Lifti Muhimbili zazua kasheshe
Na Pamela Chilongola
Kwa ufupi
Wauguzi watumia ngazi kupanda na kushuka na maiti, wagonjwa. Kaimu mkurugenzi akiri lifti kutofanyakazi
Pia, wauguzi hao wanalazimika kuzibeba maiti
kutoka wodini na kuzipeleka kwenye chumba cha kuhifadhi kupitia ngazi za
hospitali hiyo kutokana na tatizo hilo la lifti na kuwasababishia adha
kubwa.
“Kuharibika kwa lifti hizi kwa zaidi ya mwezi sasa
kunasababishia kufanya kazi katika mazingira magumu hasa ya utoaji
huduma kwa wagonjwa na ubebaji wa maiti,” alisema jana mmoja wa wauguzi
wa wodi ya Kibasila, Afred Ismail.
Alisema mgonjwa mahututi akipelekwa kwenye wodi
hiyo anatakiwa kulazwa chumba namba 16 ambacho kipo gorofa ya tatu
wanalazimika kumweka chumba cha upasuaji ambacho kipo chini na
kusababisha kutotibiwa kwa wakati.
“Wauguzi tuna wakati mgumu wa kazi, utakuta
mgonjwa anatakiwa alazwe kwenye chumba namba 16 kutokana na lifti kuwa
mbovu, tunashindwa kumpandisha kwenye ngazi hadi hapo tutafute watu
zaidi ya saba wa kumbeba ili akapatiwe matibabu,” alisema Ismail.
Muuguzi Edita Amandous alisema wanapata wakati
mgumu hasa mgonjwa anapofariki kwani kumtoa ghorofa ya tatu na kumshusha
chini ili kumpeleka kwenye chumba cha mahututi wanalazimika kumbeba
watu zaidi ya 10 kushuka kwenye ngazi.
Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Dk Hussein Kidanto
alisema hospitali hiyo ilijengwa miaka mingi iliyopita hivyo wanampango
wa kuboresha wodi ya Kibasila, Mwaisela na Sewahaji ila wanasubiria
fedha zilizotengwa kwa ajili ya hospitali hiyo.
Dk Kidanto alisema, suala la lifti ni tatizo kubwa
hasa kwenye wodi ya Kibasila na Sewahaji hivyo uongozi wa hospitali
hiyo wamekuwa wakitengeneza kwa gharama kubwa kutokana na kuwa chakavu
kila wakati zimekuwa zikiharibika.
“Hizi lifti kila wakati tunazitengeneza na
tunatumia gharama kubwa sana lakini sasa hivi tumejipanga kununua mpya
na tunampango wa kujenga wodi ya ghorofa 10 ambayo itaondoa hii
changamoto,” alisema Dk Kidanto.
Alisema changamoto zinazojitokeza zinasababishwa
na ufinyu wa bajeti, hivyo fedha inayotengewa hospitali hiyo ni ndogo na
kusababisha kushindwa kuboresha majengo na kununua vifaa vya hospitali
hiyo.
Habari kutoka: Gazeti la Mwananchi
Habari kutoka: Gazeti la Mwananchi
No comments:
Post a Comment