Kwa muda mrefu wahudumu wa afya ya masuala ya ngono wamesisitiza
matumizi ya mipira ya kondomu kama mbinu bora zaidi dhidi ya maambukizi
ya virusi vya ukimwi.
Lakini tabia moja hatari ya kutumia madawa ya kulevya na wapenzi wa jinsia moja inazidi kuibua wasiwasi.
kumekuwa
na njia nyingi za kinga dhidi ya virusi vya ukimwi, lakini kuna dawa
moja mpya - Pre-Exposure Prophylaxis (PrEP) - ambayo inaweza kutoa kinga
dhidi ya maambukizi ya ukimwi iwapo itatumika kabla ya kushiriki ngono.
Utafiti
unaofanywa na daktari Sheena McCormack kutoka chuo kikuu cha London,
unasema kwamba unapomeza dawa hiyo, inazuia maambukizi ya ukimwi kwa
kuzuia ongezeko la virusi, hii ni baada ya majaribio kufanyiwa kundi
moja la wapenzi wa jinsia moja, ambao wamo katika hatari kubwa zaidi ya
maambukizi
Shirika la afya duniani limetambua kwamba dawa hiyo ya tembe inaweza kupunguza maambukizi kwa kiwango kikubwa.
Baadhi ya wakosoaji wanasema kuwa dawa ya aina hii inahamasisha watu wengi kushiriki ngono bila kutumia mipira ya kondomu
Hata
hivyo matumizi ya dawa hii haizuii maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama
vile kisonono na kaswende, je, kukubalika kwa matumizi ya dawa hii
duniani kunamaanisha ongezeko la magonjwa ya zinaa.
Habari na: http://www.bbc.com
Misime alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu wiki hii ambayo inatarajiwa
kuwa na ugeni mkubwa wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM ambao amesema
kuwa unakadiriwa kuwakusanya watu takribani 10,000.
Dodoma. Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Dodoma, David Misime amewataka wageni wasiokuwa na shughuli muhimu ya
kufanya mkoani hapa kutokuja katika kipindi cha juma hili ili kuepusha
usumbufu utakaojitokeza.
Misime alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu wiki hii ambayo inatarajiwa
kuwa na ugeni mkubwa wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM ambao amesema
kuwa unakadiriwa kuwakusanya watu takribani 10,000.
Alisema ili kuepusha usumbufu utakaojitokeza kama
vile kukosa mahali pa kulala, ni vyema kama mtu hana shughuli ya muhimu
ya kufanya mjini hapa asije mpaka mkutano huo utakapokwisha.
“Kuna wengine wanataka kuja kwa ajili ya ushabiki
tu au kuja kushuhudia tukio zima na hata kama hawatakuja haitawaathiri
kitu hivyo ni vyema wasije ili kuepusha usumbufu,” alisema Misime.
Alisema Jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha
ulinzi na usalama kwa wananchi wote watakaofika katika mkutano huo na
kuwataka wananchi kutoa taarifa za viashiria vyovyote vya uvunjifu wa
amani katika maeneo yao.
Aliwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni
kuhakikisha kuwa vitu vyote vyenye thamani vya wateja wao vinatunzwa
vizuri ili kuepusha usumbufu au kupotea kwenye mikono yao.
Ulinzi mkali bungeni
Jana, Polisi waliimarisha ulinzi bungeni kwa
kuongeza idadi ya askari na pia kufunga kipande cha barabara kuanzia
kwenye mzunguko wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani kupitia eneo
la Bunge hadi mwanzo wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Tawi la
Dodoma.
Kulikuwa na idadi kubwa ya polisi wa usalama
barabarani, utepe mweupe uliofungwa katika barabara hiyo huku kukiwekwa
kibao kilichoandikwa kwa maandishi mekundu, “barabara hii imefungwa.”
Alipoulizwa kuhusu hatua hiyo, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Dodoma, David Misime (pichani) alisema kufungwa kwa barabara
hiyo ni miongoni mwa shughuli za usalama.
Habari na: http://www.mwananchi.co.tz
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana
imewahukumu kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya shilingi
milioni 5 kila mmoja aliyekuwa Waziri wa Fedha Basil Mramba na
aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona baada ya kuwatia
hatiani kwa makosa mawili.
Hukumu hiyo imetolewa na Jaji John
Utamwa, Jaji Sam Rumwenyi pamoja na Hakimu Saul Kinemela ambapo
mtuhumiwa wa tatu wa kesi hiyo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha, Gray Mgonja amekutwa hana hatia.
Washitakiwa hao walikuwa
wanakabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka na
kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 kutokana na
kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya MS
Alex Stewart ya Uingereza.