Tuesday, 30 June 2015

CHADEMA WATIFUANA LUDEWA MZIMU WA UKABILA WAWATAFUNA

 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kimeingia katika mgogoro mkubwa kutokana na wanachama wa chama hicho kushangazwa na kitendo cha uongozi wa chama hicho kutoka kanda ofisi za mkoa wa Mbeya kufanya uchaguzi wa viongozi wa wilaya kwa kushitukiza.

Wakiongea kwa nyakazi tofauti baadhi ya wananchama wa chama hicho hapa wilayani kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa kuhofia kuvuliwa uanachama walisema kuwa licha ya kuwa uongozi wa awali ulikuwa na mapungufu ya kuwa na migogoro ya mara kwa mara hasa katika kuendekeza ukabila lakini ulikuwa na watu wenye uwezo wa kufanya maamuzi kutokana na elimu waliokuwa nayo.

Walisema kuwa kitendo cha viongozi wa kanda kuitisha mkutano mkuu wa dharula na kufanya uchaguzi wa viongozi wengine kimewashitua wanachama hao ambao walikuwa na imani kubwa na viongozi wao wa awali hivyo kuwaletea viongozi wengine ni sawa na kukivuruga chama na kusababisha kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu ujao.

Aliyekuwa katibu mwenezi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Ludewa Bw.Kathbet Haule apotakiwa kutolea maelezo kuhusiana na mgogoro huo unaokitafuna chama alisema kuwa viongozi wa wilaya akiwemo yeye kama katibu mwenezi hawajavuliwa madaraka  na nib ado wao ni viongozi wa wilaya licha ya kuwa waliochaguliwa kupitia uongozi wa kanda wanajinadi kuwa wao ndio viongozi.

“sisi ni viongozi wa chadema wilaya ya Ludewa nabado tunatambulika waliochaguliwa ni tume tu kama taxforce itakayofanya kazi katika kipindi hiki cha uchaguzi lakini sisi tutabaki kuwa viongozi wa wilaya na kama wanawatangazia watu kuwa sisi tumepigwa chini huo ni uongo kwani kazi ya ofisi ya kanda si kuchagua viongozi wa wilaya”,alisema Bw.Haule.

Kuhusiana na mgogoro mkubwa unaokitafuna chama hicho wilayani hapa Bw.Haule alisema kuwa ni kweli baadhi ya viongozi ndani ya chama wamekuwa wakishindwa kuelewana kutokana na baadhi ya mambo mfano ni katibu na mwenyekiti ndio walikuwa na mgogoro ambao ungeweza kumalizika kabla ya kufanya uchaguzi uliofanyika. 

Bw.Haule alisema kuwa suala la ukabila ndani ya chama hicho wilayani Ludewa limekuwa likuzungumzwa mara kwa mara licha ya kuwa hakuna malalamiko kwa maandishi yaliyowahi wasilishwa katika ofisi yake na katibu ila kumekuwa na minong’ono kwa baadhi ya wanachama kulalamikia jambo hilo hivyo hakuna uhakika kama jambo hilo ni chanzo cha migogoro ndani ya chama.
                          Habari na: http://habariludewa.blogspot.com

Wasichana wa Chibok washinikizwa kuua

Wasichana wa Chibok washinikizwa kuua

     Wasichana wa Chibok waliotekwa kaskazini mwa Nigeria zaidi ya mwaka mmoja
Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC limeelezwa kuwa baadhi ya wasichana waliotekwa na wanamgambo mjini Chibok Nigeria wamekuwa wakishinikizwa kuwaua Wakristo.
Wanawake watatu ambao wanasema walikuwa wakishikiliwa katika kambi moja na wasichana hao wanasema wapiganaji wa BOKO HARAM waliwafunga mikono wanaume wa Kikristo. Wasichana hao waliwachinja wanaume hao kwa kuwakata shingo.
Wanawake hao wanasema baadhi ya wasichana hao wa Chibok walikuwa na silaha. Baadhi ya wasichana waliwachapa mateka wengine wa kike. Haikuwa rahisi kuthibitisha ukweli wa taarifa hii. Wasichana 219 kati ya zaidi ya wasichana 270 waliotekwa kutoka shule moja ya bweni ya Chibok bado wanashikiliwa na Boko Haram.
              Habari na: BBC

Ghana yazindua gari lake linalojulikana kwa jina la KANTANKA

Ghana yazindua gari lake linalojulikana kwa jina la KANTANKA

Gari la kantanka nchini Ghana
Wakati unapoangazia swala la utengezaji magari mataifa ya Afrika kwa kawaida hayaorodheshwi katika swala hilo.
Lakini hilo sasa huenda likabadilika kufuatia kuwasili kwa kampuni ya magari ya Ghana Kantanka ambayo hivi karibuni yataanza kuingia katika soko.
Miongoni mwa magari ya kampuni hiyo ni lile la lita mbili aina ya 4 by 4 ambalo linatarajiwa kuuzwa kwa takriban pauni 14,000.
null
Gari aina ya kantanka
Lakini je,kampuni hiyo itaweza kukabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa magari kama vile Toyota,Land Rover na BMW?.
Kwadwo sarfo ni mwana wa mmiliki wa magari hayo.
Babaake ni m'bunifu ambaye pia ni kiongozi wa dini.Hupata fedha kutokana na kilimo na uchimbaji.
Magari ya Kantanka yanafananishwa na magari makubwa kama vile Toyota Prado ama MItsubishi Pajero.
null
Magari aina ya kantanka
Mbele ya gari hilo kuna michoro ya kucha za chui pamoja na nembo ya kampuni hiyo ya nyota ya Afrika.
Kulingana na raia mmoja wa Ghana uvumbuzi kama huo haujafanyika nchini humo.
Tunapenda kununua bidhaa kutoka nje kwa hivyo italazimu kufanyika kwa mauzo ya ziada kwa gari hizi za kantanka kukubalika.
Profesa Robert Ebo Hinson ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo katika chuo kikuu cha Ghana:Nadhani kile kilichotokea hapo awali ni kwamba tumefanywa tuamini kwamba kile kinachotengezwa katika mataifa ya magharibi ni
null
Gari aina ya kantanka
bora zaidi kwa sababu zote zile.
Wakati mwengine bidhaa zinazotengezwa kutoka Ghana haziwezi kudumu.
Serikali ya Ghana inaelewa kikwazo hicho na tayari imeanzisha kampeni kubwa ya kuwafanya wakaazi kununua bidhaa zinazotengezwa nchini humo.
Waziri wa biashara daktari Ekow Spio Gabrah anaongoza kampeni hiyo na anasema:Nitaendesha moja ya magari haya,kwa kweli niliketia gari moja wakati lilipokuwa likitengezwa na nafurahi kuwa na moja kama gari langu rasmi.
null
Magari aina ya kantanka kutoka Ghana
Waziri na rais wana uwezo wa kuendesha magari hayo kwa gharama ya walipa ushuru.
Lakini je,raia wataweza kutumia fedha zao wenyewe kulipia gharama za kulinunua gari hilo?
Inaonekana kwamba raia wengi kama alivyodai hapo awali Professa wana wasiwasi kuhusu usalama wa gari hilo na kudumu kwake.
null
Gari aina ya kantanka
Je, unadhani wasiwasi huo huenda ukaathiri uzalishaji wa magari hayo? Kulingana na Kwadwo Sarfo gari hilo la kwanza kutengezwa nchini Ghana litapata umaarufu.
                                           Habari na: BBC

Monday, 29 June 2015

U-15 YAICHAPA 3-0, KOMBAINI YA MBEYA

TIMU ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kombaini ya vijana chini ya umri wa 17 ya mkoa wa Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa.
 

Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi dakika 45 za kwanza zilimalizika U15 wakiwa mbele kwa bao 1-0.
 

Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Timoth Maziku dakika ya 17 kwa guu la kulia akimalizia krosi ya Nahodha Issa Abdi.
 

Baada ya bao hilo, Mbeya Kombaini walitulia na kuanza kusukuma mashambulizi langoni mwa timu ya taifa, hali ambayo ilifanya timu hizo zishambuliane kwa zamu huku pia vijana wakionyesha uwezo wa kuridhisha.
 

Dakika ya 72, Albinius Haule almanusra aisawazishie bao Mbeya kama si shuti lake zuri la kitaalamu alilopiga kutoka umbali wa mita 25 kugonga mwamba wa juu na kutoka nje.
Nahodha Issa Abdi aliifungia timu ya taifa bao la pili dakika ya 82 kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya Timoth Maziku kuangushwa nje kidogo ya boksi na Richard Paul.
 

Emmanuel Ntindi wa Mbeya alijifunga dakika ya 87 katika harakati za kuokoa krosi ya Asad Ally dhidi ya Maziku.
 

Mchezo ulikuwa mzuri, vijana walionyesha ufundi wa hali ya juu na Mbeya pamoja na kufungwa, walicheza vizuri na kilichowakwamisha kupata japo bao moja ni uhodari wa kipa Kelvin Deogratius wa U15 ya taifa.
 

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana kesho jioni kwenye Uwanja Sokoine na mapema Jumanne U15 watarejea Dar es Salaam na vijana kuvunja kambi hadi watakapokusanyika tena mwishoni mwa mwezi ujao kwa safari ya Zanzibar kwa michezo mingine ya kujipima.
 

Vijana hao walio chini ya kocha Bakari Shime wanaandaliwa kwa ajili ya kucheza mechi za kufuzu Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2017 na kila wiki ya mwisho wa mwezi watakuwa wakikutana kwa mazoezi na michezo ya kujipima nguvu.

Kikosi cha Mbeya Kombaini kilikuwa; Edward Mwakyusa, Josephat Frank, Seif Gabriel, Emmanuel Ntindi, Richard Paul/Hassam Abdallah dk87, Goodluck Ezeria, Amiri Nyeo, Castro Issa, Albinius Haule, Biya Stephen na Daniel Samson/Castro Moses dk73.
 

Tanzania U15; Kelvin Deogratius, Kibwana Ally, Faraji John, Maulid Salum, Ally Hussein, Athumani Maulid/Rashid Kilomtola dk75, Robert Philipo/Morris Michael ‘Chuji’ dk86, Asad Ally, Timoth Joseph, Issa Abdi na Juma Zubeiry/Juma Juma dk61.
 

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Habari na: http://rweyunga.blogspot.com/

BLACK FIRE MABINGWA KOMBE LA MBUNGE CHIKAWE JIMBO LA NACHINGWEA, MKOANI LINDI

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea akizungumza na wanamichezo (hawapo pichani) kabla ya kuanza fainali ya Kombe la Chikawe katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo na Timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa zilipambana na Timu ya Black Fire iliibuka mshindi kwa magoli 3 kwa 1. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
Kapteni wa Timu ya Black Fire, Ally Njaidi (kulia) akipokea fedha taslimu Shilingi 500,000 pamoja na Kikombe cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema, baada ya kumalizika fainali ya Kombe la Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Timu hiyo iliirarua timu ya Motisha mabao 3 kwa 1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salimu Mwalimu, naye alihudhuria fainali ya mashindano hayo ambayo yalianzishwa na Mbunge Chikawe jimboni humo kwa kushirikisha timu 178 katika jimbo hilo.
  
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea akimsalimia mchezaji wa Timu ya Black Fire, Faraji Mohamed wakati alipokuwa anaikagua timu hiyo kabla ya fainali ya Kombe la Chikawe ambayo yalifanyika katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo iliibuka kidedea baada ya kuinyuka Timu ya Motisha, Kata ya Kilimani magoli 3 kwa 1. Nyuma ya Waziri Chikawe ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.

Kapteni wa Timu ya Motisha, Saidi Chakupewa (kulia) akipokea zawadi ya ushindi wa pili, kikombe na fedha taslimu Shilingi 200,000 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema, baada ya kumalizika fainali ya Kombe la Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Timu hiyo ilifungwa na Timu ya Black Fire mabao 3 kwa 1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salimu Mwalimu, naye alihudhuria fainali ya mashindano hayo ambayo yalianzishwa na Mbunge Chikawe jimboni humo kwa kushirikisha timu 178 katika jimbo hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (aliyevaa kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Black Fire ambao ndio waliibuka washindi. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (aliyevaa kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
Msanii maarufu wa bongofleva, Seleman Jabir ‘Msaga Sumu’ akitumbuiza katika fainali ya Kombe la Chikawe lililofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Katika fainali hiyo, Timu ya Black Fire iliibuka kidedea baada ya kuifunga timu ya Motisha magoli 3 kwa 1.
Mchezaji wa timu ya Black Fire (kulia) akisakata kabumbu katika fainali ya kombe la Mbunge Chikawe lililofanyika katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu hiyo ya Black Fire iliinyuka timu ya Motisha magoli 3 kwa 1. Picha zote na Felix Mwagara.

Saturday, 27 June 2015

Chadema wafurika kurudisha fomu za ubunge

Chadema wafurika kurudisha fomu za ubunge

Katibu wa Chadema Ofisi ya Kanda ya Pwani, Halfan  Milambo akipokea fomu za mtangazania ya kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Ilala kupitia chama hicho, Joyce Charles (katikati) huku akimpongeza kwa kurudisha fomu hizo Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory 
Kwa ufupi
  • Mchakamchaka huo wa kurudisha fomu hizo ulifanyika katika maeneo mbalimbali nchini jana ambayo ilikuwa siku ya mwisho
  • Katika Jimbo la Monduli linaloshikiliwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa tayari makada watatu wamerudisha fomu. Waliorudisha fomu ni Mwenyekiti wa Chadema wa wilaya hiyo Josephat Sironga, Mwenyekiti Baraza la Wanawake (Bawacha) Mkoa wa Arusha, Cecilia Ndosi na Katibu Mwenezi wa chama hicho Monduli, Patrick Ngala ole Mong’i.
Mikoani. Makada mbalimbali wa Chadema jana walirudisha fomu za kuwania kuteuliwa na chama hicho katika nafasi ya ubunge katika majimbo ambayo yanashikiliwa na CCM.
Mchakamchaka huo wa kurudisha fomu hizo ulifanyika katika maeneo mbalimbali nchini jana ambayo ilikuwa siku ya mwisho.
Katika Jimbo la Monduli linaloshikiliwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa tayari makada watatu wamerudisha fomu. Waliorudisha fomu ni Mwenyekiti wa Chadema wa wilaya hiyo Josephat Sironga, Mwenyekiti Baraza la Wanawake (Bawacha) Mkoa wa Arusha, Cecilia Ndosi na Katibu Mwenezi wa chama hicho Monduli, Patrick Ngala ole Mong’i.
Akizungumza jana Mong’i alisema: “Tumechukua fomu sisi watatu na tumerejesha ili kupisha vikao vya maamuzi.”
Mkoani Mbeya makada lukuki wa Chadema mkoani humo walimiminika kurudisha fomu katika muda uliotakiwa huku wengine wengi wakitajwa kucheleweshwa na kazi ya kuweka fedha benki.
Katika Jimbo la Mbarali linaloshikiliwa na Modestus Kilufi (CCM), makada saba walirudisha fomu hadi saa 10.00 jioni muda ambao ulikuwa wa mwisho.
Katibu wa chama hicho wilayani hapo, Nicolaus Lyaumi aliwataja waliorudisha fomu kuwa ni Jidawaya Kazamoyo, Grace Mboka, Dick Baragasi, Tazan Ndingo, Liberatus Mwang’ombe, Rajab Kilemile na Machami Kasambala.
Katika Jimbo la Mbozi Mashariki, linaloshikiliwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi, wanachama 27 wa Chadema walichukua fomu, lakini hadi saa 10.00 jioni, Katibu wa chama hicho, Michael Mwamlima aliwataja waliorudisha kuwa ni Happness Kwilabya, Abraham Msyete, Anastazia Nzowa, Abdul Nindi, Gerald Silwimba, Eliud Msongole, Zablon Nzunda na Eliud Kibona.
Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Wilaya ya Vijijini, Jackson Mwasenga alisema jimbo la wilaya hiyo ambalo linashikiliwa na Mchungaji Luckson Mwanjale (CCM), waliorudisha fomu ni Daud Mponzi, Edson Jisandu, Adam Zela, Anthony Mwaselela Hadson Sheyo, Benson Mwamengo, Stephano Mwandiga, Frank Mwaisumbe Christina Kalisoto, William Msokwa, Elias Songela na Jeremiah Mwaweza.
Katika jimbo la Kwela linaloshikiliwa na Ignas Malocha (CCM), Daniel Ngogo pekee amerudisha fomu jana huku akitaja vipaumbele vinne ambavyo ni elimu, afya, kuboresha miundombinu ya barabara na ajira jimboni kupitia kilimo.
Pia katika jimbo la Sumbawanga Mjini linaloshikiliwa na Aeshi Hilal(CCM) tayari mfanyabiashara wa mjini Sumbawanga, Casiano Kaegele, maarufu kwa jina la Upendo alirudisha fomu ya kuomba kuteuliwa na Chadema kuwania jimbo hilo.
Kaegele alisema amesukumwa na mambo kadhaa kugombea ubunge katika hilo ikiwamo kuanzisha miradi ya wajasiriamali, kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana na wanawake, sambamba na miundombinu hususan uwanja cha ndege.
Katika jimbo la Morogoro Mjini linaloshikiliwa na Mohammed Abood, makada wa 11 walijitokeza kuomba kuteuliwa baadhi yao ni Marcussy Albaine, James Pawa Mabula, Batromeo Tarimo, Esther Tawete, Steven Daza, Doris Kweka, Gerard Temba, Robert Mruge.
Katika jimbo la Kibaha Mjini linaloshikiliwa na Sylivestry Koka (CCM) wanachama sita kati ya saba waliochukua fomu waliorudisha.
Katibu wa Chadema Kibaha Mjini, Michael Nkobi aliwataja waliorudisha kuwa ni Michael Mtally, Joachim Mahenga, Frank Mzoo, Henry Msukwa, Bosco Mfundo na Isihaka Omari.
Katibu wa Chadema Kanda ya Pwani, Khalfan Mirambo alisema Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, waliorudisha fomu za Ubunge jumla yao ni 60 na kati ya hao, 56 ni viti maalumu. Hata hivyo alisema bado majimbo matatu ya Mkuranga, Rufiji na Chalinze.
Imeandikwa na Mussa Juma(Arusha), Godfrey Kahango, Stephano Simbeye na Sylvester Mkombe(Mbeya), Julieth Ngarabali (Kibaha), Mussa Mwangoka (Sumbawanga), Juma Mtanda (Morogoro)
Habari na; http://www.mwananchi.co.tz

RAIS KIKWETE AONGOZA SIKU YA KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA DUNIANI MJINI BAGAMOYO LEO

 RAIS KIKWETE AONGOZA SIKU YA KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA DUNIANI MJINI BAGAMOYO LEO  

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipungia mkono wakati wa kupokea maandamano ya waathirika wa madawa ya kulevya walio katika matibabu kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Dunia ni katika Viwanja vya Taasisi ya sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) mjini Bagamoyo leo Juni 26, 2016.
Wasanii wanafunzi wa Mwaka wa tatu wakichezaa igizo la athari za madawa ya kulevya mbele ya Rais Kikwete wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Dunia ni katika Viwanja vya Taasisi ya sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) mjini Bagamoyo leo Juni 26, 2016.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipena mikono na timu za michezo zilizoshinda michezo ya waathirika wa madawa ya kulevya walio katika matibabu kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Dunia ni katika Viwanja vya Taasisi ya sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) mjini Bagamoyo leo Juni 26, 2016.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mpango wa mawasiliano kuhusu athari za magonjwa mbalimbali hatarishi kupitia simu ya mkononi akiwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Selemani Rashid na Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA) Bw. Peter Masika kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Dunia ni katika Viwanja vya Taasisi ya sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) mjini Bagamoyo leo Juni 26, 2016. PICHA NA IKULU
Habari na:http://rweyunga.blogspot.com

Friday, 26 June 2015

LOWASSA AZIDI KUJIPATIA WADHAMINI LUKUKI, WANACCM 42, 405 WAMDHAMINI MKOANI MANYARA.JUNI 25, 2015


Msafara wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa ukipokelewa kwa shangwe na wanaCCM na Wananchi wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara, wakati alipowasili kwenye mji huo kusaka wadhamini watakaomuwezesha kutapa ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Sehemu ya Wakazi wa Mji wa Babati wakimshangilia Mh. Lowassa pale walipomuona.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa na baadhi la viongozi wa CCM Mkoa wa Manyara wakati alipowasili kwenye Ofisi Kuu za Chama hicho, Mjini Babati leo Juni 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akimsalimia Kijana Jacob Jeremiah ambaye ni mlemavu wa miguu, alipokutana nae nje ya Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Manyara, iliopo Mjini Babari leo Juni 25, 2015, wakati akiwa katika ziara ya kusaka wadhamini watakaomuwezesha kutapa ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha,Onesmo Ole Nangole pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu wakitembea sambamba na wanaCCM wengine kuelekea kwenye uwanja wa CCM Wilaya ya Babati, tayari kwenda kukabidhiwa fomu za Wadhamini, leo Juni 25, 2015.
                                                                                                 Safari ikiendelea.
Mh. Lowassa akisaini kutabu cha Wageni cha Ofisi ya CCM Wilaya ya Babati, Mkoani Manyara.
Muimbaji wa Nyimbo za Injili, Bahati Bukuku akiimba moja ya nyimbo zake wakati akiwasalimia WanaCCM na Wananchi wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara leo Juni 25, 2015.
Sehemu ya WanaCCM na Wananchi wakazi wa Mji wa Babati Mkoani Manyara, wakiwa kwenye Uwanja wa CCM Wilaya ya Babati.
Mjumbe wa NEC kutoka Wilaya ya Mlele, Mkoani Katavi, Kampala Thomas Maganga akiwasalimia wanaCCM wa Mji wa Babati Mkoani Manyara.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akisema neno wakati akiwasalimia wanaCCM na Wananchi wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara leo Juni 25, 2015.
                                                                      WanaCCM wa Babati Mkoani Manyara.
Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Mh. Kiseryi Chambiri akizungumza jambo wakati Mh. Lowassa alipofika kuomba udhanini wa WanaCCM wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara leo Juni 25, 2015.
                                                                                                            Meza kuu.
Tabasamu la Mh. Lowassa baada ya maneno ya Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Mh. Kiseryi Chambiri.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Mh. Kiseryi Chambiri.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Edward Lowassa akipokea fomu ya udhamini kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Babati Mjini, Daniel Ole Porokwa, leo Juni 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 42, 405 wa Mkoa wa Manyara.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Edward Lowassa akizungumza wakati akiwashukuru wanaCCM wa Mkoa wa Manyara, waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Lowassa amepata wadhamini 42, 405 , Mjini Babati Mkoani Manyara leo, Juni 25, 2015.
Habari na: http://rweyunga.blogspot.com