Na Lauden Mwambona, Mwananchi
Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini aliwataja waliohukumiwa kuwa ni Hakimu Mwakalinga na Leonard
Mwakisole wote wakazi wa Kijiji cha Kiwira wilayani Rungwe na Gerard
Kalonge na Asangalwisye Kayuni wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje.
Mshtakiwa aliyenusurika kwenye kesi hiyo ni Mawazo
Figomole ambaye alikuwa mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo ambaye
aliachiwa huru baada ya ushahidi kutojitosheleza dhidi yake.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda
hiyo, Dk Mary Revila alisema mahakama imeridhika pasipo shaka na
ushahidi ulitolewa dhidi ya washtakiwa hao na kwamba, wanastahili
kunyongwa hadi kufa huku akisisitiza kwamba ushahidi kwa mshtakiwa namba
nne haukujitosheleza.
Awali, ilielezwa mahakamani hapo kwamba Februari
5, mwaka 2008, washtakiwa hao walimteka marehemu Henry akiwa katika
Shule ya Sekondari Ukukwe wilayani Rungwe na kwenda kumuua.
Ilielezwa kwamba Mshtakiwa Kayuni ambaye ni mganga
wa jadi maarufu kwa jina la Katiti alikutwa na utumbo uliodaiwa kuwa wa
binadamu na hatimaye Mkemia Mkuu wa Serikali alithibitisha kwamba
ulikuwa wa marehemu Henry.
Ilifafanuliwa kwamba mshtakiwa Kalonge alikutwa na
vidole vinne na mifupa 10 iliyodaiwa kuwa ya binadamu na baadaye Mkemia
Mkuu wa Serikali kuthibitisha kuwa ilikuwa ya marehemu Henry.
Habari na: http://www.mwananchi.co.tz
Habari na: http://www.mwananchi.co.tz