Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea
akizungumza na wanamichezo (hawapo pichani) kabla ya kuanza fainali ya
Kombe la Chikawe katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya
Black Fire kutoka Kata ya Marambo na Timu ya Motisha kutoka Kata ya
Kilimanihewa zilipambana na Timu ya Black Fire iliibuka mshindi kwa
magoli 3 kwa 1. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
Kapteni
wa Timu ya Black Fire, Ally Njaidi (kulia) akipokea fedha taslimu
Shilingi 500,000 pamoja na Kikombe cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya
ya Nachingwea, Pololeti Mgema, baada ya kumalizika fainali ya Kombe la
Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe. Timu hiyo iliirarua timu ya Motisha mabao 3 kwa 1
katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea.
Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Salimu Mwalimu, naye alihudhuria fainali ya mashindano hayo
ambayo yalianzishwa na Mbunge Chikawe jimboni humo kwa kushirikisha timu
178 katika jimbo hilo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea
akimsalimia mchezaji wa Timu ya Black Fire, Faraji Mohamed wakati
alipokuwa anaikagua timu hiyo kabla ya fainali ya Kombe la Chikawe
ambayo yalifanyika katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya
Black Fire kutoka Kata ya Marambo iliibuka kidedea baada ya kuinyuka
Timu ya Motisha, Kata ya Kilimani magoli 3 kwa 1. Nyuma ya Waziri
Chikawe ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
Kapteni
wa Timu ya Motisha, Saidi Chakupewa (kulia) akipokea zawadi ya ushindi
wa pili, kikombe na fedha taslimu Shilingi 200,000 kutoka kwa Mkuu wa
Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema, baada ya kumalizika fainali ya
Kombe la Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mathias Chikawe. Timu hiyo ilifungwa na Timu ya Black Fire mabao 3
kwa 1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini
Nachingwea. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Salimu Mwalimu, naye alihudhuria fainali ya
mashindano hayo ambayo yalianzishwa na Mbunge Chikawe jimboni humo kwa
kushirikisha timu 178 katika jimbo hilo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (aliyevaa kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Black
Fire ambao ndio waliibuka washindi. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa
Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (aliyevaa kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Motisha
kutoka Kata ya Kilimanihewa. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya
Nachingwea, Pololeti Mgema.
Msanii
maarufu wa bongofleva, Seleman Jabir ‘Msaga Sumu’ akitumbuiza katika
fainali ya Kombe la Chikawe lililofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini
Nachingwea. Katika fainali hiyo, Timu ya Black Fire iliibuka kidedea
baada ya kuifunga timu ya Motisha magoli 3 kwa 1.
Mchezaji
wa timu ya Black Fire (kulia) akisakata kabumbu katika fainali ya kombe
la Mbunge Chikawe lililofanyika katika Uwanja wa Sokoine, mjini
Nachingwea. Timu hiyo ya Black Fire iliinyuka timu ya Motisha magoli 3
kwa 1. Picha zote na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment