SAMATTA AFUNGA, LAKINI SFAXIEN YAIUA MAZEMBE DAKIKA YA 88 LUBUMBASHI, WAMKOSA MWALI WA CAF HIVI HIVI!
MSHAMBULIAJI
Mbwana Ally Samatta na Thomas Emanuel Ulimwengu leo wameshindwa
kutimiza ndoto zao za kuwa Watanzania wa kwanza kuvaa Medali za Dhahabu
za michuano ya Afrika baada ya klabu yao, Tout Puissant Mazembe kushinda
2-1 dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia, katika fainali ya pili ya Kombe la
Shirikisho Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, hivyo kuangushwa kwa
matokeo ya jumla ya 3-2, baada ya awali kufungwa 2-0 Uwanja Olympique de
Rades mjini Tunis katika Fainali ya kwanza.
Mazembe
ilitakiwa kushinda mabao 3-0 leo nyumbani ili kutwaa taji hilo, na
ilionekana kama ingeweza kufanya hivyo baada ya kuongoza kwa mabao 2-0
hadi dakika ya 88, yaliyofungwa na nyota wa Mali, Traore Cheibane dakika
ya 10 na Samatta dakika ya 24.
Lakini
wakati Mazembe wakiwa bize na mashambulizi ya kusaka bao la tatu dakika
za lala salama, Ben Youssef akaifungia bao muhimu Sfaxien dakika ya 88
na kuzima ndoto za akina Samatta kuvaa Medali za Dhahabu za Kombe la
Shirikisho.
Katika
mchezo wa kwanza, mabao yaliyoizamisha Mazembe yalifungwa na
washambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Ibrahim Didier Ndong aliyefunga bao
la kwanza dakika ya 16 na mshambuliaji Taha Yassine Khenissi aliyefunga
la pili dakika ya 90 na ushei wakimtungua kipa mahiri, Robert Muteba
Kidiaba.
Washambuliaji
wote wa Tanzania, Samatta na Ulimwengu walianza katika kikosi cha
Mazembe pamoja na Tressor Mputu Mabi, lakini hawakuweza kuwanusuru
mabingwa mara nne Afrika na kipigo hicho.
Sfaxien,
timu pekee iliyoshinda Kombe la Shirikisho mara mbili tangu
kutambulishwa kwa mfumo mpya mwaka 2004, yenye maskani yake katika mji
uliozungukwa na bahari ya Mediterranean, Sfax kwa ushindi huo
itazawadiwa kitita cha dola za Kimarekani, 625 000, wakati Mazembe
watapata dola 432 000.
Sfaxien
pia watamenyana na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Al Ahly ya Misri
kuwania taji la Super Cup mechi itakayopigwa nchini Misri Februari 2014.
Wachezaji
waliokuwa wakiunda kikosi cha Simba SC mwaka 1993 walivalishwa Medali
za Fedha pia na Rais mstafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi
baada ya kufungwa mabao 2-0 na Stellah Abidjan ya Ivory Coast mwaka 1993
katika fainali ya pili ya Kombe la CAF Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Awali, Simba ilitoa sare ugenini na kuwapa matumaini Watanzania kwamba taji la kwanza kubwa Afrika lingetua nchini mwaka 1993.
Baada
ya mchezo huo, Samatta na Ulimwengu watapanda ndege kesho kuelekea
Nairobi, Kenya kuungana na kikosi cha Bara, Kilimanjaro Stars
kinachoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Challenge.
No comments:
Post a Comment