Kiungo mshambuliaji wa Barcelona Neymar Da Silva Jr vamekuwa kwenye kiwango cha juu msimu huu ambapo amekuwa sehemu muhimu sana ya timu yake katika michezo ya hivi karibuni .
Neymar amedhihirisha ubora wake kwa jinsi ambavyo amekuwa akifunga mabao mfululizo huku akisaidia kwa kutoa pasi za mwisho kwa wenzie na amekuwa akifanya hivyo kwa mwendelezo mzuri ,
Tatizo limekuwa moja tu , jinsi amabvyo mchezaji huyu amekuwa akilaumiwa hasa na wapinzani kwa kuwa mtovu wa nidhamu na mkosefu wa heshima ambapo amekuwa akiwadhihaki wachezaji wa timu pinzani kwenye nyakati tofauti hali ambayo imeonekana kuwakera wengi .
Neymar amekuwa na tabia ya kuwatukana wachezaji wa timu pinzani na wakati mwingine hata kwa vitendo na ndio maana amekuwa kwenye vurugu nyingi ambazo zimekuwa zikitokea kwenye michezo ya Fc Barcelona .
Majuzi wakati wa mchezo war obo fainali ya michuano ya Kombe la Mfalme ambapo Barcelona ilishinda kwa 3-2 Neymar alikuwa kwenye fujo zilizoibuka kati yake na wachezaji wa Atletico ambao ni Gabi , Juan Fran na Raul Garcia.
Ilifikia mpaka kocha Luis Enrique alilazimika kumtoa uwnajani ambapo baadae alikir kufanya hivyo kwa lengo la kumlinda .
Hivi karibuni Luis Enirque alisikika akisema kuwa Neymar anapaswa kujiheshimu na kuwaheshimu wapinzani na kama asipofanya hivyo huenda akafanywa ‘chambo’ na kuumizwa na wachezaji wa timu pinzani ambao wamejawa na hasira juu yake .
Tabia hii ya Neymar itawakumbusha wengi juu ya kile kilichokuwa kinafanywa na Ronaldinho Gaucho wakati akiwa na klabu hii ya Barcelona ambapo aliripotiwa kuwadhihaki na kuwatusi wapinzani huku akiendelea kuwakera kwa chenga zake za maudhi .
Credit:Millardayo.