Fanya haya upate mafanikio maishani
Na Emanuel Gingi
Kwa ufupi
Hata hivyo, unajua siri ya kufanikiwa maishani?
Makala haya yanajaribu kutaja baadhi ya njia za unazoweza kupita ili
ufike katika safari yako.
Hata hivyo, unajua siri ya kufanikiwa maishani?
Makala haya yanajaribu kutaja baadhi ya njia za unazoweza kupita ili
ufike katika safari yako.
Kuwa na mawazo chanya: Akili yako ni kifaa cha
ajabu, chaweza kuamua kufanikiwa au kutofanikiwa. Fanya unachoamua
kufanya usifanye unachoambiwa ufanye pasipo kukipenda. Inategemea na
mawazo uliyoyajaza ndani ya akili yako, kwa hiyo kwa nini usijaze mawazo
yako au akili yako na hisia chanya za kufanikiwa?
Zungumza kuhusu mafanikio: Wachunguzi wanasema
takribani asilimia 75 ya mawazo ya ndani ya mtu ni hasi, yatupasa
kuyabadili mawazo au maneno na kuwa chanya muda wote. Kwa mfano, badala
ya kusema tatizo sema fursa, badala ya kusema hakuna kitu ninachoweza
kufanya, sema naangalia hatua nyingine.
Jipe mazoezi ya kufanikiwa: Inakupasa kujipa
mazoezi ya kujihamasisha hata kama muda mwingine huwezi kujisikia vyema;
lazima utoke na kujihamasisha katika hatua chanya.
Jitose: Lazima uishi maisha ya utulivu au kuridhika, jiepushe na mawazo ya kufeli.
Wasome waliofanikiwa: Ukitaka kufanikiwa lazima
utafute maisha au uige maisha ya watu waliofanikiwa. Kati ya vitabu au
nyaraka nzuri za kukujenga ni pamoja na kutafuta machapisho
yanayozungumzia watu kama kina Mwalimu Julius Nyerere, Benjamin
Franklin, Abraham Lincoln, Mahatma Ghandhi na wengineo.
Hivi ni vitabu vitakavyokuongezea mbinu au ujuzi
wa kushinda changamoto na kuongeza thamani ya kubadilisha maisha yako
yakawa mazuri.
Panda mbegu ya mafanikio: Inakupasa wewe mwenyewe
kupanda mawazo ya mafanikio kwa kufanya yafuatayo: Nenda sehemu yeyote
tulivu labda nyumbani au sehemu yeyote na uzime radio na televisheni.
Tafuta kiti kikufaacho na utulize mawazo, anza kufikiria lengo moja
ulikamilishe.
Chukua maono ya kukuwezesha au kukamilisha maono
yako yafanikiwe. Ukianza kuwa na maono utaanza kujihisi vizuri, utasema
vizuri, utaona vizuri. Ni wewe mwenyewe tu. Angalizo ni kuwa kama
hujaweka muda maalumu, ni vigumu kukamilisha jambo litokee
Fikiria mafanikio: Lazima uone picha kubwa kwa
kila kitu unachokifanya usipoteze muda kwa vitu ambavyo si muhimu katika
maisha. Vaa utofauti chanya kwenye familia, jumuiya, kampuni au
taasisi. Fikiria makubwa leo kesho utapata mazuri, ukweli ni kwamba
ukifikiria makubwa lazima upate makubwa, ukifikiria madogo utapata
madogo.
Jiwekee malengo: Vitu ambavyo vinaangusha watu
katika maisha ni kukosa malengo madhubuti. Weka malengo katika uchumi,
familia, afya, roho na pia taaluma .
Hatua za kuchukua ni hizi: hakikisha lengo au malengo yamepangika, yanafikiwa, yanaeleweka, na yana muda maalumu wa kuyafikia.
Jali mwonekano wako: Watu wenye kupenda mafanikio
kwanza wako makini kimwonekano. Ukweli ni kwamba ukiwa upo vizuri
kimwonekano utajisikia vizuri. Vaa mavazi na sura ya mafanikio. Kuwa na
akili ya mafanikio, wenye hamasa ndiyo wanaokwenda mbele kwa kujiamini.
Wasaidie wengine: Endeleza nia yako kwa kuwasaidia
wengine, shirikisha kipawa chako na wengine bila kutarajiwa kulipwa.
Faida kubwa ambayo utaipata ni kujenga ujasiri mkubwa pia uzoefu ambao
utakufanya uwe tofauti. Daima watu wenye mafanikio, wanapenda hamasa
chanya na zenye maana huku wakiwasaidia wengine.
Habari kutoka Gazeti la Mwananchi.
Habari kutoka Gazeti la Mwananchi.