Thursday, 25 June 2015

LOWASSA APATA UDHAMINI WA KISHINDO JIJINI ARUSHA LEO, WANACCM 120,335 WAMDHAMINI

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (wa tatu kulia) sambamba na Mkewe Mama Regina Lowassa, wakiongozana na viongizi mbali mbali wa Chama wa Mkoa wa Arusha waliofika kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa KIA, wakati akitokea Mkoani Dodoma kuhudhulia vikao cha Bunge na kupigia kura bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na Waumini wa Kanisa la International Evangelical Church (hawapo pichani).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM wa Mkoa wa Arusha waliomdhamini ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini, Ferouz Bano, ambapo WanaCCM wapatao 120, 335 wamemdhamini Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akikabidhi sehemu ya fomu hizo kwa Mkewe Mama Regina Lowassa. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM jijini Arusha, Ndg.Onesmo Ole Nangole.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia WanaCCM wa Mkoa wa Arusha waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Msikiti Mkubwa uliopo mbele ya Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha, leo Juni 24, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akimjulia hali Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM, Mathias Manga, aliyejeruhiwa kwa risasi jana usiku na watu wasiofahamika, wakati walipokutana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa KIA, Mkoani Kilimanjaro leo Juni 24, 2015.
Sehemu ya Wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaoishi maeneo ya jirani na Uwanja wa Ndege wa KIA wakimshangilia Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa wakati walipomsimamisha ili aweze kuwasalimia leo Juni 24, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Sioi Sumary.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya madakrari wa kigeni wanaotoa huduma kwenye hospitali ya Kanisa na International Evangelical Church, lililopo katika Kijiji cha Sakila, Wilayani Arumeru jijini Arusha. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu Eliud Isanja.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwapungua mkoni ikiwa ni ishara ya kuwasalimia waumini wa Kanisa na International Evangelical Church, waliomualika leo Juni 24, 2015 ili aweze kuzungumza nao pamoja na kufanyiwa ibada maalum ya kumuombea.
Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelical Church, Askofu Eliud Isanja akizungumza jambo wakati akimtambulisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa kwa waumini wa kanisa hilo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Mkewe, Mama Regina Lowassa kabla ya kufanyiwa Ibada maalum ya kumuombea Mh. Lowassa katika Kanisa la International Evangelical Church, lililopo katika Kijiji cha Sakila, Wilayani Arumeru jijini Arusha.
Sehemu ya Maaskofu wa Kanisa la International Evangelical Church, wakimuombea Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa, leo Juni 24, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiagana na Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelical Church, Askofu Eliud Isanja.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwa safarini kuelekea Jijini Arusha, mara msafara wake ukasimamishwa na WanaCCM wa Mji wa Maji ya Chai Wilayani Arumeru waliotaka kumsalimia.
Dereva wa Daladala uzalendo ukamsinda kwenye usukani na kuamua kukaa Dirishani ili aweze kumuona Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa alishuka kwenye gani na kuungana na WanaCCM hao.
Msafara wa Mh. Lowassa ulizuiwa tena eneo la Tengeru, Jijini Arusha baada ya WanaCCM wa Mji huo kufunga barabara ili waweze kuzungumza na kipenzi chao.
Mh. Lowassa akiwapungia mkono WanaCCM hao wa Mji wa Tengeru waliokuwa wamefurika kwa wingi barabarani.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mwenyekiti wa CCM jijini Arusha, Ndg.Onesmo Ole Nangole pamoja na WanaCCM wengine, wakati wakielekea kwenye Uwanja wa Msikiti Mkubwa, kulikoandaliwa shughuli nzima ya kukabidhiwa fomu za kumdhamini Mh. Lowassa ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla ya WanaCCM 120, 335 wa jiji la Arusha wamemdhamini Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wanaCCM na Wananchi wa Jiji la Arusha waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Msikiti Mkubwa uliopo mbele ya Ofisi za CCM Mkoa wa Arusha, leo Juni 24, 2015. Jumla ya WanaCCM 120, 335 wa jiji la Arusha wamemdhamini Mh. Lowassa.
Baadhi ya Wazee wa Kabila la Kimasai wakimbariki Mh. Lowassa katika Safari yake ya Matumaini.

Mbunge wa Arumeru Magharibi, Mh. Goodluck Ole Mideye akiwasalimia wanaCCM wa Mkoa wa Arusha.
Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Namelock Sokoine akiwasalimia WanaCCM wa Arusha.
Umati wa Watu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Hamis Mngeja akisalimia.
Sehemu ya WanaCCM wa Mkoa wa Arusha wakionekana ni wenye Furaha na Imani Kubwa na Mh. Lowasaa.
Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Arumeru, Mathias Manga akisalimia.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisikiliza jambo kutoka kwa Mkewe, Mama Regina Lowassa.
Mwenyekiti wa CCM jijini Arusha, Ndg.Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia kuzungumza na WanaCCM wa Mji wa Arusha.
 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akimpa pole Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM, Mathias Manga, aliyejeruhiwa kwa risasi jana usiku na watu wasiofahamika, wakati alipomwita jukwaani kuwasalimia WanaCCM wa Arusha.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Jiji la Arusha waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa ulipo mbele ya Ofisi za CCM Mkoa huo, leo Juni 24, 2015, wakati alipofika kwa ajili ya kupata udhamini utakaomuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
 
Mh. Lowassa akiwaaga WanaCCM wa Mji wa Arusha.
Habari na: http://rweyunga.blogspot.com
You might also like:

No comments:

Post a Comment