Dar/mikoani. Kura za maoni
ndani ya Chadema zimeanza kuwa chungu kwa baadhi ya wabunge. Mbunge wa
Mbulu, Mustapha Akoonay na mwingine wa Viti Maalumu, Susan Lyimo
(Kinondoni) jana waliangukia pua, huku mwenzao wa Karatu, Mchungaji
Israel Natse akitangaza kuachana na ubunge na kurejea katika Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
“Jumatano (leo),
nitawaaga rasmi wananchi wangu, binafsi niliombwa na Dk (Willibrod)
Slaa kugombea jimbo hili kwa miaka mitano,” alisema.
Lyimo
alianguka baada ya kupata kura 32 nyuma ya Mustafa Muro aliyepata kura
47. Wengine ni Rose Moshi (8), Agrey Mkwama (6), Gemeral Kaduma (4) na
Francis Nyerere (0). Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa
alisema tayari uchaguzi umefanyika katika majimbo matano.
Alisema
Mbulu Mjini, kulikuwa na wagombea wawili, Akoonay alipata kura 108
dhidi ya 132 alizopata Diwani wa Mbulu, Michael Sulle.
Golugwa
alisema, Joseph Selasini ametetea nafasi yake katika Jimbo la Rombo
baada ya kupata kura 313 akiwaacha mbali wapinzani wake Ben Sanane
aliyepata kura 26 na wengine kura mojamoja.
Babati
Mjini, Mbunge wa Viti Maalumu, Paulina Gekur ameibuka kidedea kwa kura
88 akiwatupa nje wapinzani wake, akiwamo mkuu wa wilaya wa zamani,
Gabriel Kimolo na wenzake.
Mbulu Vijijini, Aman Gaseri alishinda kwa kura 76 huku Michael Aweda akipata 75.
Jimbo la Same Magharibi: Jonas Kadeghe alishinda kwa kura 68 akifuatiwa na Christ Mbanjo aliyepata kura 49 na Gervas Mgonja kura 30.
Muleba Kaskazini:
Najim Kasange alipata kura 247 na kumshinda mwandishi wa habari
mkongwe, Ansbert Ngurumo aliyepata kura 55. Mgombea mwingine, Christina
Mwainunu alijitoa.
Jimbo la Ukonga, Nickson Tugara
alishinda kwa kura 59 hivyo kuwaacha kwa mbali wagombea wenzake 14.
Alifuatiwa na Waitara Mwikwabe aliyepata kura 49, Elly Dallas (15),
Deogratias Munishi (8), Lucas Otieno (6), Asia Msangi na Deogratias
Mramba waliopata kura tano kila mmoja na Gasto Makwetta (1). Wengine
saba hawakuambulia kura hata moja.
Butiama:
Yusuf Kazi aliibuka kifua mbele baada ya kujikusanyia kura 202 na
kuwapiku Adam Taya (39) na Issa Yusuf (31), Daniel Obeiya (3), Annicent
Marwa (2) na Lucas Ossoo na Marto Yohana waliopata kura moja kila
mmoja.
Nyamagana: Wenje aliibuka kidedea kwa kupata kura 194 na Patrick Masagati (32).
Nyamagana: Wenje aliibuka kidedea kwa kupata kura 194 na Patrick Masagati (32).
Msalala:
Paulo Ndundi alishinda kwa kura 113 akiwashinda Peter Machanga (49) na
Ezekiel Kazimoto (48). Wengine ni Emmanuel Mbise (43), Francis Makune
(15), Vincent Manoni Mhagwa (10) na Richard Mabilika aliyepata kura moja
na Stephen Bundala (0).
Sumbawanga:
Shadrack Malila aliibuka na ushindi wa kura 277 dhidi ya Kassian Kaegele
(28), Musa Ndile (9) na Matokeo Lyimo (1), Eliud Mwasenga na James
Kusula (0).
Nkasi Kusini: Alfred
Sotoka aliongoza kwa kupata kura 70 akifuatiwa na Kaminga Hyporito (39),
Emmanuel Sungura (9), Edson Ndasi (4) na Joseph Kitakwa (2).
Nkasi Kaskazini: Keissy Sudi alishinda kwa kura 158 na kufuatiwa na Triphone Simba (70) na Stanley Khamsini (5).
Kwela:
Daniel Ngogo aliwabwaga wenzake kwa kura 151 akifuatiwa na James
Mwamlyela (117), Ameri Nkulu (27), Alstidi Maufi (13) na Michael Moka
(4).
Mlalo: Kelvin Shemboko alipata kura 56 akifuatiwa na Lewis Kopwe (31), Jumanne Pazia (15) na Mkazeni Mkazeni (0).
Mabadiliko ya ratiba
Wakati
kukiwa na sintofahamu na wanachama wanaojiunga na Chadema huku kipindi
cha kurejesha kikiwa kimekwisha, chama hicho kimetangaza mabadiliko
kwenye ratiba ya kurudisha fomu hasa katika majimbo mapya yaliyotangazwa
na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Julai 12.
Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema jana: “Fomu za
kugombea kwenye majimbo hayo zitaendelea kutolewa na hata kura ya maoni
watapiga tofauti na majimbo yaliyokuwapo.”
Alisema hata
katika majimbo mengine, Sikukuu ya Eid el Fitr iliingilia ratiba
iliyopangwa awali na kwamba uongozi wa chama umeona kuwa ipo haja ya
kuongeza siku ili kutenda haki kwa wale waliokosa kulipia fomu benki
kutokana na sherehe hizo.
“Kinachotakiwa sasa ni katibu
wa wilaya kutuma mapendekezo ya kuongeza siku atakazoona zitafaa kwa
zoezi hilo na makao makuu itaidhinisha hilo,” aliongeza.
Msimamizi ‘aingia mitini’
Uchaguzi
wa mgombea ubunge Mbeya Vijijini ulikwama baada ya msimamizi wa kura za
maoni wa Chadema, Christopher Mwamsiku kutokomea kusikojulikana katika
hatua za mwisho.
Kitendo hicho kiliwafanya wajumbe wa
Kamati ya Siasa Mbeya Vijijini na mawakala kubaki njiapanda wasijue cha
kufanya huku wengine wakidai kuwa hizo ni njama za kutaka kumbeba mmoja
wa wagombea.
Mwenyekiti wa Chadema wilayani hapo,
Jackson Mwasenga alishindwa kutoa maelezo ya tukio hilo huku akimtaka
katibu wake kuzungumza.
Katibu huyo, James Mpalaza alisema: “Hata sisi hapa kama unavyotuona tumeduwaa hatujui ni kwa nini ameondoka.”
Alipotafutwa
kwa simu, Mwamsiku alijibu kwa kifupi: “Sijakimbia, nimeondoka kwa
utaratibu mzuri tu… lakini siwezi kukwambia ni kwa nini kamuulize
Mwasenga anayo majibu yote niache nipumzike.”
Dalili za
kuvurugika kwa uchaguzi huo zilianza wakati wa kuhesabu kura baada ya
Mwenyekiti wa Bavicha, Mbeya Vijijini kuingia ndani ya chumba hicho
akidaiwa hahusiki jambo lililozua mzozo mkubwa uliodumu kwa takriban
dakika tano hadi alipotoka.
Wengine wajitokeza Chadema
Tabora Mjini: Peter Mkufya, Nhombar Imajamasallah, Elifuraha Kisangi, Said Mwakasekela na Raymond Maganga.
Kaliua: Anthony Mwakammoja, Godluck Jilinga, Prosper Guga, Peter Msazya na Wilson Lukobe.
Ulyankulu: Dk Deus Kitapondya.
Igalula: Mustapha Kado na James Kabepele.
Tabora Kaskazini: Daud Nteminyanda.
Igunga: Joseph Kashindye, Ngasa Mbojenamba na Gw’igulu Darushi.
Manonga: Ally Halfan Nguzo, Athanas Shija Michael na Simon Seleli.
Nzega Vijijini: Albino Mayani Simbila na Nicholaus Zakaria.
Nzega Mjini: Gisberth Kabamba, Daniel Simba, Boniface Masasi, Charles Mabula, Monica Nsaro, Ally Ndee na Mary Atonga.
Bukene: Alex Mpugi, Lumola Kahumbi, Elias Machibya, Dickson Kagembe na Emmanuel Ntobi.
Rorya):
Mtatiro Sanya, Evangel Dea, Kevin Makooko, Matiko Seruka, Emmanuel
Werema, Ezekiel Kachare, Steven Owawa, Opiyo Nalo, Herman Odemba,
Thomas Risa na Ochora Ndira.
Tarime Vijijini: John Heche, Peter Busene, Moses Yomami, Prosper Nyamuhanga, Johanes Manko na Fabiani Mwita.
Tarime Mjini: Ester Matiko, Lucas Ngoto, Christopher Chomete, Charles Werema na Martinus Joseph.
Waliojitokeza CCM
Arumeru Mashariki: Elirehema Kaaya, Jackson Ezekiel, John Sakaya. Angela Palangyo, William Sarakikya, Dk Daniel Pallangyo na Siyoi Sumari.
Longido:
Philip Kitesho, Dk Stivin Kiluswa, Lee Mamaseta, Daniel Marari, Lesioni
Mollel, Joseph Kulunju, Lemayani Logoliye na Emmanuel Sirikwa.
Monduli: Sakata Babuti, Loota Sanare, Loliayu Mkoosi, Namelock Sokoine, Mbayani Kayai na Amani Turongei.
Arumeru Magharibi: Loy Thomas Sabaya, Daudi Mollel, Elisa Mollel, Osilili Losai, Henri Majola, Lekoko Piniel na Lomoni Mollel.
Ngorongoro: Eliaman Laltaika, Elias Ngolisa, Joseph Parsambei, Patrick Kasongo, William Ole Nasha na Saning’o Telele.
Karatu: John Dodo, Dk Willbrod Rorri, Joshua Mbwambo na Rajabu Malewa.
Arusha Mjini:
Mustapha Panju, Justin Nyari, Philemon Mollel, Victa Njau, Thomas
Munisi, Hamis Migire, Admund Ngemera, Moses Mwizarubi, Ruben Mwikeni,
Endrew Lymo, Salehe Kiluvia, Lukiza Makubo, Mohammed Omar na Emmanuel
ole Ngoto.
Mkalama: Mgana Msindai,
Profesa Shaban Mbogho, Nakey Sule, Orgenes Joseph Mbasha na Allan Kiula,
Emmanuel Mkumbo, Dk Kissui Kissui, William Makali, Kyuza Kitundu, Dk
Charels Mgana, Salaome Mwambu, Francis Mtinga, Dk George Mkoma na Lameck
Itungi.
Manyoni Magharibi: John
Lwanji, Eliphas Lwanji, Jamal Kuwingwa, Jane Likuda, Mohammed Makwaya,
Yahaya Masare, Athumani Masasi, Yohana Msita, Moshi Mmanywa, Adimini
Msokwa, Dk Mwanga Mkayagwa, Rashidi Saidi na Francis Shaban.
Manyoni Mashariki: Dk Pius Chaya, Joseph Chitinka, Alex Manonga, Jumanne Mtemi, Daniel Mtuka, Harold Huzi na Gaitani Romwad.
Singida Mashariki: Jonathan Njau, Hamisi Maulid, Mdimi Hongoa, Jocab Kituu, Emmanuel Hume na Martin Lissu.
Ikungi Magharibi: Dinawi Gabaraiel, Hamisi Lissu, Wilson Khambaku, Dk Hamisi Mahuna, Dk Grace Puja, Yona Makala, Elibariki Kingu na Hamisi Ngila.
Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba, David Jairo, Juma Kilimba na Amon Gyuda.
Singida Mjini: Hassan Mazala, Amani Rai, Mussa Sima, Leah Samike, Philemon Kiemi na Juma Kidabu.
Singida Kaskazini: Lazaro Nyalandu, Amosi Makiya, Justin Monko, Michael Mpombo, Sabasaba Manase, Yahana Sinton, Mugwe na Aron Mgogho.
Imeandikwa
na Robert Kakwesi, Dinna Maningo, Mussa Juma, Filbert Rweyemamu, Gaspar
Andrew na Mussa Juma, Joseph Lyimo, Mussa Mwangoka, Godfrey Kahango na
Julius Mathias.
Habari kutoka:http://www.mwananchi.co.tz
Habari kutoka:http://www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment