Kashfa ya ESCROW vigogo watajwa TZ
Ripoti
ya Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali imewataja baadhi ya vigogo
wanaohusika na kashfa ya IPTL Nchini Tanzania akiwemo Waziri Mkuu na
kuwataka kuwajibika kisiasa na kisheria.
Sakata hiyo ya IPTL
inahusihswa na upotevu wa mamilioni ya fedha na kwa muda mrefu umezusha
mjadala mzito katika bunge la Tanzania.Katika ripoti hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe na makamu mwenyekiti Deo Filikunjombe, imethibitisha kuwepo mazingira ya udanganyifu na ufisadi katika mchakato wa malipo yaliyofanyika na kueleza kuwa upotevu huo wa fedha ungeweza kudhibitiwa kama kungekuwa na uwajibikaji wa kutosha kwa baadhi ya viongozi.
Kamati hiyo imewataja viongozi wengine wanaotakiwa kuwajibika kutokana na kashfa hiyo kuwa ni mwanasheria,Waziri wa nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati pamoja na viongozi wengine wa bodi.
Kashfa nyingine zilizowahi chukua uzito mkubwa katika bunge la Tanzania na kusababisha viongozi kuwajibika wakiwemo Waziri Mkuu ni pamoja na kashafa ya Richmond,EPA na sasa hii ya ESCROW ambayo kwa mara nyingine kamati hiyo imeonyesha wazi mapendekezo yake ya kutaka kuwajibika kwa waziri mkuu, Mawaziri na viongozi wengine.