MASKINI:MUONE HUYU PADRE NA WANAFUNZI SITA WALIVYOTETEKETEA KWA MOTO
WANAFUNZI sita wa Sekondari ya CTC
Kigonsera inayomilikiwa na Misheni ya Mbinga mkoani Ruvuma na Mkuu wa
Shule hiyo, Padre Yazint Kawonga, wamefariki dunia baada ya gari
walilokuwa wakisafiria kutumbukia bondeni kisha kuwaka moto na
kuiteketeza miili yao.
Akizungumza na Mpekuzi juzi shuhuda
wa ajali hiyo, Makarius Nchimbi, alisema ilitokea juzi saa tisa alasiri
katika mlima uliopo karibu na shule hiyo huku likiwa limewabeba
wanafunzi waliokuwa wakitokea shambani kuvuna mahindi ya shule hiyo.
Nchimbi ambaye ni mfanyakazi wa
kitengo cha udereva katika misheni hiyo alidai yeye ndiye aliyekuwa
dereva wa gari hilo kabla ya kupokelewa na Padre Kawonga aliyemtaka
amsaidie kuliendesha kwa kuwarudisha shuleni wanafunzi waliokuwa shamba
lililopo Kijiji cha Mkulumus kilichopo Kigonsera.
Alisema gari hilo aina ya Land
Rover 110 Station Wagon lenye namba T 306 AYM lilipofika katika mlima
huo lilimshinda Padre Kawonga wakati akitumia gia namba mbili na kuanza
kurudi nyuma huku wanafunzi wengine waliokaa juu walifanikiwa kuruka
kabla halijatumbukia na baadhi yao 24 waliumia.
Alisema baada ya gari hilo
kutumbukia bondeni wao walijitahidi kuingia kwenda kuvunja milango ili
waweze kuwaokoa baadhi yao lakini ilishindikana kutokana na nyaya za
umeme wa gari kulipuka na kuliunguza huku miili yao ikiwemo ndani na
kusababisha ishindwe kutambulika.
Alisema kutokana na moto kuwaka
iliwalazimu watafute mbinu za kuuzima na walitumia maji lakini
haikuwezekana na walifanya jitihada ya kuipata winchi iliyoweza kwenda
kuliinua gari hilo likiwa limeteketea.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa
Kituo cha Afya cha Kigonsera, Dk. Patrik Mhagama, alisema kituo hicho
kilipokea maiti saba na majeruhi wakiwa 24 na kati ya hao wawili
wamepekwa Hospitali ya Mbinga kutokana na hali zao kuwa mbaya huku 17
walitibiwa na kuruhusiwa na watano bado wapo kituoni hapo.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ruvuma, Mihayo Msikihela, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na
alisema taratibu za kuyapata majina halisi ya marehemu bado zinaendelea
na zikikamilika zitatolewa taarifa.
Aliwataja majeruhi hao kuwa ni
Japheth Komba (16), Regobert Mahai (16), Edgar Maseko (16), Luiza
Mbunda, Afa Kifaru (15), Nelalfred Nchimbi (16), Teodora Wolfa (16).
Habari na Masama blog
No comments:
Post a Comment