: John Heche, Peter Busene, Moses Yomami, Prosper Nyamuhanga, Johanes Manko na Fabiani Mwita.
Tarime Mjini:  Ester Matiko, Lucas Ngoto, Christopher Chomete, Charles Werema na Martinus Joseph.
Waliojitokeza CCM
Arumeru Mashariki: Elirehema Kaaya, Jackson Ezekiel, John Sakaya. Angela Palangyo, William Sarakikya, Dk Daniel Pallangyo na Siyoi Sumari.
Longido: Philip Kitesho, Dk Stivin Kiluswa, Lee Mamaseta, Daniel Marari, Lesioni Mollel, Joseph Kulunju, Lemayani Logoliye na Emmanuel Sirikwa.
Monduli: Sakata Babuti, Loota Sanare, Loliayu Mkoosi, Namelock Sokoine, Mbayani Kayai na Amani Turongei.
Arumeru Magharibi: Loy Thomas Sabaya, Daudi Mollel, Elisa Mollel, Osilili Losai, Henri Majola, Lekoko Piniel na Lomoni Mollel.
Ngorongoro: Eliaman Laltaika, Elias Ngolisa, Joseph Parsambei, Patrick Kasongo, William Ole Nasha na Saning’o Telele.
Karatu: John Dodo, Dk Willbrod Rorri, Joshua Mbwambo na Rajabu Malewa.
Arusha Mjini: Mustapha Panju, Justin Nyari, Philemon Mollel, Victa Njau, Thomas Munisi, Hamis Migire, Admund Ngemera, Moses Mwizarubi, Ruben Mwikeni, Endrew Lymo, Salehe Kiluvia, Lukiza Makubo, Mohammed Omar na Emmanuel ole Ngoto.
Mkalama: Mgana Msindai, Profesa Shaban Mbogho, Nakey Sule, Orgenes Joseph Mbasha na Allan Kiula, Emmanuel Mkumbo, Dk Kissui Kissui, William Makali, Kyuza Kitundu, Dk Charels Mgana, Salaome Mwambu, Francis Mtinga, Dk George Mkoma na Lameck Itungi.
Manyoni Magharibi: John Lwanji, Eliphas Lwanji, Jamal Kuwingwa, Jane Likuda, Mohammed Makwaya, Yahaya Masare, Athumani Masasi, Yohana Msita, Moshi Mmanywa, Adimini Msokwa, Dk Mwanga Mkayagwa, Rashidi Saidi na Francis Shaban.
Manyoni Mashariki: Dk Pius Chaya, Joseph Chitinka, Alex Manonga, Jumanne Mtemi, Daniel Mtuka, Harold Huzi na Gaitani Romwad.
Singida Mashariki: Jonathan Njau, Hamisi Maulid, Mdimi Hongoa, Jocab Kituu, Emmanuel Hume na Martin Lissu.
Ikungi Magharibi: Dinawi Gabaraiel, Hamisi Lissu, Wilson Khambaku, Dk Hamisi Mahuna, Dk Grace Puja, Yona Makala, Elibariki Kingu na Hamisi Ngila.
Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba, David Jairo, Juma Kilimba na Amon Gyuda.
Singida Mjini: Hassan Mazala, Amani Rai, Mussa Sima, Leah Samike, Philemon Kiemi na Juma Kidabu.
Singida Kaskazini: Lazaro Nyalandu, Amosi Makiya, Justin Monko, Michael Mpombo, Sabasaba Manase, Yahana Sinton, Mugwe na Aron Mgogho.
Imeandikwa na Robert Kakwesi, Dinna Maningo, Mussa Juma, Filbert Rweyemamu, Gaspar Andrew na Mussa Juma, Joseph Lyimo, Mussa Mwangoka, Godfrey Kahango na Julius Mathias.
                                    Habari kutoka:http://www.mwananchi.co.tz

Tuesday, 21 July 2015

Wabunge wa Chadema wamkaribisha Lowassa

Wafuasi wa Chadema wakiwa katika moja ya
Wafuasi wa Chadema wakiwa katika moja ya mikutano ya hadhara ya chama hicho. Picha na Maktaba 
By Florence Majani, Mwananchi
Dar es Salaam. Baadhi ya wabunge wa Chadema wamezungumzia taarifa zinazosambaa zikieleza kuwapo mkakati wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia katika chama hicho, wengi wao wakimkaribisha.
Wakati wabunge hao wakikubali kumpokea, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa amesema wananchi wasubiri mambo yatakapokuwa tayari badala ya kutegemea mitandao ya kijamii.
“Nitazungumza pale mambo yatakapokuwa sawa, siwezi kuzungumza sasa, subirini… sasa hivi mambo mengi yanazungumzwa kwenye mitandao,” alisema Dk Slaa ambaye pia anatajwa kuwa mgombea wa chama hicho ndani ya Ukawa.
Msemaji wa Lowassa, Aboubakary Liongo alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa mpango huo alisema hawezi kulizungumzia hilo kwa kuwa ni suala la mtu binafsi. Hata hivyo, jitihada za kumpata Lowassa jana hazikufanikiwa kwani simu yake iliita pasi na kupokewa.
Hivi karibuni, idadi kubwa ya madiwani wa CCM walirudisha kadi zao na kujiunga na Chadema wakisema sababu ni kutoridhishwa na kukatwa kwa jina Lowassa kati ya wagombea urais wa CCM.
Kadhalika, mtandao wa kijamii uliokuwa ukimuunga mkono mbunge huyo wa Monduli unajulikana kwa jina la 4U Movement ulitangaza kuhamia Chadema hali inayoashiria kuwa kuna dalili ya Lowassa pia kujiunga nao.
Wakiandika katika akaunti ya Twitter ya 4U Movement, wafuasi hao walisema: “Ukimya ni hekima na ukimya ni busara. Ukimya wa Edward Lowassa ni kutafakari Safari ya Matumaini... Tuungane kuyapata mabadiliko nje CCM.”
Chadema ni kanisa la wokovu
Akizungumzia taarifa hizo, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alikifananisha chama hicho na kanisa ambalo kwa kawaida halikatai mtu, bali linawapokea wenye dhambi na kuwaongoza kufanya toba.
“Chadema ni kama kanisa, hakataliwi mtu, tunahubiri habari njema ya wokovu, ukija hapa unatubu unaendelea kufanya kazi,” alisema.
Kuhusu viongozi wa CCM kuhamia Chadema, Msigwa alisema inawezekana kasi hiyo inachagizwa na Lowassa kukosa nafasi aliyoitaka ndani ya chama hicho.
“Unapokuwa mwanasiasa unakuwa na wafuasi, inawezekana wengine wanaohamia Chadema ni watu wake ambao wameona mtu wao amekosa nafasi aliyoitaka ndiyo maana wanakihama chama,” alisema.
Msigwa alisema Chadema ilikuwa inakusanya wanachama wapya kwa muda mrefu hata kabla ya vuguvugu la Lowassa na chama chake kuibuka na ushindi na wanaohamia wanafanya hivyo kwa sababu wanakipenda chama na wameichoka CCM.
Huenda akatimiza safari ya matumaini
Akizungumzia ujio wa Lowassa kwenye chama hicho, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema iwapo Lowassa atahamia Chadema anakaribishwa na huenda akaitimiza safari yake ya matumaini.
“Namkaribisha Lowassa Chadema, huenda safari yake ya matumaini ikaishia huku, akawa mwanachama au hata kiongozi,” alisema.
Alisema hakuna shaka kuwa mbunge huyo wa Monduli ana nguvu ndani ya CCM ndiyo maana viongozi wengi wa chama hicho wanakihama wakati huu.
“Hiyo ilijionyesha kuanzia kwenye Kamati Kuu ya CCM, Halmashauri Kuu, Lowasa amekamata wajumbe kwa asilimia 80 na hiyo ni ishara kuwa ameishika CCM,” alisema.
Lema aliongeza kuwa wanaoihama CCM hawaihami kwa bahati mbaya, bali wameona mtu wao waliyemtarajia ameondoka.
“Ni wengi wanaohamia Chadema, kwa sasa kadi zimetuishia na hiyo ni ishara kuwa CCM inakufa, ripoti za mikoa yote tunazo,” alisema.
Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya alisema  wanaoihama CCM kwa sasa wamegundua kuwa chama pekee kinachoweza kutetea wananchi ni Chadema.
“Sisi tunawakaribisha kwa mikono miwili, waje tuchape kazi, ilimradi wanafuata kanuni na taratibu za chama, basi.  Wamejionea wenyewe kuwa CCM hakuna chochote,” alisema.
 Alisema CCM waliamua kupitisha katiba bila kuwapo kwa Ukawa, lakini sasa wameona kuwa walichokifanya ni makosa na wameanza kurudi Chadema ambako wanaamini kuna demokrasia ya kweli.
Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Paresso alisema: “Tunamkaribisha kwa mikono miwili. Tumekinyooshea CCM vidole kwa muda mrefu kuwa kuna rushwa na makundi na hilo linajidhihirisha sasa. Lakini wale wote wanaokuja Chadema, tunawakaribisha ili mradi wafuate kanuni na taratibu zetu.”
Paresso alisema hana tathmini ya kina kuhusu wafuasi wa Lowassa wanaoihama CCM, bali wanaokihama chama hicho wameona kina matatizo.
Atakiwa akidhi vigezo na masharti
Licha ya kuonyesha kumkaribisha, katika chama hicho, baadhi ya wabunge walimtaka Lowassa afuate kanuni ili awe mwanachama mwenye sifa.
Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde alisema anakaribishwa lakini hana budi kufuata sheria na kanuni za chama... “Anatakiwa afuate taratibu za chama, milango ipo huru, lakini afuate kanuni… asije akafikiri ataleta taratibu zake hapa, sitakubali.”
Silinde alisema wanaohamia Chadema hawajapendezwa na mwenendo mzima wa uteuzi wa mgombea wa urais na hivyo wameifuata demokrasia ya kweli ndani ya chama hicho.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hilo lakini alisema endapo atajiunga, chama hicho kitampokea kulingana na vigezo na taratibu.
“Akihamia Chadema nitatoa maoni yangu lakini ninachoweza kusema ni kuwa kila mtu ana haki ya kwenda chama chochote ili mradi ana tija,” alisema.
Mdee alisema wanaCCM wanaohamia Chadema wamesoma alama za nyakati na kuona kuwa CCM haiendani na ahadi zake.
Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo alisema, Lowassa ni binadamu wa kawaida kwa hiyo kuhamia kwake Chadema si kitu cha ajabu ilimradi afuate kanuni... “Cha muhimu afuate masharti ya chama, kanuni na  taratibu, kama watu wanahama vyama vingine yeye ni nani asihame CCM?”
Lyimo alisema wanaCCM wengine wanakaribishwa kujiunga kwa sababu kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.
Mbunge wa Viti Maalumu, Pauline Gekul, aliwataka wana CCM na Lowasa kuhamia zaidi  Chadema ili kuunganisha nguvu na kuichukua nchi.
 “Mfikishie salamu Lowassa mwambie karibu kwenye jeshi la ukombozi,” alisema.
Katibu wa CCM amuonya
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma, Katibu wa CCM mkoa huo, Albert Mgumba alisema ingawa kuhama chama ni hiari ya mtu, Lowassa hapaswi kuchukua uamuzi wa hasira kiasi hicho badala yake awe mstari wa mbele kuhamasisha umoja ndani ya chama.
Alimtaka kutothubutu kuihama CCM na endapo afanya uamuzi huo atambue kuwa hawezi kukisababishia pengo lolote zaidi ya kujipunguzia hadhi yake ya kisiasa.
“Mgombea tuliyempata sasa ni makini kuliko, anapendwa, utendaji wake unajulikana kila mahali,” alisema Mgumba.
Mgumba alisisitiza kuwa badala ya Lowassa kuwa na mawazo ya kuihama CCM, anapaswa kutuliza fikra na kuonyesha ukomavu wake kisiasa kwa kuwa mstari wa mbele kuwaonya na kuwatuliza wote waliokuwa wakimuunga mkono ili wabaki kwa utulivu ndani ya chama na si vinginevyo.
“CCM siyo Mgumba, ni taasisi iliyosimama. Lowassa anapaswa kutambua hilo, atulie na awe mstari wa kwanza kuwaonya wanachama wachanga kisiasa, wasiokuwa na uzalendo ndani ya chama kwa kumfikiria mtu badala ya chama na masilahi ya Taifa” alisema Mgumba.
Habari na: http://www.mwananchi.co.tz

Tuesday, 14 July 2015

MAJIMBO MAPYA 26 YA UCHAGUZI BAADA YA KUGAWANYWA


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza majimbo mapya ya uchaguzi katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)

                                                                    Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza majimbo 26 mapya ya uchaguzi ambayo yatakuwa na wagombea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kukata kwa majimbo hayo wamezingatia idadi ya watu pamoja na Jiografia katika majimbo mapya.

Amesema katika upande wa Zanzibar majimbo yamebaki kuwa 50 kama awali hiyo inatokana vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.

Majimbo yaliongezwa ni Handeni Mjini, Nanyamba, Makambako, Butiama, Tarime Mjini, Tunduma, Msimbo, Kavu, Geita Mjini, Mafinga Mjini, Ushetu, Nzega Mjini, Kahama Mjini, Kondoa Mjini, Newala Mjini, Bunda Mjini, Mbulu Mjini, Ndanda, Madaba, Mbinga Mjini, Mbagala, Kibamba,Vwawa,Monongo,Mlimba, Pamoja na Uliambulu.

Jaji Lubuva amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakiingia katika Halmashauri mbili hiyo kuweka mipaka katika maeneo ili mbunge aweze kushiriki katika Halmashauri moja tu.

Amesema baadhi majimbo yamebadilishwa majina na kuendelea kuwepo kwa majimbo hayo kisheria.
You might also like:

Wednesday, 8 July 2015

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR, MAALIM SEIF AITEMBELEA FAMILA YENYE WATOTO SITA WENYE ULEMAVU


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na familia ya Bw. Saleh Juma Saleh (mwenye mtoto), yenye watoto sita wenye ulemavu wa aina tofauti, huko nyumbani kwao Kinyasini Mkarafuuni Wilaya ya Wete. (Picha na OMKR)

                                                                                Na: Hassan Hamad, OMKR

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo ameitembelea na kuifariji familia ya Bw. Saleh Juma Saleh yenye watoto sita wenye ulemavu.

Akizungumza na familia hiyo nyumbani kwao Kinyasini Mkarafuuni Wilaya ya Wete Pemba, katika mfululizo wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, Maalim Seif ameitaka kuwa na subra na upendo kwa watoto hao wakielewa kuwa huo ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Amemuagiza Mkuu Mkuu wa Wilaya ya Wete kukutana na familia hiyo, ili kuandaa mipango itakayoweza kuwasaidia katika kuendesha maisha yao na shughuli zao za kila siku.

Baba mzazi wa watoto hao Bw. Saleh Juma Saleh amesema watoto wake wanashindwa kusoma kutokana na kukosa nyenzo kwa vile wote sita hawawezi kutembea.
Amesema watoto hao wakiwemo wanne wa kike na wawili wa kiume wanasikia vizuri, wanazungumza na wanafahamu wanachoambiwa, ingawaje baadhi ya wakati wanapoteza uelewa kutokana na hali ya ulemavu wao.
Amefahamisha kuwa iwapo watapatiwa nyenzo wataweza kwenda skuli na kusoma kama wenzao wengine, na kuiomba serikali na wasamaria wema kuwapatia misaada inayostahiki, ili nao waweze kwenda skuli.
                                              Habari na: http://rweyunga.blogspot.com/

Tuesday, 7 July 2015

Dawa mpya ya ukimwi yakosolewa

Truvada
Kwa muda mrefu wahudumu wa afya ya masuala ya ngono wamesisitiza matumizi ya mipira ya kondomu kama mbinu bora zaidi dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Lakini tabia moja hatari ya kutumia madawa ya kulevya na wapenzi wa jinsia moja inazidi kuibua wasiwasi.
kumekuwa na njia nyingi za kinga dhidi ya virusi vya ukimwi, lakini kuna dawa moja mpya - Pre-Exposure Prophylaxis (PrEP) - ambayo inaweza kutoa kinga dhidi ya maambukizi ya ukimwi iwapo itatumika kabla ya kushiriki ngono.
Utafiti unaofanywa na daktari Sheena McCormack kutoka chuo kikuu cha London, unasema kwamba unapomeza dawa hiyo, inazuia maambukizi ya ukimwi kwa kuzuia ongezeko la virusi, hii ni baada ya majaribio kufanyiwa kundi moja la wapenzi wa jinsia moja, ambao wamo katika hatari kubwa zaidi ya maambukizi
Shirika la afya duniani limetambua kwamba dawa hiyo ya tembe inaweza kupunguza maambukizi kwa kiwango kikubwa.
Baadhi ya wakosoaji wanasema kuwa dawa ya aina hii inahamasisha watu wengi kushiriki ngono bila kutumia mipira ya kondomu
Hata hivyo matumizi ya dawa hii haizuii maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na kaswende, je, kukubalika kwa matumizi ya dawa hii duniani kunamaanisha ongezeko la magonjwa ya zinaa.
                         Habari na: http://www.bbc.com

Polisi: Msiokuwa na shughuli maalumu msije Dodoma

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ,David Misime. 
Na Rachel Chibwete
Kwa ufupi
Misime alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu wiki hii ambayo inatarajiwa kuwa na ugeni mkubwa wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM ambao amesema kuwa unakadiriwa kuwakusanya watu takribani 10,000.



Dodoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime amewataka wageni wasiokuwa na shughuli muhimu ya kufanya mkoani hapa kutokuja katika kipindi cha juma hili ili kuepusha usumbufu utakaojitokeza.
Misime alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu wiki hii ambayo inatarajiwa kuwa na ugeni mkubwa wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM ambao amesema kuwa unakadiriwa kuwakusanya watu takribani 10,000.
Alisema ili kuepusha usumbufu utakaojitokeza kama vile kukosa mahali pa kulala, ni vyema kama mtu hana shughuli ya muhimu ya kufanya mjini hapa asije mpaka mkutano huo utakapokwisha.
“Kuna wengine wanataka kuja kwa ajili ya ushabiki tu au kuja kushuhudia tukio zima na hata kama hawatakuja haitawaathiri kitu hivyo ni vyema wasije ili kuepusha usumbufu,” alisema Misime.
Alisema Jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi wote watakaofika katika mkutano huo na kuwataka wananchi kutoa taarifa za viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani katika maeneo yao.
Aliwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuhakikisha kuwa vitu vyote vyenye thamani vya wateja wao vinatunzwa vizuri ili kuepusha usumbufu au kupotea kwenye mikono yao.
Ulinzi mkali bungeni
Jana, Polisi waliimarisha ulinzi bungeni kwa kuongeza idadi ya askari na pia kufunga kipande cha barabara kuanzia kwenye mzunguko wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani kupitia eneo la Bunge hadi mwanzo wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Tawi la Dodoma.
Kulikuwa na idadi kubwa ya polisi wa usalama barabarani, utepe mweupe uliofungwa katika barabara hiyo huku kukiwekwa kibao kilichoandikwa kwa maandishi mekundu, “barabara hii imefungwa.”
Alipoulizwa kuhusu hatua hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime (pichani) alisema kufungwa kwa barabara hiyo ni miongoni mwa shughuli za usalama.
                                    Habari na: http://www.mwananchi.co.tz

MAHAKAMA YAWAHUKUMU MRAMBA NA YONA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU JELA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana imewahukumu kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya shilingi milioni 5 kila mmoja aliyekuwa Waziri wa Fedha Basil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona baada ya kuwatia hatiani kwa makosa mawili.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji John Utamwa, Jaji Sam Rumwenyi pamoja na Hakimu Saul Kinemela ambapo mtuhumiwa wa tatu wa kesi hiyo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja amekutwa hana hatia.

Washitakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya MS Alex Stewart ya Uingereza.
                                      Habari na: http://rweyunga.blogspot.com

Saturday, 4 July 2015

Majambazi yachakaza gari la polisi kwa risasi

 
Kwa ufupi
Majambazi hayo pamoja na askari polisi waligeuza mtaa huo kuwa eneo la mapambano baada ya kutupiana risasi kwa zaidi ya dakika 15, huku jambazi moja likiuawa kwa kupigwa risasi na askari waliokuwa kwenye mpambano huo.
SHARE THIS STORY
0
Share


Mwanza. Ilikuwa kama sinema, lakini ndivyo ilivyokuwa, majambazi yamelichakaza gari la polisi kwa risasi wakati wakijiandaa kufanya uhalifu eneo la Nyegezi mkoani Mwanza.
Tukio hilo ambalo lilikuwa la aina yake lilitokea kwenye Kata ya Nyegezi, Mtaa wa Igubinya Wilaya ya Nyamagana mkoani hapa.
Majambazi hayo pamoja na askari polisi waligeuza mtaa huo kuwa eneo la mapambano baada ya kutupiana risasi kwa zaidi ya dakika 15, huku jambazi moja likiuawa kwa kupigwa risasi na askari waliokuwa kwenye mpambano huo.
Tukio hilo lilitokea jana saa sita mchana karibu na Kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), iliyopo Nyegezi Kona.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema majambazi hao walianza kuonekana saa 3:00 asubuhi, wakipita kwenye eneo hilo kila wakati na kuanza kuwatilia shaka.
Tukio hilo lilizua taharuki baada ya milio ya risasi kuanza kusikika, hali iliyosababisha wapita njia na wafanyabishara kuhaha na kukimbia huku na kule bila kujua kitu gani kimetokea.
Kati ya majambazi hayo alikuwemo mwanamke, ambaye naye alionekana akitupiana risasi na polisi kabla ya kukimbia kwa kutumia usafiri wa pikipiki, baada ya kuzidiwa nguvu na askari hao.
Wanajeshi pia walionekana kufurika kwenye eneo hilo, ambao nao walikuwa wanashuhudia kinachoendelea. Baada ya kuzidiwa nguvu majambazi mawili yalikimbia pembezoni mwa eneo la kambi ya jeshi, jambo lililoelezwa kuwa walikuwa wageni.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo, Emmanuel John alisema; “Watu hawa walianza kuonekana tangu asubuhi, tuliwatilia shaka, hatukujua wanataka kuiba wapi, lakini baada ya kujua tumewagundua na kwakuwa polisi walikuwa karibu, walikuja ghafla tukaanza kusikia milio ya risasi hewani.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa watu hao ambao walikuwa watatu walifanikiwa kukimbia baada ya kutupiana risasi na polisi, huku mmoja wao akiuawa baada ya kupigwa risasi ya paja.
Alisema polisi waliliua jambazi moja ambalo walilikuta na silaha aina ya SMG ikiwa risasi 19 ambazo hazijatumika pamoja na maganda ya rasasi 23 zilizotumika katika mapambano hayo.
“Nikweli kumetokea tukio la majambazi ambayo yalikuwa yanazunguka zunguka eneo la Nyegezi kona Mtaa wa Igubinya, walitiliwa shaka na watu wa kawaida baada ya kuwahoji,” alisema Mkumbo na kuongeza:
“Kwa bahati nzuri polisi tayari walikuwa wameweka mtego na walikuwa wamefika kwenye eneo hilo na kuyafuatilia. Majambazi hayo yalianza kupiga risasi, jambo ambalo polisi walikabiliana nalo na kuweza kuwadhibiti.”
Alisema jambazi mmoja aliuawa baada ya kupigwa risasi na wengine watatu wakakimbia, polisi inaendele kuwatafuta ili kuhakikisha wanakamatwa.
Mkumbo alisema gari lao aina Land Rover Defender liliharibiwa baada ya kushambuliwa kwa risasi, lakini hakuna askari aliyejeruhiwa kutokana na tukio hilo.
Eneo la Nyegezi limekuwa na matukio kadhaa ya uharifu ,ambapo mwaka jana matukio mawili yalitokea katika eneo hilo.
                                     Habari na: http://www.mwananchi.co.tz

Friday, 3 July 2015

Wanne wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua albino

                 https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcRwp1dXuojJxQfkcrHy6jHhwoxsuGfHSoEp1EDfA_RoIXSleGQA6g

Na Lauden Mwambona, Mwananchi

Mbeya. Washtakiwa wanne kati ya watano wa kesi ya kumuua mtu mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Henry Mwakajila mwaka 2008 wilayani Rungwe, wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa mjini hapa jana.
Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Nyanda za Juu Kusini aliwataja waliohukumiwa kuwa ni Hakimu Mwakalinga na Leonard Mwakisole wote wakazi wa Kijiji cha Kiwira wilayani Rungwe na Gerard Kalonge na Asangalwisye Kayuni wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje.
Mshtakiwa aliyenusurika kwenye kesi hiyo ni Mawazo Figomole ambaye alikuwa mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo ambaye aliachiwa huru baada ya ushahidi kutojitosheleza dhidi yake.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda hiyo, Dk Mary Revila alisema mahakama imeridhika pasipo shaka na ushahidi ulitolewa dhidi ya washtakiwa hao na kwamba, wanastahili kunyongwa hadi kufa huku akisisitiza kwamba ushahidi kwa mshtakiwa namba nne haukujitosheleza.
Awali, ilielezwa mahakamani hapo kwamba Februari 5, mwaka 2008, washtakiwa hao walimteka marehemu Henry akiwa katika Shule ya Sekondari Ukukwe wilayani Rungwe na kwenda kumuua.
Ilielezwa kwamba Mshtakiwa Kayuni ambaye ni mganga wa jadi maarufu kwa jina la Katiti alikutwa na utumbo uliodaiwa kuwa wa binadamu na hatimaye Mkemia Mkuu wa Serikali alithibitisha kwamba ulikuwa wa marehemu Henry.
Ilifafanuliwa kwamba mshtakiwa Kalonge alikutwa na vidole vinne na mifupa 10 iliyodaiwa kuwa ya binadamu na baadaye Mkemia Mkuu wa Serikali kuthibitisha kuwa ilikuwa ya marehemu Henry.
                                                             Habari na: http://www.mwananchi.co.tz

Thursday, 2 July 2015

WAKULIMA KIJIJI CHA AMANI WILAYANI LUDEWA WAFUNDWA ILI KUENDELEA KUZALISHA MAHINDI KWA WINGI.

                                            Siku ya wakulima wa Amani ndivyo ilivyokuwa 
Mgeni rasmi wa hafla hiyo ambaye ni ofisa kilimo wa wilaya ya Ludewa  Bw.Naftari Mundo akiongea na wakulima wa kata ya Mundindi katika kijiji cha Amani

Mkulima wa kijiji cha Amani wilayani Ludewa akitoa maelekezo namna ya elimu aliyoipata na na alivyoweza kuitumia katika uzalishaji wa zao la mahindi


                                        Afisa miradi wa shirika la ACTN Bw.Deogratias Ngotio
                                                                 wakulima wakipata somo

                                   mtaalamu wa mbegu za mahindi Bw.Mbele akiongea na wakulima
                             Mtaalamu wa mbolea toka YARA Bw.Shine akitoa elimu kwa wakulima








Wakulima wa kijiji cha amani wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wamepata elimu ya kilimo bora cha mazao ya mahindi,maharage na soya kupitia mashamba darasa ili kuweza kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao hayo kutokana na kijiji hicho kuwa kinara wa uzalishaji wa mazao ya aina hiyo wilayani hapa na mkoa wa Njombe kwa ujumla.

Elimu hiyo imetolewa hivi karibuni na wafadhiri ambao ni African conservation tillage network(ACTN BRITEN,RUDI na CRDB BANK wakiwa na kauli mbiu isemayo “kilimo hifadhi kwa mazao bora mavuno zaidi gharama nafuu na ardhi yenye rutuba”ikiwa na lengo kuu la kukuza uchumi kwa wakulima ambao wataanza kufanya kazi za kilimo kwa kisasa zaidi.

Akiongea katika hafla ya kufunga mafunzo hayo na wakulima wa kata ya Mundindi katika kijiji cha Amani wilayani Ludewa afisa miradi wa ACTN Bw.Deogratias Ngotio alisema kuwa  muungano wao ni kutoa mafunzo ya miradi shirikishi ya kuongeza tija ya uzalishaji katika nyanda za juu kusini mwa Tanzania kwa mazao ya mahindi,mpunga,maharage na soya kupitia elimu hiyo wakulima wataweza kunafaika na kilimo.

Bw.Ngotio alisema kuwa kilimo kimekuwa ni mzigo kwa wakulima kutokana na wakulima kutokuwa na elimu ya kutosha ya kilimo hivyo wadau wa kilimo nchini wameona ni bora kutoa elimu ya kilimo bora na kuhifadhi ardhi yenye rutuba ili kilimo kiweze kuwa ni ukombozi kwa wakulima na sio mzigo wa wakulima kama inavyoonesha katika meneo mengi.
 

Alisema kuwa wakulima walio wengi wamekuwa wakilima maeneo makubwa na kupata mavuno kidogo hali inayowakatisha tama wakulima na wengine huachana na kilimo kwa kuona hakina faida ikiwa haya yate husababishwa na elimu duni waliyonayo wakulima wa Nyanda za juu kusini lakini kwa kupitia wadau mbalimbali wa kilimo wanaoweza kutoa elimu baadhi ya wakulima wameshaanda kutambua umuhimu wa kilimo katika uchumi wa taifa na maisha yao kwa ujumla.

“tumegundua kuwa baadhi ya wakulima wanakatishwa tama ya kuendelea na kilimo kutokana na ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusiana na kilimo bora lakini kutokana na muungano wetu kwa pamoja tumeweza kutoa elimu ya shamba darasa ambapo baadhi ya wakulima wameanza kupata mafanikio kupitia mafunzo yetu hali ambayo inatupatia moyo wa kuendelea na mafunzo haya maeneo mbalimbali ili kuweza kuwainua wakulima katika mavuno zaidi”,alisema Bw.Ngotio.

Mmoja wa wakulima  wa Kijiji cha Amani Bw.Fransis Mlelwa alisema kuwa  kijiji hicho kinachoongoza wilayani Ludewa na mkoa wa Njombe kwa uzalishaji wa mazao ya mahindi na maharage ambapo mkulima wa hali ya chini anauwezo wa kuvuna magunia 1500 katika msimu mmoja wa kilimo kwa hali hiyo mashirika mbalimbali yameweza kuungana kuanza kutoa elimu ya kilimo bora.

Bw.Mlelwa alisema kuwa licha ya kupata mafunzo hayo ambayo ni msaada mkubwa kwao katika uzalishaji pia changamoto kubwa inayowakabili wakulima wa kijiji hicho ni upatikanaji wa masoko ya mahindi wakati wa mavuno kwani kumekuwana na shida kubwa kutokana na uzalishaji mkubwa wa mahindi walio nao.

Alisema licha ya kuwa Serikali imekuwa ikiyanunua mahindi kupitia wakala wa hifadhi ya chakula ya Taifa lakini bado wakulima wamekuwa wakibaki na kiasi kikubwa cha mahindi na kushindwa kupata masoko hivyo aliiomba Serikali kuiangalia upya wilaya ya Ludewa kutokana na uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi unaofanyika.

Mgeni rasmi wa hafla hiyo ya mafunzo ya shamba darasa ambaye ni ofisa kilimo wa wilaya ya Ludewa Bw.Naftari Mundo akitoa hotuba yake kwa wakulima hao alisema kuwa anatoa pongezi kwa shirika la ACTN kwa kubuni mafunzo hayo ambayo yatainua uchumi wa wakulima na Taifa kwa ujumla katika mpango mzima wa uboreshaji wa kilimo nchini.

Bw.Mundo alisema kuwa Serikali bado inaangalia uwezekano wa kutafuta mashirika mbalimbali ya nje ya nchi ili yaweze kuyanunua mazao ya wakulima kwa bei nzuri hivyo wakulima hawapaswi kukata tama ya kuendelea na kilimo kutokana na kukosa masoko kwani tayari juhudi za ununuzi wa mazao yao zimeshafanyika.

Aidha aliwataka wadau mbalimbali wa kilimo kuiga mfano wa ACTN na washirika wake katika kuendeleza kilimo nchini ili kuweza kuinua pato la taifa na kutengeneza maisha bora ya wakulima kwani kilimo nio msingi wa maisha ya mtanzania bila kilimo hakuna chakula.

mwisho.
                                              Habari na: http://habariludewa.blogspot.com