Wasichana wa Chibok washinikizwa kuua
Shirika
la Utangazaji la Uingereza, BBC limeelezwa kuwa baadhi ya wasichana
waliotekwa na wanamgambo mjini Chibok Nigeria wamekuwa wakishinikizwa
kuwaua Wakristo.
Wanawake watatu ambao wanasema walikuwa
wakishikiliwa katika kambi moja na wasichana hao wanasema wapiganaji wa
BOKO HARAM waliwafunga mikono wanaume wa Kikristo. Wasichana hao
waliwachinja wanaume hao kwa kuwakata shingo.Wanawake hao wanasema baadhi ya wasichana hao wa Chibok walikuwa na silaha. Baadhi ya wasichana waliwachapa mateka wengine wa kike. Haikuwa rahisi kuthibitisha ukweli wa taarifa hii. Wasichana 219 kati ya zaidi ya wasichana 270 waliotekwa kutoka shule moja ya bweni ya Chibok bado wanashikiliwa na Boko Haram.
Habari na: BBC
No comments:
Post a Comment