BILIONEA DANGOTE ALIRIDHIA UJENZI WA BANDARI YAKE MTWARA KWA KUSHIRIKIANA NA TPA
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote,
akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa
Ghasia alipowasili kwenye uwanja wa Ndege mjini Mtwara jana kwa ajili ya
kutembelea kiwanda chake cha Cementi kilichoko Msijute, mkoani Mtwara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Hawa Ghasia akiteta jambo
na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote,
alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara leo kwa ajili ya kuangalia
maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Cementi cha Dangote. Katikati ni
Balozi wa Nigeria Nchini Tanzania, Ishaya Manjanbu.
Mkurugenzi wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote (kulia),
akijadiliana jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban
Mwinjaka, walipokutana mjini Mtwara jana kuangalia uwezekano wa kujenga
kituo cha kusafirisha saruji katika eneo la Bandari ya Mtwara.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, akizungumza na
waandishi wa habari baada kuwasili mjini Mtwara jana na kutembelea
kiwanda chake cha Cementi, kilichoko Msijute, mkoani Mtwara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote
akisaini kitabu cha wageni, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege
mjini Mtwara jana, kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda
chake cha saruji. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban
Mwinjaka.
Mkurugenzi wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote akiwafuatana na
wenyeji wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Hawa Ghasia (wa pili
kushoto), Balozi wa Nigeria, Ishaya Manjanbu (wa pili kulia) na Mkuu wa
Wilaya ya Mtwara, Bi. Fatma Salum Ali (kushoto), alipowasili kwenye
uwanja wa ndege, mjini Mtwara jana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote, akiteta jambo na
Mwakilishi mkazi wa Dangote nchini Tanzania, Bi. Esther, mjini Mtwara ,
baada ya Mkurugenzi huyo kutembelea kiwanda chake cha saruji
kinachojengwa mkoni Mtwara.
Habari na: http://rweyunga.blogspot.com
No comments:
Post a Comment