Moto waunguza Msikiti wa Omary Bin Hatwah uliopo karibu na jengo la Yanga
Baada ya Msikiti kuwa umeungua na huyu raia mwema akiwa anaangalia na kujaribu kukagua vizuri vitu vilivyoungua.
Msikiti uliopo jijini Dar es Salaam eneo la kariakoo mtaa wa jangwani na twiga umeungua moto leo mnamo majira ya saa kumi na moja kasoro.
Chanzo cha moto huo hakikufahamika mara moja ingawa watu wengi waliuwa wanahisi kwamba pengine utakuwa umesababishwa na umeme.
Moto huo umeleta madhala makubwa ikiwa pamoja na kuunguza matanki ya maji, vitabu vya dini, makapeti, mabati, feni, na mtu mmoja alionekana kupata majeraha ya moto mguuni, vioo vya madilisha vilivunjwa ili kuokoa baadhi ya vifaa vya msikitini.
Watu wa zima moto walichelewa kufika ingawa ofisi zao zipo karibu na eneo la tukio walitumia kama dakika 45.
Watu waliokuwepo eneo la tukio waliokuwa wanasaidia kuzima moto walitoa lawama zao kwa zima moto kwa kuchelewa kufika na kwa raia ambao sio wema waliokuwa wakijaribu kuiba badala ya kuokoa.
Habari hii imeletwa kwenu na Hatasisitupo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment