Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na familia ya Bw. Saleh Juma Saleh (mwenye mtoto), yenye watoto sita wenye ulemavu wa aina tofauti, huko nyumbani kwao Kinyasini Mkarafuuni Wilaya ya Wete. (Picha na OMKR)
Na: Hassan Hamad, OMKR
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo
ameitembelea na kuifariji familia ya Bw. Saleh Juma Saleh yenye watoto
sita wenye ulemavu.
Akizungumza
na familia hiyo nyumbani kwao Kinyasini Mkarafuuni Wilaya ya Wete
Pemba, katika mfululizo wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa
wa Kaskazini Pemba, Maalim Seif ameitaka kuwa na subra na upendo kwa
watoto hao wakielewa kuwa huo ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Amemuagiza
Mkuu Mkuu wa Wilaya ya Wete kukutana na familia hiyo, ili kuandaa
mipango itakayoweza kuwasaidia katika kuendesha maisha yao na shughuli
zao za kila siku.
Baba
mzazi wa watoto hao Bw. Saleh Juma Saleh amesema watoto wake wanashindwa
kusoma kutokana na kukosa nyenzo kwa vile wote sita hawawezi kutembea.
Amesema
watoto hao wakiwemo wanne wa kike na wawili wa kiume wanasikia vizuri,
wanazungumza na wanafahamu wanachoambiwa, ingawaje baadhi ya wakati
wanapoteza uelewa kutokana na hali ya ulemavu wao.
Amefahamisha
kuwa iwapo watapatiwa nyenzo wataweza kwenda skuli na kusoma kama
wenzao wengine, na kuiomba serikali na wasamaria wema kuwapatia misaada
inayostahiki, ili nao waweze kwenda skuli.
Habari na: http://rweyunga.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment