Akamatwa akitafuta mteja wa mtoto albino
Na Robert Kakwesi
Kwa ufupi
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Juma Bwire
alimtaja mtuhumiwa huyo aliyekamatwa juzi kuwa ni Masanja Mwinamila
(44), mkazi wa Ugembe wilayani Nzega.
Tabora. Mtu mmoja amekamatwa na polisi akiwa katika harakati za kutafuta soko la kuuza mtoto mdogo wa dada yake ambaye ana ulemavu wa ngozi mwenye umri wa miaka sita.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Juma Bwire
alimtaja mtuhumiwa huyo aliyekamatwa juzi kuwa ni Masanja Mwinamila
(44), mkazi wa Ugembe wilayani Nzega.
Kamanda Bwire alisema polisi walipata taarifa za
mtuhumiwa huyo kutafuta wateja ndipo askari walipoweka mtego kwa
kujifanya wanunuzi na kukubaliana naye kufanya biashara kwa kiwango cha
fedha alichohitaji na kudai kwamba mtuhumiwa alitekeleza makubaliano
hayo na kwenda kumchukua mtoto huyo akiwa na mama yake na ndipo askari
walipomtia mbaroni. Kamanda Bwire alieleza kuwa mtuhumiwa huyo
atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Kamanda Bwire alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo
ni mkakati maalumu unaoendelea kufanywa na polisi kuwalinda watu wenye
ulemavu wa ngozi.
Mama mzazi wa mtoto huyo, Joyce Mwandu alieleza
kuwa kaka yake alifika nyumbani kwake na kudai kuwa amekwenda
kumtembelea na baada ya muda alitokomea na mtoto hadi alipopata taarifa
za kukamatwa kwake.
No comments:
Post a Comment