Maafisa wa Indonesia wamesema miili
ya watu 144 imepatikana, baada ya ndege ya usafirishaji mizigo ya
jeshi kuanguka katika makazi ya watu katika eneo la Medan, hapo jana.
Jeshi limesema hakuna hata mtu mmoja
kati ya 122 waliokuwemo kwenye ndege hiyo aina ya Hercules C-130
aliyenusurika kifo baada ya kuanguka na kugonga nyumba pamoja na
hoteli na kisha kulipuka moto.
Wengi wa waliokufa inaaminika kuwa
ni ndugu na jamaa wa wanajeshi wa Indonesia. Taarifa za hivi karibuni
zimesema watu 19 waliokuwa kwenye nyumba wamekufa.
Habari na: http://rweyunga.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment