Friday, 30 January 2015

Baba ajiua kutokana na picha za mwanawe

Loredana Chivu ni mwanamitindo nchini Romania
Baba mmoja amejiua baada ya kuona picha za uchi zamwanawe wa kike katika jarida la Playboy nchini Romania.
Loredana Chivu alirarua ukurasa uliokuwa na picha yake akiwa 'amepos' katika jarida hilo la Playboy na punde babake alipogundua kuhusu picha hizo, alizongwa na mawazo na hata kumkana mwanawe.
Kwa mujibu wa mtandao wa Mirror, msichana huyo mwenye umbo la kuvutia alisema, '' babangu aliacha kuongea na mimi na kuonekana mwenye hasira sana''.
"alipogundua kuwa picha hizo zilikua zangu, alijitenga sana na kujaribu kunitenga na mimi''.
Nilidhani labda angesahau na sikudhani hata siku moja angejitoa uhai.
Loredana Chivu anasema anajuta sana kwani babake hakuwahi kuongea naye baada ya kupata picha zake
Mwanamitindo huyo Loredana Chivu mwenye mamia ya picha akiwa nusu uchi kwenye akaunti yake ya Instagram, alikuwa na uhusiano wa karibu sana na babake lakini alisema yote hayo yalibadilika baada ya babake kuona picha zake akiwa nusu uchi.
Alipokwenda kumtembelea babake miezi michache baadaye, baada ya kuamua kwamba kimya kilikuwa kimeendelea kwa muda mrefu sana, alishtuka sana kumpata babake akiwa amejitoa uhai
"nilipata akiwa na kamba shingoni akiwa ananing'inia chumbani''.
Loredana,anayeishi nchini Romania, anasema kuwa tangu kifo cha babake, amekuwa akiwaza na kuwazua kwamba aliamua kujiua kwa sababu ya mgogoro kati yetu na hasa kuhusu picha zangu zilizoziona kwenye jarida la Playboy.
''Najuta sana kwamba hakuwahi kupata muda wa kuzungumza na babangu kuhusu yaliyotokea''.
''Hakuwacha ujumbe wowote kabla ya kujitoa uhai, siku zote tulikuwa na uhusiano mzuri lakini yote yalibadilika baada ya baba kuona picha zangu nikiwa uchi. Bado inaniuma sana na singemtakia mtu yeyote kupatwa na kama yaliyonikuta''.

No comments:

Post a Comment