huu ndio mtaro wa maji kwaajili ya kufua umeme kata ya Kilondo
Filikunjombe akipata maelezo kuhusiana na ujenzi wa mradi huo
Ujenzi wa
mradi wa umeme wa kutumia maji kwa ufadhiri wa REA katika kata ya Kilondo
wilayani Ludewa mkoa wa Njombe umeanza kuleta matumaini baada ya hatua ya awali
kukamilika ambayo ni ujenzi wa njia ya maji na nyumba ya kufunga mtambo wa
kufua umeme kukamilika.
Hivi
karibuni mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe aliweza kutembelea mradi
huo ambao uko mwambao wa ziwa Nyasa na kujionea maendeleo yake ambapo aliweza
kuwashukuru wananchi kwa kushirikiana na wakandarasi wa mradi huo.
Filikunjombe
alisema kuwa wakati wa utawala wake yeye kama mbunge Serikali kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali imeweza kuanzisha miradi ya umeme katika vijiji 67 wakati
wilaya ya Ludewa inajumla ya vijiji 77 hivyo ni vijiji 10 tu ndivyo vitakuwa
havina nishati ya umeme lakini juhudi za kukamilisha miradi hiyo na
kuhakikivijiji vyote vya wilaya ya Ludewa vinakuwa na nishati hiyo zinaendelea.
Aidha
aliwataka wananchi wa wilaya ya Ludewa katika vijiji hivyo 67 kushirikiana
kikamirifu na wawekezaji hasa wataalamu wa miradi hiyo ili kuhakikisha miradi
hiyo inakamirika haraka kwa muda uliopangwa na Serikali.
“nawaomba
wananchi wa jimbo langu kushirikiana kikamirifu bila kujari itikadi za vyama
vyenu kufanya kazi na wawekezaji hasa hawa wataalamu wa miradi hii ya umeme
ambao wanafanya kazi ngumu katika maeneo yetu na tuondoe dhana potofu ya kuwa
hizi kazi ni za Serikali wakati umeme tutautumia sisi wananchi ambao ndio
Serikali yenyewe”,alisema Filikunjombe.
Naye mmoja
wa wananchi wa kata hiyo Bw.George Mwakipokile alisema kuwa wananchi wamekuwa
wakishirikiana kikamirifu na mafundi wa
kazi hiyo katika kila hatua kwani ni jambo la kimaendeleo kupata nishati hiyo
Kilondo awali hakuna hata mtu mmoja ambaye alifikiria siku moja kata ya Kilondo
ingeweza kuwa na umeme.
Bw.Mwakipokile
alisema kuwa wananchi wanamshukuru mbunge wao ambye ni Filikunjombe kwa
kushirikiana na Bw.Mwambeleko kubuni mradi huo wenye tija kwa jamii ya
wanaludewa kwani mradi huo ni mkubwa na unauwezo wa kusambaza umeme huo katika
kata zote za mwambao wa ziwa Nyasa.
Mwisho.
Habari na:http://habariludewa.blogspot.com
No comments:
Post a Comment