Tuesday, 30 June 2015

CHADEMA WATIFUANA LUDEWA MZIMU WA UKABILA WAWATAFUNA

 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kimeingia katika mgogoro mkubwa kutokana na wanachama wa chama hicho kushangazwa na kitendo cha uongozi wa chama hicho kutoka kanda ofisi za mkoa wa Mbeya kufanya uchaguzi wa viongozi wa wilaya kwa kushitukiza.

Wakiongea kwa nyakazi tofauti baadhi ya wananchama wa chama hicho hapa wilayani kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa kuhofia kuvuliwa uanachama walisema kuwa licha ya kuwa uongozi wa awali ulikuwa na mapungufu ya kuwa na migogoro ya mara kwa mara hasa katika kuendekeza ukabila lakini ulikuwa na watu wenye uwezo wa kufanya maamuzi kutokana na elimu waliokuwa nayo.

Walisema kuwa kitendo cha viongozi wa kanda kuitisha mkutano mkuu wa dharula na kufanya uchaguzi wa viongozi wengine kimewashitua wanachama hao ambao walikuwa na imani kubwa na viongozi wao wa awali hivyo kuwaletea viongozi wengine ni sawa na kukivuruga chama na kusababisha kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu ujao.

Aliyekuwa katibu mwenezi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Ludewa Bw.Kathbet Haule apotakiwa kutolea maelezo kuhusiana na mgogoro huo unaokitafuna chama alisema kuwa viongozi wa wilaya akiwemo yeye kama katibu mwenezi hawajavuliwa madaraka  na nib ado wao ni viongozi wa wilaya licha ya kuwa waliochaguliwa kupitia uongozi wa kanda wanajinadi kuwa wao ndio viongozi.

“sisi ni viongozi wa chadema wilaya ya Ludewa nabado tunatambulika waliochaguliwa ni tume tu kama taxforce itakayofanya kazi katika kipindi hiki cha uchaguzi lakini sisi tutabaki kuwa viongozi wa wilaya na kama wanawatangazia watu kuwa sisi tumepigwa chini huo ni uongo kwani kazi ya ofisi ya kanda si kuchagua viongozi wa wilaya”,alisema Bw.Haule.

Kuhusiana na mgogoro mkubwa unaokitafuna chama hicho wilayani hapa Bw.Haule alisema kuwa ni kweli baadhi ya viongozi ndani ya chama wamekuwa wakishindwa kuelewana kutokana na baadhi ya mambo mfano ni katibu na mwenyekiti ndio walikuwa na mgogoro ambao ungeweza kumalizika kabla ya kufanya uchaguzi uliofanyika. 

Bw.Haule alisema kuwa suala la ukabila ndani ya chama hicho wilayani Ludewa limekuwa likuzungumzwa mara kwa mara licha ya kuwa hakuna malalamiko kwa maandishi yaliyowahi wasilishwa katika ofisi yake na katibu ila kumekuwa na minong’ono kwa baadhi ya wanachama kulalamikia jambo hilo hivyo hakuna uhakika kama jambo hilo ni chanzo cha migogoro ndani ya chama.
                          Habari na: http://habariludewa.blogspot.com

Wasichana wa Chibok washinikizwa kuua

Wasichana wa Chibok washinikizwa kuua

     Wasichana wa Chibok waliotekwa kaskazini mwa Nigeria zaidi ya mwaka mmoja
Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC limeelezwa kuwa baadhi ya wasichana waliotekwa na wanamgambo mjini Chibok Nigeria wamekuwa wakishinikizwa kuwaua Wakristo.
Wanawake watatu ambao wanasema walikuwa wakishikiliwa katika kambi moja na wasichana hao wanasema wapiganaji wa BOKO HARAM waliwafunga mikono wanaume wa Kikristo. Wasichana hao waliwachinja wanaume hao kwa kuwakata shingo.
Wanawake hao wanasema baadhi ya wasichana hao wa Chibok walikuwa na silaha. Baadhi ya wasichana waliwachapa mateka wengine wa kike. Haikuwa rahisi kuthibitisha ukweli wa taarifa hii. Wasichana 219 kati ya zaidi ya wasichana 270 waliotekwa kutoka shule moja ya bweni ya Chibok bado wanashikiliwa na Boko Haram.
              Habari na: BBC

Ghana yazindua gari lake linalojulikana kwa jina la KANTANKA

Ghana yazindua gari lake linalojulikana kwa jina la KANTANKA

Gari la kantanka nchini Ghana
Wakati unapoangazia swala la utengezaji magari mataifa ya Afrika kwa kawaida hayaorodheshwi katika swala hilo.
Lakini hilo sasa huenda likabadilika kufuatia kuwasili kwa kampuni ya magari ya Ghana Kantanka ambayo hivi karibuni yataanza kuingia katika soko.
Miongoni mwa magari ya kampuni hiyo ni lile la lita mbili aina ya 4 by 4 ambalo linatarajiwa kuuzwa kwa takriban pauni 14,000.
null
Gari aina ya kantanka
Lakini je,kampuni hiyo itaweza kukabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa magari kama vile Toyota,Land Rover na BMW?.
Kwadwo sarfo ni mwana wa mmiliki wa magari hayo.
Babaake ni m'bunifu ambaye pia ni kiongozi wa dini.Hupata fedha kutokana na kilimo na uchimbaji.
Magari ya Kantanka yanafananishwa na magari makubwa kama vile Toyota Prado ama MItsubishi Pajero.
null
Magari aina ya kantanka
Mbele ya gari hilo kuna michoro ya kucha za chui pamoja na nembo ya kampuni hiyo ya nyota ya Afrika.
Kulingana na raia mmoja wa Ghana uvumbuzi kama huo haujafanyika nchini humo.
Tunapenda kununua bidhaa kutoka nje kwa hivyo italazimu kufanyika kwa mauzo ya ziada kwa gari hizi za kantanka kukubalika.
Profesa Robert Ebo Hinson ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo katika chuo kikuu cha Ghana:Nadhani kile kilichotokea hapo awali ni kwamba tumefanywa tuamini kwamba kile kinachotengezwa katika mataifa ya magharibi ni
null
Gari aina ya kantanka
bora zaidi kwa sababu zote zile.
Wakati mwengine bidhaa zinazotengezwa kutoka Ghana haziwezi kudumu.
Serikali ya Ghana inaelewa kikwazo hicho na tayari imeanzisha kampeni kubwa ya kuwafanya wakaazi kununua bidhaa zinazotengezwa nchini humo.
Waziri wa biashara daktari Ekow Spio Gabrah anaongoza kampeni hiyo na anasema:Nitaendesha moja ya magari haya,kwa kweli niliketia gari moja wakati lilipokuwa likitengezwa na nafurahi kuwa na moja kama gari langu rasmi.
null
Magari aina ya kantanka kutoka Ghana
Waziri na rais wana uwezo wa kuendesha magari hayo kwa gharama ya walipa ushuru.
Lakini je,raia wataweza kutumia fedha zao wenyewe kulipia gharama za kulinunua gari hilo?
Inaonekana kwamba raia wengi kama alivyodai hapo awali Professa wana wasiwasi kuhusu usalama wa gari hilo na kudumu kwake.
null
Gari aina ya kantanka
Je, unadhani wasiwasi huo huenda ukaathiri uzalishaji wa magari hayo? Kulingana na Kwadwo Sarfo gari hilo la kwanza kutengezwa nchini Ghana litapata umaarufu.
                                           Habari na: BBC